1 Yohana 1

1 Yohana 1

Neno lenye uzima lilikuwapo tangu mwanzo.

1*Yaliyokuwapo tangu mwanzo, tuliyoyasikia, tuliyoyaona kwa macho yetu, tuliyoyatazama na kuyapapasa kwa mikono yetu, ndiyo, tunayoyatangaza kuwa Neno lenye uzima.[#Yoh. 1:1,14.]

2Nao uzima ulifunuliwa, nasi tukauona, kwa hiyo twashuhudia kwa kuwatangazia ninyi huo uzima wa kale na kale uliokuwa kwa Baba, ukatufunuliwa sisi.[#Yoh. 1:4.]

3Basi, tuliyoyaona, tuliyoyasikia, twawatangazia hata ninyi, nanyi mpate kuwa mwenzetu wa bia. Nayo bia yetu sisi ni ile ya Baba na ya Mwana wake Yesu Kristo.

4Haya tunawaandikia ninyi, furaha yenu itimizwe.*[#1 Yoh. 5:13; Yoh. 15:11; 16:24.]

Damu ya Yesu huondoa makosa.

5Nao utume, tuliousikia kwake, tunaowatangazia ninyi, ndio huu: Mungu ni mwanga, namo mwake hamna giza iwayo yote.[#Yak. 1:17.]

6Tukisema: Tuko na bia naye, kisha tunaendelea gizani, twasema uwongo, nayo yaliyo ya kweli hatuyafanyi.[#1 Yoh. 2:4.]

7Lakini tukiendelea mwangani, kama yeye alivyo mwangani, tuko na bia yetu sisi kwa sisi, nayo damu ya Yesu, Mwana wake, hututakasa, makosa yote yatutoke.[#Ebr. 9:14; Ufu. 1:5; 7:14.]

8Tukisema: Makosa hatunayo, tunajidanganya wenyewe, nayo kweli haimo mwetu.

9Lakini tukiyaungama makosa yetu, yeye ni mwelekevu na mwongofu, atuondolee makosa, kisha atutakase, upotovu wote ututoke.[#Fano. 28:13.]

10Tukisema: Hatukukosa, twamfanya yeye kuwa mwongo, tena Neno lake halimo mwetu.

Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.
Published by: Bible Society of Tanzania