The chat will start when you send the first message.
1Sauli alipoupata ufalme alikuwa mwenye miaka (30); naye Sauli alipokuwa mfalme wa Waisiraeli miaka miwili,
2akajichagulia watu 3000 kwa Waisiraeli: 2000 wakawa naye Sauli huko Mikimasi na mlimani kwa Beteli, 1000 walikuwa na Yonatani huko Gibea wa Benyamini. Watu wengine akawapa ruhusa kwenda zao kila mtu hemani kwake.
3Yonatani akaipiga ngome ya Wafilisti iliyokuwa huko Geba, nao Wafilisti wakavisikia. Kisha Sauli akapiga baragumu katika nchi yote kwamba: Waebureo na wasikilize![#1 Sam. 14:49.]
4Waisiraeli wote waliposikia ya kuwa Sauli ameipiga ngome ya Wafilisti, ya kuwa Waisiraeli wanawanukia Wafilisti vibaya, ndipo, watu wote walipokwitwa kumfuata Sauli kwenda Gilgali.
5Wafilisti nao wakakusanyika kupigana na Waisiraeli; magari 30000 na wapanda farasi 6000, nao watu wao wakawa wengi kama mchanga ulioko ufukoni kwenye bahari. Hao wakapanda, wakapiga makambi kule Mikimasi kuelekea Beti-Aweni, ni upande wake wa maawioni kwa jua.
6Watu wa Waisiraeli walipoona, ya kuwa wamesongeka kwa kukaribiwa na wale watu, wakajificha mapangoni na magengeni na miambani na mashimoni na makaburini.
7Waebureo wengine wakavuka Yordani kwenda katika nchi za Gadi na za Gileadi; lakini Sauli alikuwa yuko bado Gilgali, nao watu wote wakamfuata kwa kutetemeka tu.
8Alipongoja zile siku saba alizoagizwa na Samweli, naye Samweli asipokuja, watu wakatawanyika na kumwacha.[#1 Sam. 10:8.]
9Ndipo, Sauli aliposema: Nileteeni ng'ombe ya tambiko ya kuteketezwa nzima na vipaji vya tambiko vya shukrani! Kisha akatambika na kuiteketeza hiyo ng'ombe ya tambiko.
10Ikawa, alipokwisha kuiteketeza hiyo ng'ombe ya tambiko, mara Samweli akaja, Sauli akatoka kumwendea njiani na kumpigia magoti.
11Samweli akamwuliza: Umefanya nini? Sauli akamwambia: Nimeona, ya kuwa watu wanatawanyika na kuniacha, wewe nawe hukuja siku hizo, tulizoagana, tena Wafilisti wamekwisha kukusanyika huko Mikimasi,
12basi, nikasema: Sasa Wafilisti watanishukia huku Gilgali, nikiwa sijamtokea Bwana na kumwomba, atuwie mpole; ndipo, nilipojipa moyo, nikatambika na kuiteketeza ng'ombe ya tambiko.
13Samweli akamwambia Sauli: Umefanya ujinga usipoliangalia agizo la Bwana Mungu wako, alilokuagiza, akapata sasa kuusimamisha ufalme wako wa kuwatawala Waisiraeli, uwe wa kale na kale.
14Lakini sasa ufalme wako hausimamiki, Bwana amekwisha kujitafutia mtu mwingine aupendezaye moyo wake, naye amemwagiza kuwa mkuu wao walio ukoo wake, kwani hukuyaangalia, Bwana aliyokuagiza.[#Tume. 13:22.]
15Kisha Samweli akaondoka na kutoka Gilgali, akaenda kupanda Gibea wa Benyamini. Naye Sauli akawakagua watu walioonekana kwake, wakawa kama watu 600.
16Sauli na mwanawe Yonatani na watu walioonekana kwao wakakaa katika Geba wa Benyamini, nao Wafilisti walikuwa wamepiga makambi yao Mikimasi.
17Kisha wenye kuangamiza wakatoka katika makambi ya Wafilisti, nao walikuwa vikosi vitatu; kimoja kikashika njia ya kwenda Ofura katika nchi ya Suali;
18kikosi cha pili kikashika njia ya Beti-Horoni, nacho kikosi cha tatu kikashika njia ya mpakani kunakoelekea Bonde la Mafisi upande wa nyikani.
19Katika nchi yote ya Waisiraeli hakuonekana mhunzi, kwani Wafilisti walisema: Waebureo wasijifanyie wala panga wala mikuki![#Amu. 5:8.]
20Kwa hiyo Waisiraeli hawakuwa na budi kushuka kwao Wafilisti, kama mtu alitaka kunoa tu jembe lake au mundu wake au shoka lake au muo wake,
21makali ya majembe au ya miundu au ya pembe za uma au ya mashoka yakidugika, hata wakitaka tu kunyosha ncha za fimbo.
22Kwa hiyo siku ya mapigano hamkupatikana wala upanga wala mkuki mkononi mwa mtu kwao watu wote waliokuwa na Sauli na Yonatani, ila mata yakaonekana tu kwake Sauli na kwa mwanawe Yonatani.
23Kikosi cha Wafilisti kikatoka kwenda penye njia ya magemani huko Mikimasi.