The chat will start when you send the first message.
1Mimi mzee nakuandikia wewe Gayo, mpendwa wangu, ninayempenda kweli.[#2 Yoh. 1.]
2Mpendwa, kuliko yote nakuombea, ukae vema na kuwa mzima, kama roho yako inavyokaa vema.
3Kwani nalifurahi sana, ndugu walipokuja na kutushuhudia, kuwa u mwenye kweli, kama wewe unavyoishika njia ya kweli.[#2 Yoh. 4.]
4Hakuna linalonifurahisha kuliko lile la kusikia, ya kuwa watoto wangu huishika njia ya kweli.
5Mpendwa, u mwelekevu katika yote, unayowafanyia ndugu walio wageni.
6Nao walikushuhudia mbele ya wateule, unavyowapenda. Kwa hiyo utafanya vizuri utakapowasindikiza, kama inavyowapasa walioko mbele ya Mungu.[#Rom. 15:24; Tit. 3:13.]
7Kwani walitoka kulitangaza Jina lake tu, hawataki kupewa cho chote kwa watu wa kimizimu.[#Tume. 20:35; 1 Kor. 9:12,15.]
8Nasi imetupasa kuwapokea watu kama hao, tusaidiane kufanya kazi za kweli.[#Ebr. 13:2.]
9Yako mengine, niliyoyaandikia wateule. Lakini Diotirefe anayependa kuwa mkubwa wao hatusikii sisi.
10Kwa hiyo nitakapokuja nitazikumbusha kazi zake, anazozifanya akituteta sisi kwa maneno mabaya. Nayo hayo hayamtoshi: mwenyewe hawapokei ndugu, nao wanaotaka kuwapokea huwazuia, kisha huwafukuza kwenye wateule.
11Mpendwa, usiuige uovu, ila uuige wema! Anayefanya yaliyo mema ni wa Kimungu; anayefanya yaliyo maovu hakumwona Mungu.[#1 Yoh. 3:6,9.]
12Lakini Demetirio hushuhudiwa nao wote, naye hushuhudiwa kweli. Hata sisi twamshuhudia, nawe wajua, ya kuwa ushahidi wetu ni wa kweli.[#Yoh. 19:35; 21:24.]
13Nalikuwa nayo mengi ya kukuandikia, lakini sitaki kukuandikia tu kwa wino na kalamu,[#2 Yoh. 12.]
14ila nangojea, nikuone upesi, tusemeane kinywa kwa kinywa.
15Utengemano ukukalie! Wapenzi wanakusalimu. Nisalimie wapenzi kila kwa jina lake!