The chat will start when you send the first message.
1Ninayainua macho yangu kwako,
kwako wewe unayeketi mbinguni kwenye kiti chako cha enzi.
2Kama vile macho ya watumwa
yatazamavyo mkono wa bwana wao,
kama vile macho ya mjakazi
yatazamavyo mkono wa bibi yake,
ndivyo macho yetu yamtazamavyo Mwenyezi Mungu, Mungu wetu,
hadi atakapotuhurumia.
3Uturehemu, Ee Mwenyezi Mungu, uturehemu,
kwa maana tumevumilia dharau nyingi.
4Tumevumilia dhihaka nyingi kutoka kwa wenye kiburi,
dharau nyingi kutoka kwa wenye majivuno.