The chat will start when you send the first message.
1Baada ya Sulemani kumaliza kuomba, moto ukashuka kutoka mbinguni na kuteketeza sadaka ya kuteketezwa na dhabihu, nao utukufu wa Mwenyezi Mungu ukalijaza Hekalu.
2Makuhani hawakuweza kuingia ndani ya Hekalu la Mwenyezi Mungu kwa sababu utukufu wa Mwenyezi Mungu ulilijaza.
3Waisraeli wote walipoona moto ukishuka na utukufu wa Mwenyezi Mungu ukiwa juu ya Hekalu, wakapiga magoti sakafuni wakasujudu, nyuso zao zikigusa chini, wakamwabudu na kumshukuru Mwenyezi Mungu, wakisema,
“Yeye ni mwema;
fadhili zake zadumu milele.”
4Ndipo mfalme na watu wote wakatoa dhabihu mbele za Mwenyezi Mungu.
5Naye Mfalme Sulemani akatoa dhabihu ya ng’ombe elfu ishirini na mbili pamoja na kondoo na mbuzi elfu mia moja na ishirini. Ndivyo mfalme na watu wote walivyoweka wakfu Hekalu la Mungu.
6Makuhani wakasimama kwenye nafasi zao, vivyo hivyo Walawi wakiwa na vyombo vya uimbaji vya Mwenyezi Mungu ambavyo Mfalme Daudi alikuwa ametengeneza kwa ajili ya kumsifu Mwenyezi Mungu, navyo vilitumika aliposhukuru, akisema, “Fadhili zake zadumu milele.” Mkabala na Walawi, makuhani walipiga tarumbeta zao, nao Waisraeli wote walikuwa wamesimama.
7Sulemani akaweka wakfu sehemu ya katikati ya ua uliokuwa mbele ya Hekalu la Mwenyezi Mungu, na hapo akatoa sadaka za kuteketezwa na mafuta ya wanyama wa sadaka za amani, kwa sababu madhabahu ya shaba aliyokuwa ametengeneza haikutosha kuweka sadaka hizo zote za kuteketezwa, sadaka za nafaka, na za mafuta.
8Hivyo Sulemani akaiadhimisha sikukuu wakati ule kwa muda wa siku saba, na Waisraeli wote pamoja naye. Walikuwa kusanyiko kubwa sana, watu kutoka Lebo-Hamathi hadi Kijito cha Misri.
9Katika siku ya nane walifanya kusanyiko, kwa sababu walikuwa wameadhimisha kuwekwa wakfu kwa madhabahu kwa muda wa siku saba, na sikukuu kwa muda wa siku nyingine saba.
10Katika siku ya ishirini na tatu ya mwezi wa saba Sulemani akawaaga watu waende nyumbani mwao, wakishangilia na kufurahi mioyoni mwao, kwa wema mwingi Mwenyezi Mungu aliomtendea Daudi na Sulemani na kwa ajili ya watu wake Israeli.
11Sulemani alipomaliza kujenga Hekalu la Mwenyezi Mungu na jumba la kifalme, naye akiwa amefanikiwa kutenda yale yote aliyokuwa nayo moyoni mwake kufanya katika Hekalu la Mwenyezi Mungu na katika jumba lake mwenyewe la kifalme,
12Mwenyezi Mungu akamtokea Sulemani usiku na kumwambia: