The chat will start when you send the first message.
1Sisi Paulo na Silwano na Timoteo tunawaandikia ninyi mlio wateule wa Tesalonike katika Mungu Baba na Bwana Yesu Kristo. Upole uwakalie na utengemano![#Tume. 15:40; 16:19; 17:1-10; 2 Tes. 1:1.]
2Tunamshukuru Mungu siku zote kwa ajili yenu nyote. Nasi hatuachi kuwakumbuka katika kuomba kwetu
3tukikumbuka mbele ya Mungu aliye Baba yetu, mnavyofanya kazi kwa kumtegemea, tena mnavyojisumbua, mpate kupendana, tena mnavyovumilia na kumngojea Bwana wetu Yesu Kristo.[#1 Kor. 13:13.]
4Kwani ndugu mliopendwa na Mungu, twajua: mmechaguliwa.
5Kwani Utume wetu mwema haukuwa kwenu katika maneno tu, ila ulitenda hata nguvu, ukawapo nayo Roho takatifu, mkapata pa kujishikizia sana; mwajua, tulivyokuwa kwenu kwa ajili yenu.[#1 Kor. 2:5.]
6Nanyi mkatuiga sisi naye Bwana; mlikuwa na maumivu mengi, mkalipokea Neno kwa furaha, watu wapewayo na Roho takatifu.[#1 Kor. 4:16.]
7Kwa hiyo wote wamtegemeao Mungu katika nchi ya Makedonia na ya Akea waliweza kujifundishia kwenu ninyi.[#1 Tes. 4:10.]
8Kwani uvumi wa Neno la Bwana ulitoka kwenu, ukaenea Makedonia na Akea, lakini si huko tu, ila imejulikana waziwazi po pote, mnavyomtegemea Mungu. Kwa hiyo haitupasi sisi kuvisema mahali po pote,[#Rom. 1:8.]
9kwani wenyewe huvisimuliana, mlivyotupokea, tulipoingia kwenu, nanyi mlivyomgeukia Mungu mkaviacha vinyago vya kutambikia, mpate kumtumikia Mungu aliye mwenye uzima na ukweli,[#Tume. 14:15; 1 Kor. 12:2.]
10tena mnavyomgojea Mwana wake, atoke mbinguni; ni yeye Yesu, aliyemfufua katika wafu, naye ndiye atakayetuokoa katika makali yatakayokuja.[#Tit. 2:13.]