1 Timoteo 1

1 Timoteo 1

Anwani.

1Mimi Paulo niliye mtume wa Kristo Yesu kwa agizo lake Mungu aliye mwokozi wetu na kwa agizo lake Kristo Yesu aliye kingojeo chetu[#Kol. 1:27.]

2nakuandikia, wewe Timoteo uliye mwanangu wa kweli kwa hivyo, unavyomtegemea Mungu. Upole ukukalie na huruma na utengemano unaotoka kwa Mungu Baba na kwa Bwana wetu Kristo Yesu![#Tume. 16:1-2; Tit. 1:4.]

Upendano ufaao.

3Hapo, nilipokwenda Makedonia nilikuagiza wewe kukaa Efeso, uwakataze wengine, wasifundishe menginemengine,[#Tume. 20:1.]

4wala wasishikamane na masimulio yasiyo ya kweli wala na mambo ya mashina ya koo za kale yasiyokoma. Haya huleta mabishano, lakini hayaufalii utunzaji wa Mungu wa kuwatunza wenye kumtegemea.[#1 Tim. 4:7.]

5Lakini agizo hilo linatimia, wakipendana kwa mioyo itakatayo, ijuayo yaliyo mema tu, imtegemeayo Mungu kwa kweli pasipo ujanja.[#Mat. 22:37-40; Rom. 13:10; Gal. 5:6.]

6Wengine wameikosa mioyo iliyo hivyo, wakapotelea katika maneno ya upuzi;[#1 Tim. 6:4,20.]

7walitaka kuwa wafunzi wa Maonyo, lakini hawajui, wala wasemayo, wala wabishayo.

8Twajua, ya kuwa maonyo ni mazuri, mtu akiyatumia kujionya[#Rom. 7:12; Gal. 5:18-23.]

9kwa kujua kwamba: Mwongofu siye aliyetolewa Maonyo, ila waliotolewa ndio wapotovu nao wasiotii nao wasiomcha Mungu nao wakosaji nao wachafu nao wabezi nao wauao baba zao nao wauao mama zao nao wauao wenzao

10nao wagoni nao walalanao nao wauzao watu nao waongo nao waapao viapo vya uwongo, na kama wako wengine wafanyao neno jingine lisilopatana na ufundisho uwapao watu uzima.[#1 Tim. 6:3.]

11Hivyo ndivyo, tulivyofundishwa na Utume mwema wa utukufu wake Mungu anayeshangiliwa; nami nimepewa kuutangaza.[#1 Tim. 6:15.]

12Namshukuru Bwana wetu Kristo Yesu aliyenitia nguvu, akaniona kuwa mwelekevu, akanipa utumishi mimi[#Tume. 9:1-15; 1 Kor. 15:9-10; Gal. 1:13-16.]

13niliyekuwa kale mwenye kuwatukana na kuwafukuza na kuwakorofisha walio wake. Lakini nilihurumiwa, kwani naliyafanya pasipo kujua maana, kwani nilikuwa sijamtegemea Bwana.

14Lakini mema, Bwana wetu aliyonigawia, yakawa mengi mno, nikapata kwake Kristo Yesu kumtegemea na kumpenda.

15Neno hili ni la kweli, nalo linapasa kushikwa na watu wote la kwamba: Kristo Yesu alikuja ulimwenguni kuokoa wakosaji, ambao mimi ni wa kwanza wao,[#Luk. 19:10.]

16lakini nilihurumiwa, kusudi Kristo Yesu aonyeshe kwanza kwangu mimi uvumilivu wote, niwe kielezo chao watakaomtegemea, waupate uzima wa kale na kale.

17Mungu aliye peke yake mfalme wa kale na kale, asiye na kikomo, asiyeonwa na macho ya watu, aheshimiwe na kutukuzwa kale na kale pasipo mwisho! Amin.*[#Rom. 16:27.]

18Mwanangu Timoteo, kwa ajili ya maneno ya ufumbuaji, uliyosemewa kale, nakupa agizo hili, uyashindanie mashindano mazuri[#1 Tim. 1:5; 6:12; Yuda 3.]

19ukiwa mwenye kumtegemea Mungu na wenye moyo ujuayo yaliyo mema tu. Wengine waliutupa moyo ulio hivyo, kwa hiyo nazo nguvu zao za kumtegemea Mungu zikatota;[#1 Tim. 3:9; 6:10.]

20miongoni mwao wamo Himeneo na Alekisandro; hawa nimewatoa, Satani awashike, waonyeke, wasimbeze Mungu tena.[#1 Kor. 5:5; 2 Tim. 2:17.]

Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.
Published by: Bible Society of Tanzania