The chat will start when you send the first message.
1Kisha tengeneza meza ya kutambikia kwa mbao za migunga! Urefu wake uwe mikono mitano, nao upana wake uwe mikono mitano, hiyo meza iwe sawa pande zote nne, nao urefu wake wa kwenda juu uwe mikono mitatu.
2Pembe zake zinazoipasa uzitie penye pembe zake nne, nazo hizi pembe zake ziwe za mti huohuo mmoja. Kisha hiyo meza uifunikize shaba.
3Navyo vyombo vyake vya kuondolea majivu na majembe yake na vyano vyake na nyuma zake na sinia zake, vyombo vyake vyote pia uvitengeneze kwa shaba.
4Kisha utengeneze kikingio kinachofanana na wavu wa shaba, uweke hata mapete manne ya shaba juu ya huo wavu penye pembe zake nne.
5Huu wavu uuweke chini ya ukingo wa meza ya kutambikia kuelekea chini, huu wavu ufike hapo mpaka katikati ya meza ya kutambikia.
6Kisha meza ya kutambikia ifanyizie mipiko, hii mipiko iwe ya migunga, nayo uifunikize shaba.
7Kisha mipiko itiwe katika mapete, hii mipiko iwe pande mbili za meza ya kutambikia, wakiichukua.
8Uitengeneze kwa mbao, iwe yenye mvungu ndani ulio wazi; kama alivyokuonyesha mlimani, ndivyo waifanye.[#2 Mose 26:30.]
9Kisha utengeneze ua wa hilo kao upande wa kusini ulio wa juani, nguo za huo ua zitengenezwe kwa bafta ngumu, nao urefu wa upande mmoja uwe mikono mia.
10Nguzo zake ishirini ziwe zenye miguu yao ishirini ya shaba; vifungo vya nguzo na vijiti vyao vya kuziungia juu viwe vya fedha.
11Hata upande wa kaskazini viwe vivyo hivyo: nguo ziwe zenye urefu wa mikono mia, nazo nguzo zao ishirini ziwe zenye miguu yao ishirini ya shaba, navyo vifungo vya nguzo na vijiti vyao vya kuziungia juu viwe vya fedha.
12Nao upande wa ua unaoelekea baharini uwe wenye nguo ya mikono hamsini na nguzo zake ziwe kumi zenye miguu yao ya shaba kumi.
13Nao upana wa upande wa maawioni kwa jua uwe mikono hamsini.
14Nguo yake upande wa huku iwe ya mikono kumi na mitano, nazo nguzo zake ziwe tatu zenye miguu ya shaba mitatu.
15Nao upande wa huko nguo yake iwe ya mikono kumi na mitano, nazo nguzo zake ziwe tatu zenye miguu yao ya shaba mitatu.
16Hapo kati liwe lango la ua lenye pazia la mikono ishirini lililotengenezwa kwa nguo za kifalme nyeusi na nyekundu na kwa nguo za bafta ngumu, lifumwe nao wanaojua kufuma kwa nyuzi za rangi. Nguzo zake ziwe nne zenye miguu minne.
17Nguzo zote zinazouzunguka ua ziwe zimeungwa kwa vijiti vya fedha, navyo vifungo vyao viwe vya fedha, lakini miguu yao iwe ya shaba.
18Urefu wa ua uwe mikono mia, nao upana mikono hamsini, nao urefu wa kwenda juu mikono mitano. Nguo yake iwe ya bafta ngumu, nayo miguu yake iwe ya shaba.
19Navyo vyombo vyote vya hili kao vinavyotumika kwa kazi yo yote na mambo zake zote nazo mambo za ua ziwe za shaba.
20Kisha wewe uwaagize wana wa Isiraeli, wakupatie mafuta ya chekele yaliyotwangwa vema kuwa safi ya kinara ya kutia siku zote katika taa zake.[#3 Mose 24:2.]
21Katika Hema la Mkutanao hapo nje ya pazia lililoko penye Sanduku la Ushahidi Haroni na wanawe wazitengeneze hizo taa, ziwake tangu jioni hata asubuhi mbele ya Bwana pasipo kukoma. Maongozi haya na yawe ya kale na kale kwa vizazi vyao kwa wana wa Isiraeli.