2 Timoteo 2

2 Timoteo 2

Askari mwema wa Kristo.

1Basi wewe mwanangu, ujipatie nguvu, tunazogawiwa tukiwa wake Kristo Yesu!

2Nayo mambo, uliyoyasikia kwangu mbele yao wengi waliosikiliza, hayo uwalimbikishe watu welekevu watakaoweza kufundisha hata wengine.

3Vumilia ukiteswa vibaya pamoja nami, kama inavyompasa askari mzuri wa Kristo Yesu![#2 Tim. 1:8; 4:5-8.]

4Hakuna askari wa kwenda vitani anayejitia katika machumo ya pamba, ampendeze yule mwenye vita.

5Lakini mtu angawa anashindana, hafungwi kilemba asiposhinda kikweli.[#2 Tim. 4:8.]

6Mkulima ajisumbuaye na kulima imempasa kuyalimbua matunda.[#1 Kor. 9:7.]

7Itambue maana yao, nisemayo! Kwani Bwana atakupa utambuzi katika mambo yote.

8*Mkumbuke Yesu Kristo aliyefufuliwa katika wafu, aliyezaliwa katika uzao wa Dawidi, kama nilivyoutangaza Utume mwema.[#2 Sam. 7:12; 1 Kor. 15:4,20.]

9Kwa ajili yake nateseka vibaya, mpaka nikifungwa kama mwenye maovu, lakini Neno la Mungu halifungiki.[#Ef. 3:1,13; Fil. 1:12-14; 2:17.]

10Kwa hiyo nayavumilia yote kwa ajili yao waliochaguliwa, kwamba nao waupate wokovu uliomo mwake Kristo Yesu, wafike penye utukufu wa kale na kale.[#Kol. 1:24.]

11Neno hili ni la kweli: Kama tumekufa pamoja naye;[#2 Kor. 4:11.]

12kama twavumilia pamoja naye, tutatawala pamoja naye; kama tutakana kwamba: Hatu wake, naye atatukana sisi;[#Mat. 10:33.]

13kama hatumtegemei, yeye hufuliza kuwa mwelekevu, kwani hawezi kujikana mwenyewe.*[#4 Mose 23:9; Rom. 3:2-3.]

Kuepusha wapuzi.

14Wakumbushe mambo hayo na kuwaonya mbele yake Mungu, wasibishane! Maana haifai kitu, huwapotoa tu wenye kusikiliza.[#1 Tim. 6:4; Tit. 3:9.]

15Jipingie kujitokeza kwa Mungu kuwa mfanya kazi aliye wa kweli, asiyefanya mambo yenye soni, anayelilinganisha vema neno la kweli, atakalogawia watu![#1 Tim. 4:6; Tit. 2:7-8.]

16Lakini penye upuzi wa bure usio na maana uepuke! Kwani wako watakaoendesha mambo ya kumbeza Mungu,[#1 Tim. 4:7.]

17nalo neno lao litaambukiza kama ukoma; miongoni mwao hao wamo Himeneo na Fileto[#1 Tim. 1:20.]

18waliopotelewa nayo yaliyo ya kweli wakisema: Ufufuko umekwisha kuwapo. Ndivyo, walivyokosesha hata wengine, wasimtegemee Bwana tena.

19Lakini msingi, Mungu aliouweka, uko, umeshupaa vivyo hivyo, hujulikana kwa muhuri yake, ni hii: Bwana huwatambua walio wake! Tena: Kila mwenye kulitambikia Jina la Bwana atenguke penye upotovu![#4 Mose 16:5; Yoh. 10:14,27.]

20Katika nyumba kubwa hamna vyombo vya dhahabu au vya fedha tu, ila vimo hata vyombo vya miti na vya udongo; navyo vingine ni vya mapambo, vingine ni vya machafu.

21Mtu akiwaepuka wale watu, asijichafue, atakuwa chombo cha pambo kilichotakaswa, naye mwenye nyumba atakitumia, maana kimefalia kazi zote zilizo njema.

Kuzikimbia tamaa.

22Tamaa za ujana zikimbie, ukimbilie kupata wongofu na kumtegemea Mungu na kupendana na kupatana nao wote wanaomtambikia Bwana kwa mioyo itakatayo![#1 Tim. 6:11.]

23Lakini mabishano ya upuzi wa watu wasioonyeka yakatae! Jua, ya kuwa huleta magombano tu![#1 Tim. 4:7.]

24Lakini aliye mtumwa wa Bwana haimpasi kugombana, sharti awaendee wote kwa unyenyekevu akijua kuwafundisha, akivumilia wenye uovu.[#Tit. 1:7.]

25Akiwa mpole hivyo ataweza kuwaonya wapingani nao, kama Mungu anawajutisha, wayatambue yalio ya kweli;

26kisha watalevuka, wajinasue matanzini mwa Msengenyaji, ambaye walinaswa naye, wamfanyizie, ayatakayo yeye.

Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.
Published by: Bible Society of Tanzania