The chat will start when you send the first message.
1Kwa hiyo hatukuweza kuvumilia tena, tukapendezwa kuachwa peke yetu huko Atene,[#Tume. 17:14-15.]
2tukamtuma ndugu yetu Timoteo anayemtumikia Mungu na kuutangaza Utume mwema wa Kristo; tulimtuma, awashupaze ninyi na kuwatuliza mioyo kwa hivyo, mnavyomtegemea Mungu,[#Tume. 16:1-3.]
3mtu asitikisike katika maumivu ya siku hizi; kwani mwajua wenyewe: jambo tulilowekewa, ni hilo.[#Tume. 14:22; Ef. 3:13; 2 Tim. 3:12; Ebr. 10:39.]
4Kwani hata hapo, tulipokuwa kwenu, tuliwafumbulia kwamba: Inatupasa kuumizwa; ndivyo vilivyotimia sasa, kama mnavyojua.[#1 Kor. 6:19.]
5Kwa hiyo nami sikuweza kuvumilia tena, nikamtuma, nipate kutambua, kama mwamtegemea Mungu bado, au kama yule mwenye kujaribu amewajaribu, masumbuko yetu ya kwenu yakawa ya bure.[#Fil. 2:16.]
6Lakini sasa Timoteo amefika kwetu kutoka kwenu, akatusimulia vema mambo mema, mnavyomtegemea Mungu, mnavyopendana, mnavyotukumbuka vema siku zote mkitunukia kutuona sisi, kama sisi tunavyotunukia kuwaona ninyi.[#Tume. 18:5.]
7Kwa hayo, ndugu, tumetulizwa mioyo kwa ajili yenu katika mahangaiko na maumivu yetu yote, tuliposikia, mnavyomtegemea Mungu.
8Kwani sasa tumerudi uzimani tena, ikiwa ninyi mmesimama penye Bwana.
9Kwa shukrani gani, tutakazomtolea Mungu kwa ajili yenu, tutaweza kumlipa furaha zote, tulizozipata kwenu mbele yake yeye Mungu wetu?[#3 Mose 19:18.]
10Nasi twafuliza kuomba sanasana usiku na mchana, tupate kuonana nanyi uso kwa uso, tuweze kuziongeza nguvu zenu za kumtegemea Mungu, pakiwapo zilipokoseka.
11Yeye Mungu aliye Baba yetu naye Bwana wetu Kristo na atuongoze njia ya kufika kwenu!
12Ninyi Bwana awaongezee upendano, mfurikiwe nao, mpate kupendana ninyi kwa ninyi, kisha mwapende nao wote wengine, kama sisi nasi tunavyowapenda ninyi!
13Hivyo mioyo yenu itashupaa, tena haitakosa kutakata kwa kuwa haina madoadoa, Mungu aliye Baba yetu akiitazama hapo, Bwana wetu Yesu atakapokuja pamoja na watakatifu wake wote.[#Fil. 1:10.]