The chat will start when you send the first message.
1Hezekia alikuwa na umri wa miaka ishirini na tano alipoanza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu kwa miaka ishirini na tisa. Mama yake aliitwa Abiya binti Zekaria.
2Akafanya yaliyo mema machoni pa Bwana kama Daudi baba yake alivyofanya.
3Katika mwezi wa kwanza wa mwaka wa kwanza wa utawala wake, alifungua milango ya Hekalu la Bwana , na kuikarabati.
4Akawaingiza makuhani na Walawi ndani na kuwakutanisha katika uwanja upande wa mashariki
5na kusema: “Nisikilizeni mimi, enyi Walawi! Jitakaseni nafsi zenu sasa, mkalitakase Hekalu la Bwana , Mungu wa baba zenu. Ondoeni uchafu wote kutoka mahali patakatifu.
6Baba zetu hawakuwa waaminifu, walifanya maovu machoni pa Bwana Mungu wetu na wakamwacha yeye. Wakageuza nyuso zao mbali na Maskani ya Bwana wakamgeuzia visogo vyao.
7Pia walifunga milango ya ukumbi wa Hekalu na kuzima taa zake. Hawakufukiza uvumba wala kutoa sadaka yoyote ya kuteketezwa katika mahali patakatifu kwa Mungu wa Israeli.
8Kwa hiyo, hasira ya Bwana ikashuka juu ya Yuda na Yerusalemu, naye akawa amewafanya kitu cha kutisha, cha kushangaza na kitu cha kufanyia mzaha kama mnavyoona kwa macho yenu wenyewe.
9Hii ndiyo sababu baba zetu wameanguka kwa upanga na ndiyo sababu wana wetu wa kiume na wa kike, na pia wake zetu wamekuwa mateka.
10Sasa ninadhamiria moyoni mwangu kufanya agano na Bwana , Mungu wa Israeli, ili hasira yake kali igeuziwe mbali nasi.
11Wanangu, basi msipuuze jambo hili sasa, kwa kuwa Bwana amewachagua ninyi msimame mbele zake na kumtumikia, mkawe watumishi wake na mkamfukizie uvumba.”
Kutoka kwa Wakohathi,
kutoka kwa Wamerari,
kutoka kwa Wagershoni,
13kutoka kwa wana wa Elisafani,
kutoka kwa wana wa Asafu,
14kutoka kwa wana wa Hemani,
kutoka kwa wana wa Yeduthuni,
15Walipomaliza kuwakusanya ndugu zao na kujiweka wakfu, wakaingia ndani ili kutakasa Hekalu la Bwana , kama vile mfalme alivyokuwa ameagiza, kwa kufuata neno la Bwana .
16Makuhani wakaingia patakatifu pa Hekalu la Bwana ili kupatakasa. Wakatoa nje penye ua wa Hekalu la Mungu kila kitu kichafu walichokikuta kwenye Hekalu la Bwana . Walawi wakavichukua na kuvipeleka nje katika Bonde la Kidroni.
17Walianza kazi ya utakaso siku ya kwanza ya mwezi wa kwanza na kufikia siku ya nane ya mwezi huo wakawa wamefikia kwenye ukumbi wa Bwana . Kwa siku zingine nane wakalitakasa Hekalu la Bwana lenyewe, wakakamilisha katika siku ya kumi na sita ya mwezi huo wa kwanza.
18Kisha wakaingia ndani kwa Mfalme Hezekia kutoa habari na kusema: “Tumelitakasa Hekalu la Bwana lote, madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa pamoja na vyombo vyake vyote, meza ya kupanga mikate iliyowekwa wakfu, pamoja na vyombo vyake vyote.
19Tumeviandaa na kuvitakasa vyombo vyote ambavyo Mfalme Ahazi, kwa kukosa uaminifu kwake, aliviondoa alipokuwa mfalme. Sasa viko mbele ya madhabahu ya Bwana .”
20Ndipo Mfalme Hezekia akainuka asubuhi na mapema, akakusanya maafisa wa mji wakakwea hekaluni mwa Bwana .
21Wakaleta mafahali saba, kondoo dume saba, wana-kondoo dume saba na beberu saba kuwa sadaka ya dhambi kwa ajili ya ufalme, kwa ajili ya mahali patakatifu na kwa ajili ya Yuda. Mfalme akawaamuru makuhani, wazao wa Haruni, kuvitoa vitu hivyo sadaka katika madhabahu ya Bwana .
22Hivyo wakachinja wale mafahali, nao makuhani wakachukua ile damu na kuinyunyiza kwenye madhabahu, halafu wakawachinja wale kondoo dume saba na kunyunyiza hiyo damu yao kwenye madhabahu, kisha wakawachinja wale wana-kondoo dume na kunyunyiza damu yao kwenye madhabahu.
23Wale beberu waliokuwa kwa ajili ya sadaka ya dhambi wakaletwa mbele ya mfalme na kusanyiko nao wakaweka mikono yao juu hao beberu.
24Ndipo makuhani wakawachinja hao beberu na kuweka damu yao kwenye madhabahu kwa ajili ya sadaka ya dhambi ili kufanya upatanisho kwa ajili ya Israeli wote, kwa sababu mfalme alikuwa ameamuru hiyo sadaka ya kuteketezwa na hiyo sadaka ya dhambi kwa ajili ya Israeli wote.
25Akawaweka Walawi kwenye Hekalu la Bwana wakiwa na matoazi, vinubi na zeze kama ilivyoagizwa na Daudi na Gadi mwonaji wa mfalme pamoja na nabii Nathani kwani hili lilikuwa limeamriwa na Bwana kupitia manabii wake.
26Hivyo Walawi wakasimama tayari wakiwa na ala za uimbaji za Daudi na makuhani walikuwa na tarumbeta zao.
27Hezekia akatoa amri ya kutoa sadaka ya kuteketezwa madhabahuni. Walipoanza kutoa sadaka, wakaanza pia kumwimbia Bwana pamoja na tarumbeta na zile ala za uimbaji za Daudi mfalme wa Israeli.
28Kusanyiko lote kusujudu katika kuabudu, huku waimbaji wakiimba na wenye tarumbeta wakipiga tarumbeta zao. Yote haya yaliendelea hadi walipomaliza kutoa ile dhabihu ya sadaka ya kuteketezwa.
29Walipomaliza kutoa sadaka, mfalme na kila mtu aliyekuwa pamoja naye wakapiga magoti na kuabudu.
30Mfalme Hezekia na maafisa wake wakawaamuru Walawi kumsifu Bwana kwa maneno ya Daudi na ya Asafu mwonaji. Hivyo wakaimba sifa kwa furaha, nao wakainamisha vichwa vyao na kuabudu.
31Kisha Hezekia akasema, “Sasa mmejiweka wakfu kwa Bwana . Njooni mlete dhabihu na sadaka za shukrani Hekaluni mwa Bwana .” Hivyo kusanyiko likaleta dhabihu na sadaka za shukrani, nao wote waliokuwa na mioyo ya hiari wakaleta sadaka za kuteketezwa.
32Idadi ya sadaka za kuteketezwa zilizoletwa na kusanyiko zilikuwa mafahali sabini, kondoo dume mia moja, na wana-kondoo dume mia mbili. Wote hawa walikuwa kwa ajili ya sadaka za kuteketezwa kwa Bwana .
33Wanyama waliowekwa wakfu kwa sadaka ya kuteketezwa walikuwa mafahali mia sita, pamoja na kondoo na mbuzi elfu tatu.
34Lakini makuhani walikuwa wachache sana kuweza kuchuna wale wanyama wote wa sadaka za kuteketezwa, kwa hiyo ndugu zao Walawi wakawasaidia hadi kazi ile ikakamilika na hadi makuhani wengine walipowekwa wakfu, kwa kuwa Walawi walikuwa makini kujiweka wakfu kuliko makuhani.
35Kulikuwa na sadaka nyingi za kuteketezwa, pamoja na mafuta ya wanyama ya sadaka za amani na sadaka za kinywaji ambazo ziliambatana na sadaka za kuteketezwa.
Kwa hiyo huduma ya Hekalu la Bwana ikarudishwa kwa upya.
36Hezekia pamoja na watu wote wakafurahi kwa sababu ya lile Mungu alilolifanya kwa ajili ya watu wake, kwa kuwa lilitendeka papo hapo.