The chat will start when you send the first message.
1Neno la Bwana likanijia la kwamba:
2Mwana wa mtu, sema nao walio ukoo wako ukiwaambia: Kama ninailetea nchi panga, watu wa nchi hiyo watamchukua mtu mmoja miongoni mwao, wamweke kuwa mlinzi wao.
3Atakapoziona panga, zikiijia hiyo nchi, atapiga baragumu, awaonye wale watu.
4Lakini mtu akiisikiliza tu sauti ya baragumu pasipo kuonyeka, panga zitamkamata, nayo damu yake atatwikwa yeye kichwani.
5Akiisikia sauti ya baragumu pasipo kuonyeka, damu yake atatwikwa yeye, lakini yeye aonyekaye ataiponya roho yake.
6Lakini kama mlinzi anaona, panga zikija, asipige baragumu, watu hawaonyeki; basi, panga zikija, zikimkamata mtu mmoja tu wa kwao, yeye atakamatwa kwa ajili ya manza, alizozikora, lakini damu yake nitamlipisha mlinzi.
7Wewe nawe, mwana wa mtu, nimekuweka kuwa mlinzi wa mlango wa Isiraeli, utakaposikia neno kinywani mwangu, sharti uwaonye na kuwaambia hilo neno langu.[#Ez. 3:17-19; Yes. 56:10; Ebr. 13:17.]
8Nikimwambia asiyenicha: Wewe usiyenicha, utakufa kabisa, nawe humwambii neno hili la kumwonya asiyenicha, aiache njia yake, basi, yeye asiyenicha atakufa kwa ajili ya manza, alizozikora, lakini damu yake nitaitaka mkononi mwako.
9Lakini kama wewe ulimwonya asiyenicha kwa ajili ya njia yake na kumwambia, arudi na kuiacha hiyo njia yake, naye asiporudi na kuiacha hiyo njia yake basi, yeye atakufa kwa manza, alizozikora, lakini wewe utakuwa umeiponya roho yako.
10*Kwa hiyo, wewe mwana wa mtu, uambie mlango wa Isiraeli: Ninyi husema hivi kwamba: Tukitwikwa mapotovu yetu na makosa yetu, sisi tutazimia tu; hivyo tutawezaje kupata uzima?
11Waambie: Ndivyo, asemavyo Bwana Mungu: Hivyo, nilivyo Mwenye uzima, sipendezwi na kufa kwake asiyenicha, ila yeye asiyenicha, akirudi na kuiacha njia yake, apate uzima. Rudini! Rudini na kuziacha njia zenu mbaya! Kwa nini mnataka kufa, ninyi mlio mlango wa Isiraeli?[#Ez. 18:23,31-32; Yes. 55:7; Yoe. 2:12-13.]
12Nawe mwana wa mtu, waambie wana wa ukoo wako: Wongofu wa mwongofu hautamponya siku, atakapofanya mapotovu, wala asiyenicha hataangushwa kwa hivyo, asivyonicha, siku atakaporudi na kunicha, wala mwongofu hatapata uzima kwa wongofu wake siku, atakapokosa.[#Ez. 3:20; 18:24.]
13Nikimwambia mwongofu, ya kuwa atapata uzima, naye akiuegemea wongofu wake, afanye mapotovu, basi, wongofu wake wote hautakumbukwa tena, naye atakufa kwa ajili ya hayo mapotovu, aliyoyafanya.
14Tena nikimwambia asiyenicha: Utakufa kabisa, naye akirudi na kuyaacha makosa yake, afanye yaliyo sawa yaongokayo:
15yeye asiyenicha akirudisha aliyopewa ya kumwekea mtu, akilipa aliyoyanyang'anya watu, akiyafuata maongozi ya wenye uzima, basi, naye ataupata uzima wa kweli, asife kabisa.[#Ez. 18:7; Luk. 19:8.]
16Makosa yake yote, aliyoyakosa, hayatakumbukwa tena; kwa kuwa amefanya yaliyo sawa yaongokayo, ataupata uzima wa kweli.*
17Wana wa ukoo wako husema: Njia ya Bwana hainyoki, lakini njia yao ndiyo isiyonyoka.[#Ez. 18:25-30.]
18Mwongufu akirudi na kuuacha wongofu wake, afanye mapotovu, atakufa kwa ajili yao.
19Tena asiyemcha Mungu akirudi, aje kumcha Mungu, afanye yaliyo sawa yaongokayo, basi, yeye atapata uzima.
20Mkisema: Njia ya Bwana hainyoki, kwa hiyo nitawapatiliza ninyi mlio mlango wa Isiraeli kila mtu, kama njia zake zilivyo.
21Ikawa katika mwaka wa 12 wa kuhamishwa kwetu siku ya tano ya mwezi wa kumi, ndipo, mtoro aliyetoka Yerusalemu aliponijia kuniambia: Umetekwa ule mji![#Ez. 24:26.]
22Lakini mkono wake Bwana ulikuwa juu yangu jioni kabla ya kuja kwake yule mtoro, naye alinifumbua kinywa, mpaka yule akinijia asubuhi; ndivyo, nilivyofumbuliwa kinywa, nisiwe tena bubu kabisa.
23Neno la Bwana likanijia la kwamba:[#Yes. 51:2; Mal. 2:15.]
24Mwana wa mtu, watu wayakaliayo yale mabomoko katika nchi ya Isiraeli husema kwamba: Aburahamu alikuwa mmoja tu, akaipata nchi hii, iwe yake; nasi tulio wengi tulipewa nchi hii, iwe yetu.
25Kwa hiyo waambie: Hivi ndivyo, Bwana Mungu anavyosema: Ninyi hula nyama zenye damu, tena huyaelekezea magogo yenu ya kutambikia macho yenu, tena humwaga damu za watu! Je? Hivyo mtaipata nchi hii, iwe yenu?
26Ninyi hujishikiza kwa panga zenu, hufanaya machukizo mkichafua kila mtu mke wa mweziwe! Je? Hivyo mtaipata nchi hii, iwe yenu?
27Sharti uwaambie hivi: Hivi ndivyo, Bwana Mungu anavyosema: Hivyo, nilivyo Mwenye uzima, wayakaliao yale mabomoko watauawa kwa panga, nao walioko shambani nitawatoa, waliwe na nyama wa porini, nao walioko vilimani ngomeni na mapangoni watakufa kwa magonjwa mabaya.
28Nitaigeuza nchi hii kuwa mapori yaliyo peke yao, niyakomeshe majivuno yao ya nguvu zao, milima ya Isiraeli itakapokuwa peke yao, kwa kuwa hatapapita mtu.
29Ndipo, watakapojua, ya kuwa mimi ni Bwana, nitakapoigeuza nchi hii kuwa mapori yaliyo peke yao kwa ajili ya machukizo yote, waliyoyafanya.
30Nawe mwana wa mtu, wana wao walio ukoo wako huzisimulia habari za kwako barazani namo milangoni mwa nyumba, husemezana kila mmoja na mwenziwe, kila mtu na ndugu yake kwamba: Njoni, msikie, kama ni neno gani lililotoka kwake Bwana!
31Hivyo wanakujia kama watu wanaojijilia tu, kisha wao walio ukoo wangu hujikalia mbele yako, wayasikilize maneno yangu, lakini hawayafanyi; kwa vinywa vyao husema maneno mazuri ya kupendeza, lakini kwa kufanya hao hushika mioyoni mwao njia za kupata faida tu.[#Yes. 53:1; Yak. 1:22.]
32Tazama, wewe unakuwa kwao kama mtu mwenye sauti nzuri aimbaye wimbo wa kupendeza pamoja na kuupatanisha na marimba; huyasikia maneno yako, lakini hawayafanyi kabisa.
33Hapo, yatakapotimia, - nayo yatatimia kweli, - ndipo, watakapojua, ya kuwa ni mfumbuaji aliyekuwa katikati yao.[#Ez. 2:5.]