The chat will start when you send the first message.
1Nami, ndugu, nilipokuja kwenu nalijia kuutangaza ushuhuda wa Mungu; sikuja kuwaambia maneno makuu ya werevu ulio wa kweli.[#1 Kor. 1:17.]
2Kwani kwenu sikuwaza werevu mwingine, asipokuwa Yesu Kristo, naye hivyo, alivyowambwa msalabani.[#Gal. 6:14.]
3Nami nalikaa kwenu mwenye unyonge na woga na matetemeko mengi.[#Tume. 18:9; 2 Kor. 10:1.]
4Hata nilipowaambia mbiu yangu, sikutumia maneno ya werevu yenye nguvu ya kushinda, ila nimetumia Roho yenye nguvu,[#1 Kor. 2:1; Mat. 10:20.]
5kusudi mmtegemee Bwana, ila visiwe kwa kushindwa na werevu wa kimtu, ila kwa kushindwa na nguvu yake Mungu.[#Ef. 1:17,19; 1 Tes. 1:5.]
6*Tena yako ya werevu wa kweli; tunawaambia wale wenye kuyatimiza yote. Lakini nayo siyo ya werevu wa ulimwengu huu, wala wa wakuu wa ulimwengu huu walio wenye kufa.
7Ila yaliyo ya werevu wa Mungu ulio wa kweli ndiyo, tunayoyasema, nayo yalikuwa hayajatokea bado, maana yalikuwa yamefichwa; huko kale, ulimwengu ulipokuwa haujawa bado, Mungu aliyachagua yayo hayo, yatokee sasa kututukuza sisi.[#Rom. 16:25; Kol. 2:3.]
8Kwao wanaoutawala ulimwengu huu hakuna aliyeyatambua. Maana kama wangaliyatambua, wasingalimwamba msalabani Bwana aliye mwenye utukufu.
9Ila ilikuwa, kama ilivyoandikwa:
Jicho lisiyoyaona, sikio lisiyoyasikia,
moyo wa mtu usiyoweza kuyatia mwake,
ndiyo, Mungu aliyowaandalia wale wampendao.
10Lakini sisi Mungu ametufunulia hayo alipotupa Roho wake. Kwani Roho huyapambanua mambo yote, hata vilindi vya Mungu[#Mat. 13:11; Ef. 1:9-10; Kol. 1:26-27.]
11Kwani yuko mtu ayajuaye mambo ya mtu, isipokuwa roho yake yule mtu iliyomo mwake? Vivyo hivyo mambo ya Mungu nayo hakuna ayatambuaye, asipokuwa Roho wake Mungu.
12Lakini sisi hatukupewa roho ya ulimwengu huu, ila tumepewa Roho iliyotoka kwa Mungu, tupate kuyajua, tuliyogawiwa na Mungu.
13Nayo ndiyo, tuyasemayo; tena hatuyasemi kwa maneno, tuliyofundishwa na werevu wa kimtu, ila tulifundishwa na Roho; hivyo mambo ya Roho tunayapatia hata maneno ya Roho.[#1 Kor. 2:1,4.]
14Lakini mtu anayeutii moyo wake tu hayafumbui ya Roho wake Mungu; huyawazia kuwa mapumbavu tu, hawezi kuyatambua, kwani hayo sharti yachunguzwe kwa nguvu ya Roho.[#1 Kor. 1:23; Yoh. 8:47.]
15Lakini mtu anayemtii Roho huyachunguza yote, lakini mwenyewe hakuna, ambaye achunguzwa naye.[#1 Yoh. 2:20.]
16Maana:
Yuko aliyeyatambua mawazo ya Bwana, amjulishe jambo?
Lakini sisi tunayo mawazo yake Kristo.*