2 Timoteo 4

2 Timoteo 4

Mashindano ya Kikristo.

1Namtaja Mungu naye Kristo Yesu atakayewahukumu wanaoishi hata waliokufa, awe shahidi, nikikuagiza haya: Kwa hivyo, atakavyotokea, ausimike ufalme wake,[#1 Petr. 4:5.]

2litangaze Neno! Fuliza hivyo, pafaapo napo pasipofaa! Waonyeshe ubaya wao, wagombeze, wakanye ukiwaendea kna uvumilivu wote pamoja na kuwafundisha![#Tume. 20:20,31.]

3Kwani siku zinakuja, watakapoukataa ufundisho utupao uzima, ila kwa hivyo, watakavyozifuata tamaa zao wenyewe, watajitafutia wafunzi wengi wa kuwafundisha yapendezayo masikioni pao.[#2 Tim. 1:13; 1 Tim. 4:1.]

4Nao watajigeuza, wasiyasikilize tena yaliyo ya kweli, wayageukie yalio masimulio tu.[#1 Tim. 4:7; 2 Tes. 2:11.]

5*Lakini wewe levuka katika mambo yote! Vumilia ukiteswa vibaya! Fanya kazi ya mpiga mbiu njema! Utimize utumishi wako![#2 Tim. 2:3.]

6Kwani mimi pamenifikia, niwe ng'ombe ya tambiko, nayo siku yangu ya kufunguliwa kutoka ulimwenguni iko karibu.[#Fil. 2:17.]

7Nimelishindania shindano zuri, nimeimaliza mbio, sikuacha kumtegemea Bwana.[#1 Kor. 9:25; Fil. 3:14; 1 Tim. 6:12.]

8Lisaalo ni kufungwa kilemba kipasacho waongofu, nilichowekewa nami Siku ile nitakipata kwake Bwana aliye mhukumu mwenye kweli; lakini si mimi tu atakayekipata, ila nao wote waliokuwa wamempenda, atokee waziwazi.*[#2 Tim. 2:5; Mat. 25:21; Yak. 1:12; 1 Petr. 5:4; Ufu. 2:10.]

Habari nyinginenyingine.

9Jikaze, ufike kwangu upesi![#2 Tim. 1:4; 4:21.]

10Kwani Dema ameniacha, kwa kuyapenda mambo ya dunia hii akaenda zake Tesalonike. Kreske amekwenda zake Galatia, Tito amekwenda zake Dalmatia.[#Kol. 4:14.]

11Luka peke yake yuko pamoja nami. Mchukue Marko, uje pamoja naye! Kwani hunitumikia vizuri sana.[#Tume. 15:37; Kol. 4:10.]

12Tikiko nalimtuma Efeso.[#Tume. 20:4; Ef. 6:21; Kol. 4:7.]

13Utakapokuja ulete na lile joho gumu, nililoliacha huko Tiroa kwa Karpo! Vilete hata vile vitabu! Nivitakavyo sana, ni vile vya ngozi.

14Alekisandro, yule mfua shaba amenifanyia maovu mengi; Bwana atamlipa, kama matendo yake yalivyo.[#2 Sam. 3:39; Sh. 28:4; 1 Tim. 1:20.]

15Hata wewe ujilinde kwa ajili ya mtu huyo, kwani ameyapinga sana maneno yetu.

16Nilipojikania mara ya kwanza, hakuwapo hata mmoja aliyesimama upande wangu, wote waliniacha. Wasihesabiwe jambo hili![#2 Tim. 1:15.]

17Lakini Bwana alisimama upande wangu, akanipa nguvu, maana alitaka, ile mbiu itimizwe nami mimi, wamizimu wote wapate kuisikia. Nami nikaokolewa kinywani mwa simba.[#Tume. 23:11; 27:23.]

18Naye Bwana akaniokoa katika mambo mabaya yo yote, nipone, niingie katika ufalme wake wa mbinguni. Yeye atukuzwe siku zote kale na kale! Amin.

19Nisalimie Puriska na Akila walio wa nyumbani mwa Onesifiro![#2 Tim. 1:16; Tume. 18:2; Rom. 16:3.]

20Erasto alisalia Korinto, Tirofimo nalimwacha mgonjwa Mileto[#Tume. 19:22; 20:4; 21:29.]

21Jikaze, ufike, siku za kipupwe zitakapokuwa hazijatimia! Wanakusalimu Eubulo na Pude na Lino na Klaudia na ndugu wote.

22Bwana awe na roho yako! Upole uwakalie ninyi! Amin.

Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.
Published by: Bible Society of Tanzania