The chat will start when you send the first message.
1Kisha akamwambia Mose: Panda kwake Bwana, wewe pamoja na Haroni na Nadabu na Abihu, tena wazee 70 wa Waisiraeli, mniangukie mngaliko mbali![#4 Mose 11:16.]
2Kisha Mose na aende peke yake kufika kwake Bwana, lakini wale watu wengine wasifike karibu, wasipande naye.
3Mose akaja, akawasimulia hao watu maneno na maamuzi yote ya Bwana; nao watu wote wakaitikia kwa kinywa kimoja wakisema: Maneno yote, Bwana aliyoyasema, tutayafanya.[#2 Mose 19:8.]
4Kisha Mose akayaandika maneno yote ya Bwana, akajidamka asubuhi, napo hapo chini penye huo mlima akajenga pa kutambikia, akapasimamishia nguzo kumi na mbili kwa hesabu ya mashina kumi na mawili ya Waisiraeli.[#2 Mose 34:27; 1 Fal. 18:31.]
5Akatuma vijana wa wana wa Isiraeli, watolee hapo ng'ombe za tambiko za kuteketezwa nzima na kumchinjia Bwana ndama waume kuwa ng'ombe za tambiko za shukrani.[#2 Mose 3:12.]
6Mose akachukua nusu ya damu zao, akazitia katika mabakuli, nazo nyingine akazimwagia hapo pa kutambikia.
7Kisha akakichukua Kitabu cha Agano, akakisoma masikioni pa watu; nao wakaitikia kwamba: Yote, Bwana aliyoyasema, tutayafanya kwa kumtii.[#2 Mose 24:4.]
8Ndipo, Mose alipozichukua zile damu, akawanyunyizia watu akisema: Tazameni! Hizi ni damu za Agano, Bwana alilolifanya nanyi na kuwaambia haya maneno yote.[#Ebr. 9:19-22.]
9Kisha Mose na Haroni, Nadabu na Abihu, pamoja na wale wazee 70 wa Waisiraeli wakapanda,
10wakamwona Mungu wa Isiraeli, napo chini ya miguu yake palikuwa kama mahali palipotengenezwa kwa mawe ya safiro yaangazikayo au kama mbingu zenyeye kwa kutakata kwake.[#Ez. 1:26.]
11Lakini hawa wateule wa wana wa isiraeli hakuwapatia kibaya cho chote kwa mkono wake, ila walikuwapo vivyo hivyo wakila, wakinywa, ijapo walikuwa wamemwona Mungu.
12Kisha Bwana akamwambia Mose: Panda mlimani, ufike kwangu kuwa huku! Nami nitakupa mbao za mawe zenye Maonyo na maagizo, niliyoyaandika humo, upate kuwafunza.[#2 Mose 31:18.]
13Ndipo, Mose alipoinuka pamoja na mtumishi wake Yosua, naye Mose akapanda mlimani kufika kwake Mungu.
14lakini wale wazee aliwaambia: Kaeni hapa, mpaka tutakaporudi kwenu! Tazameni, Haroni na Huri mnao! Mtu akiwa na neno, na aje kwao!
15Mose alipopanda mlimani, wingu likaufunika huo mlima.
16Nao utukufu wa Bwana ukaja kukaa juu ya mlima wa sinai, nalo wingu likaufunika siku sita. Siku ya saba akamwita Mose toka winguni.[#2 Mose 16:10.]
17Nao utukufu wa Bwana ukaonekana machoni pao wana wa Isiraeli kuwa kama moto ulao huko juu mlimani.[#5 Mose 4:24; 9:3; Ebr. 12:29.]
18Mose akaingia mle winguni katikati alipoupanda huo mlima. Mose akawa huko mlimani siku 40 mchana kutwa na usiku kucha.