The chat will start when you send the first message.
1Dawidi akasema moyoni mwake kwamba: Siku moja nitaangamizwa kwa mkono wa Sauli; sitaona mema, nisipojiponya kabisa na kuikimbilia nchi ya Wafilisti, Sauli akate tamaa za kunitafuta tena katika mipaka yote ya Waisiraeli; ndivyo, nitakavyoponyoka mkononi mwake.
2Kwa hiyo Dawidi akaondoka, akapita mpaka yeye na watu 600 waliokuwa naye, wakaenda kwa Akisi, mwana wa Maoki, mfalme wa Gati.[#1 Sam. 21:10; 1 Fal. 2:39.]
3Dawidi akakaa kwa Akisi huko Gati yeye na watu wake, kila mtu na mlango wake. Yeye Dawidi alikuwa na wakeze wawili, Ahinoamu wa Izireeli na Abigaili, mkewe Nabali wa Karmeli.
4Sauli alipopashwa habari, ya kuwa Dawidi amekimbilia Gati, hakuendelea tena kumtafuta.
5Kisha Dawidi akamwambia Akisi: Kama nimeona upendeleo machoni pako, na wanipe pa kukaa katika mji mmoja wa porini, nikae huko! Inakuwaje, mtumishi wako akikaa kwako katika mji wa kifalme?
6Ndipo, Akisi alipompa Siklagi siku hiyo; ndivyo, Siklagi ulivyopata kuwa wao wafalme wa Wayuda mpaka siku hii ya leo.[#Yos. 15:31; Amu. 1:19.]
7Hesabu ya siku, Dawidi alizokaa katika nchi ya Wafilisti, ikawa mwaka na miezi minne.
8Ndipo, Dawidi na watu wake walipopanda, wakawashambulia Wagesuri na Wagirzi na Waamaleki, kwani hawa ndio waliokaa katika nchi hiyo tangu zamani zote, kufika Suri hata nchi ya Misri.
9Dawidi alipoipiga hiyo nchi, hakuacha mume wala mke, asimwue, akachukua mbuzi na kondoo na ng'ombe na punda na ngamia na nguo, kisha akarudi kufika kwa Akisi.
10Akisi alipomwuliza: Leo mmeshambulia wapi? Dawidi hujibu: Upande wa kusini wa Yuda, au: Upande wa kusini wa Wayerameli, au: Upande wa kusini wa Wakeni.
11Dawidi asipoacha mume wala mke, asimwue, ni kwa kwamba asiwapeleke Gati, wakayasimulia matendo yetu kwamba: Hivi ndivyo, Dawidi alivyovifanya. Hii desturi yake Dawidi akaifuata siku zile zote, alizokaa katika nchi ya Wafilisti.
12Akisi akamtegemea Dawidi kwamba: Kwa kuwa amejipatia mnuko mbaya kwao walio ukoo wake wa Waisiraeli, atakuwa mtumishi wangu kale na kale.[#1 Mose 34:30; 2 Mose 5:21.]