The chat will start when you send the first message.
2Msimamizi wa kikosi cha kwanza kwa mwezi wa kwanza alikuwa Yashobeamu mwana wa Zabdieli. Kulikuwa na watu elfu ishirini na nne katika kikosi chake.
3Yeye alikuwa mzao wa Peresi, na mkuu wa maafisa wote wa jeshi kwa mwezi wa kwanza.
4Msimamizi wa kikosi kwa mwezi wa pili alikuwa Dodai Mwahohi. Miklothi ndiye alikuwa kiongozi wa kikosi chake. Kikosi chake kilikuwa na watu elfu ishirini na nne.
5Jemadari wa kikosi cha tatu kwa mwezi wa tatu alikuwa Benaya mwana wa kuhani Yehoyada. Ndiye alikuwa mkuu wa kikosi chake kilichokuwa na watu elfu ishirini na nne.
6Huyu ndiye yule Benaya aliyekuwa shujaa miongoni mwa wale Thelathini, na ndiye alikuwa juu ya wale Thelathini. Mwanawe Amizabadi ndiye alikuwa mkuu katika kikosi chake.
7Jemadari wa nne kwa mwezi wa nne alikuwa Asaheli nduguye Yoabu, mwanawe Zebadia ndiye aliingia mahali pake kwenye uongozi. Kikosi chake kilikuwa na watu elfu ishirini na nne.
8Jemadari wa kikosi cha tano kwa mwezi wa tano alikuwa Shamhuthi Mwizrahi. Kikosi chake kilikuwa na watu elfu ishirini na nne.
9Jemadari wa kikosi cha sita kwa mwezi wa sita alikuwa Ira, mwana wa Ikeshi Mtekoa. Kikosi chake kilikuwa na watu elfu ishirini na nne.
10Jemadari wa kikosi cha saba kwa mwezi wa saba alikuwa Helesi Mpeloni wa Waefraimu. Kikosi chake kilikuwa na watu elfu ishirini na nne.
11Jemadari wa nane kwa mwezi wa nane, alikuwa Sibekai Mhushathi wa Wazera. Kikosi chake kilikuwa na watu elfu ishirini na nne.
12Jemadari wa tisa kwa mwezi wa tisa alikuwa Abiezeri Mwanathothi wa Wabenyamini. Kikosi chake kilikuwa na watu elfu ishirini na nne.
13Jemadari wa kumi kwa mwezi wa kumi alikuwa Maharai Mnetofathi wa Wazera. Kikosi chake kilikuwa na watu elfu ishirini na nne.
14Jemadari wa kumi na moja kwa mwezi wa kumi na moja alikuwa Benaya Mpirathoni wa Waefraimu. Kikosi chake kilikuwa na watu elfu ishirini na nne.
15Jemadari wa kumi na mbili kwa mwezi wa kumi na mbili alikuwa Heldai Mnetofathi kutoka jamaa ya Othnieli. Kikosi chake kilikuwa na watu elfu ishirini na nne.
Kwa Wareubeni: Eliezeri mwana wa Zikri;
kwa Wasimeoni: Shefatia mwana wa Maaka;
17kwa Walawi: Hashabia mwana wa Kemueli;
kwa Haruni: Sadoki;
18kwa Yuda: Elihu, nduguye Daudi;
kwa Waisakari: Omri mwana wa Mikaeli;
19kwa Wazabuloni: Ishmaya mwana wa Obadia;
kwa Wanaftali: Yeremothi mwana wa Azrieli;
20kwa Waefraimu: Hoshea mwana wa Azazia;
kwa nusu ya kabila la Manase: Yoeli mwana wa Pedaya;
21kwa nusu nyingine ya kabila la Manase huko Gileadi: Ido mwana wa Zekaria;
kwa Wabenyamini: Yaasieli mwana wa Abneri;
22kwa Wadani: Azareli mwana wa Yerohamu.
23Daudi hakuwahesabu watu waliokuwa chini ya miaka ishirini, kwa sababu Bwana alikuwa ameahidi kuwafanya Israeli kuwa wengi kama nyota za angani.
24Yoabu mwana wa Seruya alianza kuwahesabu watu lakini hakumaliza. Kwa sababu ya kuwahesabu watu, hasira ya Mungu iliwaka juu ya Israeli, nayo hiyo hesabu yao haikuingizwa katika kitabu cha kumbukumbu za Mfalme Daudi.
25Azmawethi mwana wa Adieli ndiye alikuwa msimamizi wa hazina za mfalme.
Msimamizi wa hazina katika mashamba, miji, vijiji na kwenye ngome alikuwa Yonathani mwana wa Uzia.
26Ezri mwana wa Kelubu alikuwa msimamizi wa wafanyakazi waliolima katika mashamba.
27Shimei Mramathi alikuwa msimamizi wa mashamba ya mizabibu.
Zabdi Mshifmi alikuwa msimamizi wa zabibu, utengenezaji na uhifadhi wa divai katika mapipa makubwa.
28Baal-Hanani Mgederi ndiye alikuwa mwangalizi wa mashamba ya mfalme ya mizeituni na mikuyu katika tambarare za vilima vya magharibi.
Yoashi alikuwa msimamizi wa maghala ya mafuta ya zeituni.
29Shitrai Msharoni alikuwa msimamizi wa mifugo waliolishwa huko Sharoni.
Shafati mwana wa Adlai alikuwa msimamizi wa mifugo iliyokuwa makondeni.
30Obili Mwishmaeli alikuwa msimamizi wa ngamia.
Yedeya Mmeronothi alikuwa msimamizi wa punda.
31Yazizi Mhagri alikuwa msimamizi wa makundi ya kondoo na mbuzi.
32Yonathani mjomba wa Daudi alikuwa mshauri, mtu mwenye ufahamu mkubwa na mwandishi.
Yehieli mwana wa Hakmoni alikuwa akiwahudumia wana wa mfalme.
33Ahithofeli alikuwa mshauri wa mfalme.
Hushai Mwarki alikuwa rafiki wa mfalme.
Yoabu alikuwa jemadari wa majeshi ya mfalme.