The chat will start when you send the first message.
1Sanduku la Bwana lilipokuwa miezi saba katika nchi ya Wafilisti,
2Wafilisti wakawaita watambikaji na waaguaji na kuwauliza: Sanduku la Bwana tulifanyie nini? Tujulisheni njia ya kulipeleka mahali pake!
3Wakajibu: Mkilipeleka Sanduku la Mungu wa Waisiraeli, msilipeleke bure tu, ila sharti mlirudishe pamoja na kipaji cha tambiko cha upozi. Ndipo, mtakapopona, tena itajulikana kwenu, kama ni kwa sababu gani, mkono wake usipoondoka kwenu.
4Wakauliza: Kipaji cha tambiko cha upozi, tutakachomtolea tukilirudisha, ndio nini? Wakajibu: Kwa hesabu ya wakuu wa Wafilisti mifano mitano ya dhahabu ya hayo majipu mabaya, tena mifano mitano ya dhahabu ya panya. Kwani pigo lililowapata watu wote nanyi wakuu ni lilelile moja.[#Yos. 13:3.]
5Ifanyeni hiyo mifano ya majipu yenu mabaya na ya panya wenu wanaoiangamiza nchi hii, kisha mmpe Mungu wa Waisiraeli macheo, labda ataugeuza mkono wake kuwa mwepesi kwenu na kwa miungu yenu na katika nchi yenu.
6Mbona mnaishupaza mioyo yenu, kama Wamisri na Farao walivyoishupaza mioyo yao? Je sivyo? Alipowafanyia mabaya, wakawapa ruhusa, waende zao?[#2 Mose 8:11; 12:31.]
7Sasa tengenezeni gari jipya moja, tena chukueni ng'ombe wawili wanyonyeshao, wasiobandikiwa bado mti wa kuvutia gari! Kisha wafungeni hao ng'ombe penye hilo gari, miwaondoa watoto wao kwao na kuwarudisha nyumbani.
8Kisha lichukueni Sanduku la Bwana, mliweke garini pamoja na vile vyombo vya dhahabu, mtakavyomlipa kuwa kipaji cha tambiko cha upozi. Hivyo vitieni katika kisanduku kando yake, kisha lipelekeni, liende kwao!
9Kisha tazameni: likishika njia ya kuupandia mpaka wa Beti-Semesi, basi, ndilo lililotupatia haya mabaya makubwa mno; lakini kama sivyo, ndipo, mtakapojua, ya kuwa sio mkono wake uliotupiga, ila ni tukio tu lililotupata.
10Nao watu wakafanya hivyo, wakachukua ng'ombe wawili wanyonyeshao, wakawafunga penye gari, nao watoto wao wakawafungia nyumbani.
11Kisha wakaliweka Sanduku la Bwana garini pamoja na kisanduku chenye panya za dhahabu na mifano ya majipu yao mabaya.
12Ndipo, ng'ombe waliposhika njia ya kwenda moja kwa moja, ndio njia ya Beti-Semesi; wakaenda wakilia na kuifuata barabara hiyo moja tu, hawakuiacha kwenda kuumeni wala kushotoni. Nao wakuu wa Wafilisti wakawafuata hata mpakani kwa Beti-Semesi.
13Nao watu wa Beti-Semesi walikuwa wakivuna ngano bondeni; walipoyainua macho yao wakaliona hilo Sanduku, wakafurahi kuliona.
14Lile gari likaingia shambani kwa Yosua wa Beti-Semesi, likasimama huko, nako huko kulikuwa na jiwe kubwa. Basi, wakaipasua miti ya gari, nao hao ng'ombe wakamtolea Bwana kuwa ng'ombe za tambiko.
15Nao Walawi wakalishusha Sanduku la Bwana na kile kisanduku kilichowekwa pamoja nalo, kilichotiwa vile vyombo vya dhahabu, wakaliweka juu ya hilo jiwe kubwa. Kisha watu wa Beti-Semesi wakatoa ng'ombe za tambiko za kuteketezwa nzima, wakachinja nazo ng'ombe nyingine za tambiko siku ileile.
16Wale wakuu watano wa Wafilisti walipokwisha kuviona wakarudi Ekroni siku ileile.
17Nayo mifano ya dhahabu ya majipu, Wafilisti waliyoilipa, iwe kipaji cha tambiko cha upozi, ni hii: mmoja wa Asdodi, mmoja wa Gaza, mmoja wa Askaloni, mmoja wa Gati, mmoja wa Ekroni.
18Nazo panya za dhahabu hesabu yao ilikuwa sawa na hesabu ya miji yote ya Wafilisti ya hao wakuu watano, ya miji yenye maboma na ya vijiji vya shambani. Hivi vinashuhudiwa na lile jiwe kubwa, ambalo wameliweka Sanduku la Bwana juu yake, nalo liko hata siku hii ya leo shambani kwa Yosua huko Beti-Semesi.
19(Bwana) akawapiga watu wa Beti-Semesi, kwa kuwa wamechungulia Sandukuni mwa Bwana, akapiga kwao watu 70, tena watu 50000; ndipo, watu walipolia sana, kwa kuwa Bwana amewapiga wa kwao pigo kubwa.[#4 Mose 4:20; 2 Sam. 6:6-7.]
20Watu wa Beti-Semesi wakasema: Yuko nani awezaye kusimama mbele ya Bwana, huyu Mungu mtakatifu? Sasa aende kwa nani akitoka kwetu?
21Wakatuma wajumbe kwa wenyeji wa Kiriati-Yearimu kwamba: Wafilisti wamelirudisha Sanduku la Bwana; haya! Telemkeni, mlipandishe kwenu!