The chat will start when you send the first message.
1Wale wamtumainio Mwenyezi Mungu ni kama Mlima Sayuni,
ambao hauwezi kutikisika, bali wadumu milele.
2Kama milima inavyozunguka Yerusalemu,
ndivyo Mwenyezi Mungu anavyowazunguka watu wake
sasa na hata milele.
3Fimbo ya waovu haitadumu juu ya nchi
waliyopewa wenye haki,
ili wenye haki wasije wakatumia
mikono yao kutenda ubaya.
4Ee Mwenyezi Mungu, watendee mema walio wema,
wale walio wanyofu wa moyo.
5Bali wale wanaogeukia njia zilizopotoka,
Mwenyezi Mungu atawafukuza pamoja na watenda maovu.
Amani iwe juu ya Israeli.