2 Yohana 1

2 Yohana 1

Anwani.

1Mimi mzee nakuandikia wewe, mke mkuu uliyechaguliwa, hata watoto wako, ninaowapenda kweli. Lakini si mimi tu ninayewapenda kweli, ila hata wote waliyoyatambua yaliyo ya kweli.[#1 Petr. 5:1; 3 Yoh. 1.]

2Tunawapenda kwa ajili ya kweli ikaayo mwetu, nasi tutakuwa nayo kale na kale.

3Upole na huruma na utengemano unaotoka kwa Mungu Baba na kwa Yesu Kristo aliye mwana wa Baba utukalie, tupendane kweli!

Kuwaepuka wapotevu.

4Nalifurahi sana kwa kuona, wengine walio watoto wako wanavyoishika njia ya kweli, kama tulivyoagizwa na Baba.

5Hata sasa nakuomba, mke mkuu tupendane; si kama nitakuandikia agizo jipya, ni lilelile, tulilokuwa nalo tangu mwanzo.[#1 Yoh. 2:7.]

6Nako kupendana ni huko, tukifanya mwenendo, kama alivyotuagiza. Hilo ndilo agizo lake, kama mlivyosikia tangu mwanzo, mwendelee na kulifuata.

7Kwani wapotevu wengi wametokea ulimwenguni wasioungama kwamba: Yesu Kristo amekuja mwenye mwili wa kimtu. Aliye hivyo ni mpotevu na mpinga Kristo.[#1 Yoh. 2:18; 4:1-3.]

8Jiangalieni, msiyapoteze mapato ya kazi zenu, ila mpewe mshahara wote![#Gal. 4:11.]

9Kila anayesogeza mpaka, asikae penye mafundisho ya Kristo, hanaye Mungu; anayekaa penye mafundisho huyu anaye Baba hata Mwana.[#1 Yoh. 2:23.]

10Mtu akija kwenu asiyeyaleta mafundisho haya, msimpokee nyumbani mwenu, wala salamu msimpe![#2 Tes. 3:6.]

11Kwani mwenye kumsalimia huwa mwenziwe wa kazi zake mbaya.

12Ninayo mengi ya kuwaandikia ninyi, lakini sikutaka kuyamaliza kwa karatasi na wino, ila nangojea kwamba: Nitakuja kwenu na kusema nanyi kinywa kwa kinywa, furaha yetu itimie.[#3 Yoh. 13.]

13Watoto na dada yako aliyechaguliwa naye wanakusalimu. Amin.

Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.
Published by: Bible Society of Tanzania