The chat will start when you send the first message.
1Hayo yote nikayaweka moyoni mwangu na kuyachunguza haya yote, ya kuwa waongofu na werevu wa kweli pamoja na kazi zao zote wamo mkononi mwa Mungu. Hakuna mtu ajuaye, kama ni kupenda au kama ni kuchukia kumpasako, yote pia yako yamefichika bado mbele yake.
2Kwani yote huwapata wote sawasawa, jambo lao la mwisho ni lilo hilo moja, humpata mwongofu naye asiyemcha Mungu, vilevile mwema atakataye naye mchafu, atambikaye naye asiyetambika, mwema na mkosaji, aapaye naye aogopaye kuapa;[#Mbiu. 2:14; Iy. 9:22.]
3yote yanayofanywa chini ya mbingu yako na ubaya huu, jambo la mwisho likiwa lilelile moja kwao wote; tena ni huu, mioyo ya wana wa Adamu ikijaa mabaya, mumo humo mioyoni mwao mkikaa upumbavu siku za maisha yao, kisha huenda kwao wafu, ndio mwisho wao.[#Mbiu. 8:11.]
4Mtu akingali mwenye bia nao wote walio hai hutegemeka, kwani mbwa aliye hai hupata mema kuliko simba aliyekufa.
5Kwani walio hai hujua, ya kuwa watakufa, lakini wafu hawajui cho chote, tena hakuna mshahara wo wote, watakaoupata, kwani hawakumbukwi tena, wamekwisha kusahauliwa.
6Nao upendo wao na uchukivu wao na wivu wao ulitoweka kale, kale na kale hawana fungu lo lote tena katika mambo yote yanayofanywa chini ya jua.
7Jiendee, ule chakula chako kwa kufurahi, kanywe mvinyo yako kwa kuwa na moyo mwema! Kwani kazi zako zilimpendeza Mungu tangu kale.[#Mbiu. 5:18.]
8Kavae nguo nyeupe siku zote, nacho kichwa chako kisikose mafuta!
9Kazifurahie siku za kuwapo pamoja na mkeo, umpendaye, siku zote za maisha yako zilizo za bure, Mungu alizokupa chini ya jua; kavifanye siku zako zote zilizo za bure! Kwani haya ndiyo, unayojipatia huku nchini kwa masumbuko yako, unayoyasumbuka chini ya jua.[#Fano. 5:18.]
10Yote, mkono wako utakayoyaona ya kuyafanya kwa nguvu yako, yafanye! Kwani kuzimuni, unakokwenda wewe, hakuna matendo wala mawazo wala ujuzi wala werevu wa kweli.
11Nilipoyatazama tena yaliyoko chini ya jua, nikaona, ya kuwa sio wepesi washindao katika mashindano ya mbio, wala sio mafundi wa vita washindao vitani, wala sio werevu wa kweli wapatao vilaji, wala sio watambuzi wapatao mali, wala sio wajuzi wapendezao, kwani wao wote kila mmoja wao huwa na siku zake na mambo yake yatakayompata.[#Yer. 10:23.]
12Mtu hazijui siku zake zimfaazo, huwa kama samaki wanaokamatwa katika wavu mbaya au kama videge wanaonaswa tanzini; vivyo hivyo nao wana wa Adamu hunaswa, siku zao zikiwa mbaya, nayo mabaya yakiwaangukia na kuwastusha.
13Nilipoutazama tena werevu wa kweli ulioko chini ya jua, nikauona kuwa mkubwa.
14Kulikuwa na mji mdogo, nao waume waliomo walikuwa wachache; kisha mfalme akaujia, akauzinga, akaujengea maboma makubwa.
15Basi, mle mjini akaonekana maskini mwenye werevu wa kweli, akauponya ule mji kwa huo werevu wake uliokuwa wa kweli; lakini baadaye hakuwako mtu aliyemkumbuka huyo maskini.
16Nikasema: Werevu wa kweli hufaa kuliko nguvu, lakini werevu wa maskini, ijapo uwe wa kweli, hubezwa, nayo maneno yake hayasikilizwi.
17Maneno ya werevu wa kweli wakiyasikiliza na kutulia hufaa kuliko makelele, mtawalaji anayoyapiga kwa wajinga.
18Werevu wa kweli hufaa kuliko vyombo vya vita, naye mkosaji mmoja huangamiza mema mengi.