The chat will start when you send the first message.
1Neno hili ni la kweli: Mtu akitaka kazi ya ukaguzi anataka kazi nzuri.[#Tume. 20:28.]
2Mkaguzi sharti awe mtu asiye na neno la kimkanya, mwenye mke mmoja, asiyekunywa kileo, mwerevu wa kweli, mwema, mpenda wageni, ajuaye kufundisha.[#Tit. 1:5-9.]
3Asikae na wanywaji, asiwe mgomvi, ila awe mpole, pasipo matata na pasipo choyo;
4ajue kuiangalia vizuri nyumba yake mwenyewe, hata watoto wake wawe wenye kutii na kuwapa watu wote macheo.[#1 Sam. 2:12.]
5Maana mtu asiyeweza kuiangalia nyumba yake mwenyewe atawezaje kuwatunza wateule wa Mungu?
6Mtu aliye Mkristo mpya asiwe mkaguzi, asijitutume, akaja kuanguka katika hukumu ya Msengenyaji.
7Nao walioko nje sharti wamshuhudie kuwa mwema, asije kusingiziwa mabaya, akanaswa na tanzi la Msengenyaji.[#1 Tim. 5:10; 1 Kor. 5:12-13.]
8Vivyo hivyo nao watumikiaji wa wateule wawe wenye macheo, wasiosema kuwili, wasio walewi, wasiofuata machumo mabaya,[#Tume. 6:3; Fil. 1:1.]
9ila waliangalie lile fumbo walitegemealo katika mioyo itakatayo kwa kujua tu yaliyo mema.
10Hao kwanza wajaribiwe! Ikijulikana, ya kuwa haliko neno la kuwakamia, basi, wawekwe kuwa watumikiaji.[#1 Kor. 1:8.]
11Vivyo hivyo nao wake zao wawe wenye macheo wasiosengenya, wasiokunywa kileo, walio waelekevu katika mambo yote![#Tit. 2:3.]
12Watumikiaji sharti wawe kila mtu mume wa mke mmoja, wenye kuwaangalia vizuri watoto wao na nyumba zao wenyewe.[#1 Tim. 3:2.]
13Kwani waliotumika vizuri hujipatia fungu zuri, tena kwa hivyo, wanavyomtegemea Kristo Yesu, huona furaha nyingi kwa kumtangaza.
14Nakuandikia haya, ijapo nangojea, bado kidogo nifike kwako.
15Lakini kama nakawia, ujue mwenendo unaopasa katika nyumba ya Mungu! Hiyo nyumba ndio wateule wake Mungu aliye Mwenye uzima; nao ndio nguzo na msingi wa kuyashikiza yaliyo ya kweli.[#Ef. 2:19-22; 2 Tim. 2:19-20.]
16Kweli fumbo lililo kuu ni lile la kumcha Mungu: Mungu alitokea waziwazi mwilini, akapata wongofu kwa kuwa mwenye Roho, akaonekana penye malaika, akatangazwa kwa wamizimu, akategemewa ulimwenguni, akapazwa mbinguni kwenye utukufu.[#Mar. 16:19; Yoh. 1:14; 16:10; Rom. 1:3-4.]