The chat will start when you send the first message.
1Enyi Wagalatia, hamna akili? Ni uganga gani uliowashinda, msiyatii yaliyo ya kweli? Mmeonyeshwa Yesu Kristo, mmtazame kwa mambo yenu, alivyowambwa msalabani.
2Neno hili tu nataka kuambiwa nanyi: Mmempokea Roho kwa kuyafanya Maonyo au kwa kuyategemea, mliyoyasikia?
3Imekuwaje, akili zikiwapotea hivyo? Mliyoyaanza Rohoni, mwataka kuyamaliza sasa miilini?
4Yale yote mmeteswa bure? Kweli siyo ya bure![#Gal. 6:12.]
5Ilikuwaje? Aliyewapa Roho na kufanya yenye nguvu kwenu aliyafanyia kwamba: Mmeyafanya Maonyo? au kwamba: Mmeyategemea, mliyoyasikia?
6Ndivyo, yalivyokuwa nayo ya Aburahamu:
Akamtegemea Mungu,
kwa hiyo akawaziwa kuwa mwenye wongofu.
7Kwa hiyo yatambueni: wenye kumtegemea Mungu hao ndio wana wa Aburahamu!
8Lakini Maandiko yaliona kale, ya kuwa Mungu huwapatia wamizimu wongofu, wakiwa wanamtegemea. Kwa hiyo alimpigia Aburahamu kale mbiu ile njema:
Mwako ndimo, mataifa yote yatakamobarikiwa.
9Kwa hiyo wenye kumtegemea Mungu hubarikiwa pamoja na Aburahamu aliyekuwa mtegemevu.[#Rom. 4:16.]
10Kwani wote walio wenye kuyafanya Maonyo hawajatoka bado kwenye kuapizwa. Kwani imeandikwa:
Na awe ameapizwa kila mtu asiyeandamana nayo yote
yaliyoandikwa katika chuo cha Maonyo, ayafanye!
11Lakini neno hili ni waziwazi, ya kuwa hakuna mtu atakayepata wongofu kwake Mungu, kwa kuyafanya Maonyo, kwani:
Mwongofu atapata uzima kwa kumtegemea Mungu.
12Lakini Maonyo hayakutoka kwenye kumtegemea Mungu, ila:
Atakayeyafanya atapata uzima kwa njia hiyo.
13Kristo alitukomboa, tusiapizwe na Maonyo, alipoapizwa kwa ajili yetu, kwani imeandikwa:
Kila aliyetundikwa mtini ameapizwa.
14Hivyo mbaraka yake Aburahamu imewafikia wamizimu hapo, Yesu Kristo alipotokea, nasi tukipokee kiagio cha Roho tukiwa twamtegemea.
15Ndugu, niseme kimtu: Agano la mtu aliyekufa hakuna alitanguaye, likiisha kusimikwa, wala aliongezaye neno.
16Lakini Aburahamu alikuwa amepewa viagio vile yeye nao uzao wake. Hasemi: Wazao, kama ni wengi, ila kama ni mmoja, asema: Nao uzao wako, nao huo ndiye Kristo.[#1 Mose 22:18; 26:4; Tume. 3:25.]
17Kwa hiyo nasema: Agano limetangulia kusimikwa na Mungu, Maonyo yakatokea nyuma, miaka 430 ilipopita; hayawezi kulitangua agano, wala hayawezi kukikomesha nacho kiagio.[#2 Mose 12:40.]
18Kwani huo urithi kama ungalipatikana kwa kuyafanya Maonyo usingepatikana tena kwa kupewa kiagio. Lakini Mungu alimgawia Aburahamu huohuo alipompa kiagio.
19Basi, Maonyo yako na maana gani? Yalitolewa siku za kati kwa ajili ya mapitano, mpaka atakapokuja yule mzao aliye mwenye kiagio. Nayo Maonyo hapo, yalipotolewa, yalitumikiwa na malaika, yakawekwa mkononi mwa mpatanishaji.[#5 Mose 5:25-27; Tume. 7:38,53; Rom. 5:20.]
20Lakini mpatanishaji siye wa mmoja tu, lakini Mungu ni mmoja.
21Tena je? Maonyo huvikataa viagio vya Mungu? La, sivyo! Kwani kama yangekuwako Maonyo yaliyotolewa kuwa yenye nguvu ya kuwapa watu uzima, wongofu ungepatikana kweli kwa kuyafanya maonyo.[#Rom. 8:2-4.]
22Lakini Maandiko yamewafunga wote pamoja kuwa watumwa wa makosa kwamba: Wote watakaomtegemea wapewe kile kiagio kitokacho kwenye kumtegemea Yesu Kristo.[#Rom. 3:9-20; 11:32.]
23*Lakini tegemeo lilipokuwa halijatokea bado, tulilindwa, tuyatii Maonyo, tukawa tumefungwa pamoja, tungoje, tegemeo litakapofunuliwa.[#Gal. 4:3.]
24Hivyo ndivyo, Maonyo yalivyotuongoza kama watoto, yakatupeleka kwake Kristo, tupate wongofu kwa kumtegemea.
25Lakini tangu hapo, tegemeo lilipotokea, hatushikwi tena na mwongozi.[#Rom. 10:4.]
26Kwani ninyi nyote m wana wa Mungu kwa kumtegemea mkiwa wake Kristo Yesu.[#Yoh. 1:12; Rom. 8:17.]
27Maana ninyi nyote mliobatiziwa Kristo mmemvaa Kristo.[#Rom. 6:3; 13:14.]
28Kwake yeye hakuna tena Myuda na Mgriki, wala mtumwa na mwungwana, wala mume na mke, kwani ninyi nyote m mmoja kwa kuwa wake Kristo Yesu.[#Rom. 10:12; 1 Kor. 12:13.]
29Nanyi mkiwa wake Kristo, basi, mmekuwa hata uzao wake Aburahamu, tena m warithi kwa kiagio, mlichowekewa.*[#Gal. 3:7; Rom. 9:7.]