Yeremia 29

Yeremia 29

Barua kwa watu wa uhamisho

1Haya ndio maneno ya barua ambayo nabii Yeremia aliituma kutoka Yerusalemu kwenda kwa wazee waliobaki miongoni mwa waliopelekwa uhamishoni, na kwa makuhani, manabii na watu wengine wote ambao Nebukadneza alikuwa amewachukua kwenda uhamishoni Babeli kutoka Yerusalemu.

2(Hii ilikuwa ni baada ya Mfalme Yekonia na mama malkia, maafisa wa mahakama, viongozi wa Yuda na wa Yerusalemu, mafundi na wahunzi kwenda uhamishoni kutoka Yerusalemu.)[#29:2 au Konia ; pia anaitwa Yehoyakini]

3Barua ilikabidhiwa kwa Elasa mwana wa Shafani, na kwa Gemaria mwana wa Hilkia, ambao Sedekia mfalme wa Yuda aliwatuma kwa Mfalme Nebukadneza huko Babeli. Barua yenyewe ilisema:

Ujumbe kwa Shemaya

24Mwambie Shemaya Mnehelami,

25“Hili ndilo Bwana wa majeshi, Mungu wa Israeli, asemalo: Ulituma barua kwa jina lako mwenyewe kwa watu wote wa Yerusalemu, kwa Sefania mwana wa kuhani Maaseya na kwa makuhani wengine wote. Ulimwambia Sefania,

26‘Bwana amekuweka wewe uwe kuhani badala ya Yehoyada ili uwe msimamizi wa nyumba ya Bwana . Unapaswa kumfunga kwa mikatale na mnyororo wa shingoni mwendawazimu yeyote anayejifanya nabii.

27Kwa nini basi hukumkemea Yeremia Mwanathothi, aliyejifanya kama nabii miongoni mwenu?

28Ametutumia ujumbe huu huku Babeli: Mtakuwa huko muda mrefu. Kwa hiyo jengeni nyumba mkakae; pandeni mashamba na mle mazao yake.’ ”

29Kuhani Sefania, hata hivyo, akamsomea nabii Yeremia ile barua.

30Ndipo neno la Bwana likamjia Yeremia kusema:

31“Tuma ujumbe huu kwa watu wote walio uhamishoni kusema: ‘Hili ndilo asemalo Bwana kuhusu Shemaya Mnehelami: Kwa sababu Shemaya amewatabiria ninyi, hata ingawa sikumtuma, naye amewafanya kuamini uongo,

32hili ndilo asemalo Bwana : Hakika nitamwadhibu Shemaya Mnehelami pamoja na uzao wake. Hapatakuwa na yeyote atakayebaki miongoni mwa watu hawa, wala hataona mema nitakayowatendea watu wangu, asema Bwana , kwa sababu ametangaza uasi dhidi yangu.’ ”

Neno: Biblia Takatifu™ Neno™ Hakimiliki © 1984, 1989, 2009, 2015, 2025 na Biblica, Inc. Imetumiwa kwa ruhusa. Haki zote zimehifadhiwa duniani kote. Kiswahili Contemporary Version™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015, 2025 by Biblica, Inc. Used with permission. All rights reserved worldwide.
Published by: Biblica, Inc.