The chat will start when you send the first message.
1Je? Tunaanza tena kujisifu wenyewe? Au tunatumia kama wengine barua za kusifiwa za kuwapelekea au za kupewa nanyi?[#2 Kor. 5:12.]
2Ninyi m barua yetu iliyoandikwa mioyoni mwetu, inatambulikana, maana inasomwa nao watu wote.[#1 Kor. 9:2.]
3Vyajulikana, ya kuwa m barua ya Kristo iliyotungwa na sisi, tulipowatumikia; haikuandikwa kwa wino, ila kwa Roho ya Mungu aliye Mwenye uzima; tena haikuandikwa katika vibao vya mawe, ila katika vibao vilivyo mioyo ya watu.[#2 Mose 24:12.]
4*Lakini Kristo ndiye aliyetupa shikizo kama hili kwake Mungu.
5Huku siko kwamba: Twafaa kuwaza neno lo lote kwa kulitoa mioyoni mwetu; kama liko, tuliwezalo, tutagawiwa na Mungu.[#2 Kor. 2:16.]
6Naye ndiye aliyetupa kuwa watumishi wafaao wa Agano Jipya lisilo la andiko, ila la Roho. Kwani andiko huua, lakini Roho hutupatia uzima.[#Yer. 31:31; Yoh. 6:63; Rom. 7:6; 1 Kor. 11:25.]
7Nao utumishi wa mambo yenye kuua, yaliyokuwa yameandikwa na kuchorwa maweni, ulikuwa na utukufu wake, ukawazuia wana wa Isiraeli kuutazama uso wake Mose kwa ajili ya utukufu wa uso wake uliokuwa wa kutoweka tena.[#2 Mose 32:15-16; 34:30.]
8Je? Utumishi wa Roho hautakuwa na utukufu kuupita ule?[#Gal. 3:2,5.]
9Kwani utumishi utupatiao hukumu ukiwa na utukufu, utumishi utupatiao wongofu utakuwa na utukufu ulio mkuu zaidi kuliko ule.*[#5 Mose 27:26; Rom. 1:17; 3:21.]
10Kwani utukufu ule uliokuwa wa kifungufungu tu tukiufananisha na utukufu huu uzidio kabisa tutasema: Ule sio utukufu!
11Kwani chenye kutoweka kikiwa na utukufu, chenye kuwapo kitakuwa na utukufu uupitao ule.
12*Kwa kuwa wenye kingojeo kama hiki sisi hutumia mioyo isiyojua woga kamwe.
13Nasi hatufanyi kama Mose aliyeufunika uso wake kwa mharuma, wana wa Isiraeli wasipate kuutazama mwisho wa yale yaliyo yenye kutoweka.[#2 Mose 34:33,35.]
14Lakini mawazo yao yakashupazwa. Kwani mpaka siku ya leo wakilisoma Agano la Kale, liko limefunikwa vivyo hivyo, lisiwafunukie kwamba: Limetimilia katika Kristo.[#Rom. 11:25.]
15Ila mpaka leo mioyo yao iko imefunikwa, Mose akisomwa.
16Lakini hapo, watakapomgeukia Bwana, ndipo, kile kifuniko kitakapoondolewa.[#Rom. 11:23,26.]
17Naye Bwana ndiye Roho; napo, Roho ya Bwana ilipo, ndipo, vyote vinapofunguliwa.
18Lakini nasi sote tunautazama utukufu wa Bwana kwa macho yasiyofunikwa, kama twauona katika kioo; ndivyo, tunavyogeuzwa, tufanane naye, tukipewa utukufu kwa utukufu, tuwe kama watu waliogeuzwa na Bwana mwenyewe aliye Roho.*