The chat will start when you send the first message.
1Mwanangu, angalia usimpunje maskini riziki yake, wala macho ya wahitaji usiyangojeze mno.
2Usimhuzunishe mwenye njaa, wala usimchokoze mtu mwenye shida.
3Usiudhikishe mtima wa mnyonge, wala usikawie kumpa fukara.
4Usimkatae mwombaji katika udhia wake, wala usiugeuzie uso wako mbali na mtu maskini.
5Wala usimpe mtu sababu kukulaani;
6mradi akikulaani katika uchungu wa roho yake, Yeye Muumba wake ataisikia sauti yake.
7Ujipatie kupendwa na kusanyiko, na mbele ya mkuu wa mji uiname kichwa.
8Umtegee maskini sikio lako, ukamjibu maneno ya amani kwa unyenyekevu.
9Umwopoe yeyote aliyedhulumiwa mkononi mwake yule amdhulumuye, wala usifanye woga utoapo hukumu.
10Uwe mfano wa baba kwa yatima, badala ya mume kwa mama yao; hivyo utakuwa mwana wake Aliye Juu, naye atakupenda kuliko akupendavyo mama yako.
11Hekima huwafundisha wanawe na kuwaelimisha wanaomsikiliza.
12Wao wampendao hupenda uzima, nao wamtafutao watapata kibali kwa BWANA.
13Wao wamshikao wataurithi utukufu, hata na kudumu katika baraka ya BWANA.
14Wao nao wamtumikiao watamhudumia Yeye aliye Mtakatifu, nao wampendao BWANA huwapenda.
15Amsikiaye atahukumu kwa kweli, naye amjalie atakaa katika chumba chake cha ndani.
16Akimtumaini atamrithi, atakuwa naye hata vizazi vyote vya milele.
17Kwa maana mwanzo Hekima ataandamana naye kwa njia za kikombo, na kumletea hofu na woga, na kumwadhibisha kwa marudi yake, hata atakapoweza kumwamini roho yake, na kumhakiki kwa hukumu zake.
18Ndipo atakaporudi, na kumwongoza moja kwa moja, na kumfurahisha, na kumfunulia siri zake.
19Walakini akipotea, Hekima atamwacha, na kumtia mikononi mwa waangamizi.
20Mwanangu, uziangalie nyakati na majira, ujihadhari na maovu, ili usione haya kwa mambo ya roho yako.
21Kwa maana kuna haya iletayo dhambi, tena kuna haya iliyo utukufu na neema.
22Usimjali mtu yeyote kiasi cha kujidhuru roho yako, wala usiingiwe na soni kiasi cha kujiangamiza.
23Usiyazuie maneno yako iwapo yanaelekea hali ya salama, wala usifiche hekima yako kwa ajili ya uadilifu;
24madhali kwa usemi hekima itajulikana, na mafundisho kwa neno la ulimi.
25Usiseme neno kinyume cha kweli, na machoni pa Mungu uwe mnyenyekevu.
26Usione haya kuungama dhambi zako, wala usijaribu kuuzuia mkondo wa mto.
27Usijilaze chini ili mpumbavu akukanyage, lakini usimpendelee mwenye cheo.
28Uishindanie kweli hata kufa, naye BWANA atakupigania wewe.
29Usiwe mwepesi wa kunena,
Mlegevu wa kutenda, msahaulifu.
30Usiwe kama simba nyumbani mwako,
Mwenye kutuhumu watumishi wako.
31Mkono wako usinyoshwe kupokea,[#Mdo 20:35]
Ukarudishwa wakati wa kulipa.