The chat will start when you send the first message.
1Mfalme Salomo akawa mfalme wa Waisiraeli wote;[#1 Fal. 2:35.]
2nao hawa walikuwa wakuu wake: Azaria, mwana wa Sadoki, alikuwa mtambikaji.
3Elihorefu na Ahia, wana wa Sisa, walikuwa waandishi; Yosafati, mwana wa Ahiludi, alikuwa mwandishi wa mambo yaliyopasa kukumbukwa.
4Benaya, mwana wa Yoyada, alikuwa mkuu wa vikosi, Sadoki na Abiatari walikuwa watambikaji.[#1 Fal. 2:35; 2 Sam. 23:20.]
5Azaria, mwana wa Natani, alikuwa mkuu wa waangaliaji, naye mtambikaji Zabudi, mwana wa Natani, alikuwa mpenzi wa mfalme.
6Ahisari alikuwa mkuu wa nyumbani, naye Adoniramu, mwana wa Abuda, alikuwa mkuu wa kazi za nguvu.[#1 Fal. 5:14.]
7Salomo alikuwa na waangaliaji kumi na wawili waliowekwa kuwaangalia Waisiraeli wote, ndio waliompatia mfalme nao wa nyumbani mwake vyakula, ikawa kila mmoja akaleta vyakula vya mwezi mmoja katika mwaka.
8Nayo majina yao ni haya: Mwana wa Huri milimani kwa Efuraimu;
9mwana wa Dekeri alikuwako Makasi na Salabimu na Beti-Semesi na Eloni na Beti-Hanani.
10Mwana wa Hesedi huko Aruboti, hata Soko na nchi yote ya Heferi ilikuwa yake.
11Mwana wa Abinadabu vilima vyote vya Dori vilikuwa vyake, naye Tafati binti Salomo alikuwa mkewe.[#1 Sam. 16:8.]
12Baana, mwana wa Ahiludi, yake ilikuwa Taanaki na Megido na Beti-Seani yote iliyoko kandokando ya Sartani chini ya Izireeli toka Beti-Seani hata Abeli-Mehola mpaka ng'ambo ya pili ya Yokimamu.
13Mwana wa Geberi alikuwako vilimani kwa Gileadi; navyo vijiji vya Yairi, mwana wa Manase, vilivyoko Gileadi vilikuwa vyake, hata nchi ya Argobu iliyoko Basani, ni miji mikubwa 60 yenye maboma na makomeo ya shaba.[#4 Mose 32:41.]
14Ahinadabu, mwana wa Ido, alielekea Mahanaimu.
15Ahimasi alikuwako Nafutali, naye alimchukua Basimati, binti Salomo, awe mkewe.
16Baana, mwana wa Husai, alikuwako Aseri na Baloti.
17Yosafati, mwana wa Parua, alikuwako Isakari.
18Simei, mwana wa Ela, alikuwako Benyamini.
19Geberi, mwana wa Uri, alikuwako katika nchi ya Gileadi iliyokuwa nchi ya Sihoni, mfalme wa Waamori, na ya Ogi, mfalme wa Basani. Naye mwangaliaji aliyewekwa katika nchi hizi alikuwa yeye mmoja.
20Nao Wayuda na Waisiraeli walikuwa wengi, kama mchanga ulioko ufukoni kwenye bahari ulivyo mwingi; walikuwa wakila, wakinywa na kufurahi.[#1 Fal. 3:8; 1 Mose 13:16; 22:17.]
21Salomo akawa akizitawala nchi za kifalme zote kutoka lile jito kubwa kuifikia nchi ya Wafilisti hata mipaka ya Misri; walimletea mahongo, wakamtumikia Salomo siku zake zote za kuwapo.
22Vyakula, Salomo alivyovitumia kwa siku moja, vilikuwa kori 30, ndio frasila 300 za unga mzuri na kori 60, ndio frasila 600 za unga mwingine;
23tena ng'ombe 10 waliononeshwa na ng'ombe 20 wa malishoni na kondoo 100, tena kulungu na paa na funo na mabata waliononeshwa hawakuhesabiwa.
24Kwani alikuwa akizitawala nchi zote za ng'ambo ya huku ya lile jito kutoka Tifusa hata Gaza, nao wafalme wote wa ng'ambo ya huku ya lile jito aliwatawala, kukawa na utengemano katika nchi zake zote zilizomzunguka.
25Wayuda na Waisiraeli wakakaa na kutulia kila mtu chini ya mzabibu wake na chini ya mkuyu wake kutoka Dani kufikia Beri-Seba siku zote, Salomo alizokuwapo.[#3 Mose 25:18; 2 Fal. 18:31; Mika 4:4.]
26Salomo alikuwa na majozi ya farasi 40000 ya magari yake, tena wapanda farasi 12000.
27Nao wale waangaliaji wakampatia mfalme Salomo vyakula nao wote walioikaribia meza ya mfalme Salomo, kila mmoja wao mwezi wake, hawakuwakosesha kitu cho chote.
28Nao mtama na mabua ya ngano ya farasi wa kupanda na wa magari wakayapeleka mahali hapo, alipokuwa, kila mtu hapo, alipoagizwa.
29Mungu akampa Salomo werevu wa kweli na utambuzi mwingi sana na akili za moyo zilizokuwa nyingi kama mchanga ulioko ufukoni kwenye bahari.[#1 Fal. 3:12.]
30Werevu wa kweli wa Salomo ukazidi kuliko werevu wao wote waliokuwa werevuwa kweli upande wa maawioni kwa jua, nao warevu wote wa kweli ulioko Misri.
31Akawa mwerevu wa kweli kuliko watu wote pia, akamshinda naye Etani wa Ezera na Hemani, hata Kalkoli na Darda, wana wa Maholi; jina lake likasifiwa katika mataifa yote pande zote.
32Akasema mifano 3000, nazo nyimbo zake zikawa 1005.[#Mbiu. 12:9.]
33Akaiimbia miti kuanzia miangati iliyoko Libanoni kufikisha hata mivumbasi imeayo mahameni, akawaimbia nao nyama wa porini na ndege na wadudu na samaki.
34Watu wakaja na kutoka katika makabila yote, wausikilize werevu wa kweli wa Salomo, wakatoka hata kwa wafalme wote wa huku nchini waliopata habari ya werevu wake wa kweli.[#1 Fal. 10:1,6.]