The chat will start when you send the first message.
1Katika mwaka wa kumi na nane wa utawala wa Yeroboamu, Abiya akawa mfalme wa Yuda,
2naye akatawala huko Yerusalemu miaka mitatu. Mama yake aliitwa Maaka, binti Urieli wa Gibea.[#13:2 au mjukuu wa]
Basi kulikuwa na vita kati ya Abiya na Yeroboamu.
3Abiya aliingia vitani na jeshi la watu elfu mia nne wenye uwezo wa kupigana, naye Yeroboamu akapanga jeshi dhidi ya Abiya akiwa na jeshi la watu elfu mia nane wenye uwezo.
4Abiya akasimama juu ya Mlima Semaraimu, katika nchi ya vilima ya Efraimu, naye akasema, “Yeroboamu na Waisraeli wote, nisikilizeni!
5Hamfahamu kwamba Bwana , Mungu wa Israeli, alimpa Daudi na wazao wake ufalme juu ya Israeli milele kwa agano la chumvi?
6Hata hivyo Yeroboamu mwana wa Nebati afisa wa Sulemani mwana wa Daudi, aliasi dhidi ya bwana wake.
7Baadhi ya watu wasiofaa kitu, wabaya kabisa walimkusanyikia na kumpinga Rehoboamu mwana wa Sulemani alipokuwa kijana mdogo asiyekuwa na uamuzi, asiye na nguvu za kuweza kupingana nao.
8“Hata sasa unapanga kupingana na ufalme wa Bwana ambao uko mikononi mwa wazao wa Daudi. Kweli ninyi ni jeshi kubwa nanyi mnazo ndama za dhahabu Yeroboamu alizozitengeneza kuwa miungu yenu.
9Lakini je, hamkuwafukuza makuhani wa Bwana , wana wa Haruni na Walawi na kujifanyia makuhani wenu wenyewe kama yafanyavyo mataifa ya nchi nyingine? Yeyote anayekuja kujiweka wakfu akiwa na ndama dume na kondoo dume saba aweza kuwa kuhani wa kile ambacho ni miungu kwenu.
10“Lakini kwetu sisi, Bwana ndiye Mungu wetu, wala hatujamwacha. Makuhani wanaomtumikia Bwana ni wana wa Haruni, nao Walawi wakiwasaidia.
11Kila asubuhi na jioni wao hutoa sadaka za kuteketezwa na kufukiza uvumba wa harufu nzuri kwa Bwana . Wao huweka mikate juu ya meza takatifu, na kuwasha taa kwenye kinara cha dhahabu kila jioni. Sisi tunazishika kanuni za Bwana Mungu wetu. Lakini ninyi mmemwacha Mungu.
12Mungu yu pamoja nasi; yeye ndiye kiongozi wetu. Makuhani wake wakiwa na tarumbeta zao watapiga baragumu ya vita dhidi yenu. Watu wa Israeli, msipigane dhidi ya Bwana , Mungu wa baba zenu, kwa maana hamtashinda.”
13Basi Yeroboamu alikuwa ametuma jeshi kuzunguka nyuma ya Yuda ili akiwa mbele ya Yuda, jeshi liwavizie kwa nyuma.
14Basi Yuda wakageuka na kuona kwamba wanashambuliwa mbele na nyuma. Ndipo wakamlilia Bwana . Makuhani wakapiga tarumbeta zao,
15nao wanaume wa Yuda wakapiga ukelele wa vita. Walipopiga ukelele wa vita, Mungu akawafukuza Yeroboamu na Waisraeli wote mbele ya Mfalme Abiya na Yuda.
16Waisraeli wakakimbia mbele ya Yuda, naye Mungu akawatia mikononi mwao.
17Abiya na askari wake wakawachinja kwa machinjo makuu, hata wakawepo majeruhi elfu mia tano miongoni mwa watu wenye uwezo wa Israeli.
18Waisraeli walitiishwa katika tukio lile, nao watu wa Yuda wakawa washindi kwa sababu walimtegemea Bwana , Mungu wa baba zao.
19Abiya akamfuatia Yeroboamu na kuteka miji ya Betheli, Yeshana na Efroni kutoka kwake, pamoja na vijiji vya miji hiyo.
20Yeroboamu hakupata nguvu tena wakati wa utawala wa Abiya. Naye Bwana akampiga Yeroboamu akafa.
21Lakini Abiya akapata nguvu. Alioa wanawake kumi na wanne na alikuwa na wana ishirini na wawili na binti kumi na sita.
22Matukio mengine ya utawala wa Abiya, pamoja na mambo aliyofanya na aliyosema, yameandikwa katika kitabu cha maelezo cha nabii Ido.