The chat will start when you send the first message.
1Ikawa, Dawidi alipomwuliza Bwana baadaye kwamba: Nipande kukaa katika mji mmoja wa Yuda? Bwana akamwambia: Panda! Dawidi akauliza tena: Nipande kukaa wapi? Akamwambia: Heburoni.[#1 Sam. 30:8.]
2Ndipo, Dawidi alipopanda kukaa huko pamoja na wakeze wawili, Ahinoamu wa Izireeli na Abigaili, mkewe Nabali wa Karmeli.[#1 Sam. 25:42-43.]
3Nao wale watu waliokuwa naye Dawidi akawapandisha kila mtu na mlango wake, wakakaa katika miji ya Heburoni.
4Kisha waume wa Yuda wakaja, wakampaka Dawidi mafuta, awe mfalme wa mlango wa Yuda. Nao wakampasha Dawidi habari, ya kuwa watu wa Yabesi wa Gileadi wamemzika Sauli.[#1 Sam. 16:13; 31:12; 2 Sam. 5:3.]
5Dawidi akatuma wajumbe kwa watu wa Yabesi wa Gileadi, akawaambia: Na mbarikiwe na Bwana ninyi, kwa kuwa bwana wenu Sauli mmemfanyizia tendo lililo jema la kumzika!
6Sasa Bwwana na awafanyizie nanyi matendo yanayoelekea kuwa mema kweli, mimi nami na niwarudishie wema huo, kwa kuwa mmefanya jambo hilo.
7Sasa na mwikaze mikono yenu, mpate nguvu, kwani bwana wenu Sauli amekufa, tena mimi nami wao wa mlango wa Yuda wamenipaka mafuta, niwe mfalme wao.
8Naye Abineri, mwana wa Neri, aliyekuwa mkuu wa vikosi vya Sauli, akamchukua Isiboseti, mwana wa Sauli, akampeleka Mahanaimu,[#1 Sam. 14:50.]
9akamfanya kuwa mfalme wa Gileadi na wa Asuri na wa Izireeli na wa Efuraimu na wa Benyamini na wa Waisiraeli wote.
10Isiboseti, mwana wa Sauli, alikuwa mwenye miaka 40 alipoupata ufalme wa Waisiraeli, akawa mfalme miaka 2; ni wao wa mlango wa Yuda tu waliomfuata Dawidi.
11Nayo hesabu ya siku, Dawidi alizokuwa mfalme wa mlango wa Yuda huko Heburoni, ikawa miaka 7 na miezi 6.
12Abineri, mwana wa Neri, akatoka Mahanaimu na watumishi wa Isiboseti, mwana wa Sauli, kwenda Gibeoni.
13Ndipo, Yoabu, mwana wa Seruya, alipotoka naye na watumishi wake Dawidi, wakakutana penye ziwa la Gibeoni; hao wakakaa ng'ambo ya huku ya hilo ziwa, nao wale wakakaa ng'ambo ya pili ya hilo ziwa.
14Abineri akamwambia Yoabu: Na waondokee vijana, wacheze mbele yetu! Yoabu akaitikia: Haya! Na waondokee!
15Basi, wakaondoka, wakaja kusimama huku na huko kwa kuhesabiwa: 12 wa Benyamini na wa Isiboseti, mwana wa Sauli, tena 12 watumishi wa Dawidi.
16Wakakamatana kila mtu kichwa cha mwenzake, wakachomana panga kila mtu ubavuni mwa mwenzake, kwa hiyo wakaanguka wote pia, wakafa. Wakapaita mahali pale Fungu lenye Mapanga Makali lililoko Gibeoni.
17Kisha mapigano yakawa makali sanasana siku hiyo, Abineri na watu wa Waisiraeli wakashindwa na watumishi wake Dawidi.
18Wakawako wana watatu wa Seruya, Yoabu na Abisai na Asaheli; naye Asaheli alikuwa mwepesi kwa kupiga mbio kama paa wanaokaa porini.[#1 Mambo 2:16.]
19Naye Asaheli akamkimbiza Abineri na kumfuata, hakujielekeza kwenda kuumeni wala kushotoni, asiache kumfuata Abineri.
20Abineri akageuka nyuma, akamwuliza: Wewe siwe Asaheli? Akasema: Ndimi!
21Abineri akamwambia: Geuka kuumeni kwako au kushotoni kwako, ukamate kijana mmoja, uchukue mata yake! Lakini Asaheli akakataa kuondoka kwake na kuacha kumfuata.
22Abineri akamwambia Asaheli mara ya pili: Ondoka, uache kunifuata! Kwa nini nikupige, uanguke chini? Nitawezaje kutokea usoni pa kaka yako Yoabu?
23Alipokataa kabisa kumwondokea, Abineri akamchoma tumboni kwa ncha ya chini ya mkuki, mkuki ukatokea mgongoni; ndipo, alipoanguka chini, akafa papo hapo. Ikawa, wote waliofika hapo, Asaheli alipoanguka chini akifa, wakasimama hapo.[#2 Sam. 3:27.]
24Kisha Yoabu na Abisai wakamkimbiza Abineri; jua lilipokuchwa walikuwa wamefika kwenye kilima cha Ama kielekeacho Gia penye njia ya kwenda nyikani kwa Gibeoni.
25Ndipo, wana wa Benyamini walipokusanyika, wamfuate Abineri, wakawa kikosi kimoja, wakasimama juu ya kilima kimoja.
26Hapo Abineri akamwita Yoabu kwamba: Je? Upanga na ule kale na kale? Hujui, ya kuwa mwisho wake utakuwa uchungu? Utangoja mpaka lini, uwaambie hao watu, warudi na kuacha kuwafuata ndugu zao?
27Yoabu akasema: Hivyo, Mungu alivyo Mwenye uzima, kama ungalisema hivyo asubuhi, watu wangalikwenda zao na kuacha kukimbizana kila mtu na ndugu yake.
28Kisha Yoabu akapiga baragumu; ndipo, watu wote waliposimama, hawakuwakimbiza tena Waisiraeli, wala hawakuendelea kupigana nao.
29Abineri na watu wake wakashika njia ya kupita jangwani usiku kucha, kisha wakavuka Yordani, wakapita Bitironi yote, kisha wakafika Mahanaimu.
30Yoabu naye akarudi, akaacha kumfuata Abineri, akawakusanya watu wake wote; ndipo, ilipoonekana kwa watumishi wa Dawidi, ya kuwa watu 19 hawako, tena Asaheli.
31Lakini watumishi wa Dawidi walipiga kwao Wabenyamini na kwa watu wa Abineri watu 360; ndio waliokufa.
32Wakamchukua Asaheli, wakamzika katika kaburi la baba yake lililoko Beti-Lehemu; kisha Yoabu na watu wake wakaenda usiku kucha, nao walipofika Heburoni, kukapambazuka.