Waebureo 13

Waebureo 13

Mpendane!

1*Kaeni na kupendana kindugu![#Yoh. 13:34; 2 Petr. 1:7.]

2Msisahau kuwakaribisha wageni! Kwani hivyo wengine walikaribisha malaika, nao wenyewe hawakuwajua.[#1 Mose 18:3; 19:2-3; Rom. 12:13; 1 Petr. 4:9; 3 Yoh. 5-8.]

3Mwakumbuke waliofungwa, kama m wafungwa wenzao! Mwakumbuke wenye kufanyiziwa maovu! Maana ninyi wenyewe mmo miilini bado.[#Mat. 25:36.]

4Unyumba sharti uheshimiwe nao wote, hapo penye kitanda chao wanyumba pasifanywe chochote chenye uchafu. Kwani Mungu atawahukumu wagoni na wazinzi.[#Gal. 5:19,21; Ef. 5:5.]

5Msiwe wapenda fedha, mtoshewe nayo yaliyo yenu! Kwani yeye mwenyewe anasema:

Sitakuacha, wala sitakuepuka.

6Kwa hiyo sisi hujipa moyo wa kusema:

Bwana akiwa ananisaidia, sitaogopa;

maana aliye mtu atanifanyia nini?

Ng'ombe yetu ya tambiko na mji wetu ukaao.

7Mwakumbuke waliowaongoza ninyi, waliowaambia Neno la Mungu! Tazameni, walivyotoka ulimwenguni, mviige, walivyomtegemea Mungu![#Ebr. 13:17; 1 Kor. 4:16.]

8Yesu Kristo alivyokuwa jana na leo, ndivyo, atakavyokuwa kale na kale.[#1 Kor. 3:11; Ufu. 1:17; 22:13.]

9Msijipoteze na kujifunza mafundisho mengi yaliyo mageni! Kwani ni vizuri, moyo ukishupaa kwa kugawiwa nguvu, si kwa miiko ya vyakula; kwani waifuatao hawajipatii chochote.*[#Rom. 14:17; 2 Kor. 1:21; Ef. 4:14; Kol. 2:16-17.]

10Sisi tunapo petu pa kutolea vipaji vya tambiko, napo ni penye mwiko wa kuvila kwao watambikiao Hemani.[#Ebr. 8:4-5.]

11Kwani damu za nyama zikiisha kupelekwa Patakatifu na mtambikaji mkuu kwa ajili ya makosa, basi, miili yao hao nyama huteketezwa nje ya kambi.[#3 Mose 16:27.]

12Kwa hiyo hata Yesu aliteswa nje ya mlango wa mji, awatakase watu kwa damu yake mwenyewe[#Mat. 21:39; Yoh. 9:22; 19:17.]

13Kwa hiyo tumtokee tukitoka kambini na kuvumilia maumivu yenye soni yalinganayo nayo yake![#Ebr. 11:26; 12:2.]

14Kwani huku hatuna mji ukaao, ila tunaufuata ule ujao.[#Ebr. 11:10; 12:22.]

15Tukiwa naye yeye, tumtolee Mungu po pote vipaji vya tambiko vya kumsifu, ndiyo matunda ya midomo iliungamayo Jina lake![#Sh. 50:14,23; Hos. 14:3.]

16Msisahau kutenda mema na kugawiana na wenzenu yaliyo yenu! Kwani vipaji kama hivyo humpendeza Mungu.[#Fil. 4:18.]

17Wenye kuwaongoza watiini na kuwanyenyekea! Kwani hao huzikeshea roho zenu, maana ndio watakaoulizwa kwa ajili yao, nao hutaka kuzifanya kazi zao kwa furaha pasipo kupiga kite. Kwani hivi haviwafalii kitu ninyi.[#Ez. 3:17-19; 1 Tes. 5:12.]

Mchungaji wa kondoo aliye mkuu.

18Tuombeeni sisi! Kwani mioyo yetu hutushuhudia, tuyajuayo kwamba: Twataka kufanya mwenendo mzuri katika mambo yote.[#2 Kor. 1:12.]

19Lakini nakaza kuwahimiza, mfanye hivyo, nirudishwe kwenu upesi.

20Mungu mwenye utengemano aliyemtoa kwenye wafu Bwana wetu Yesu aliye mchungaji mkuu wa kondoo kwa nguvu ya damu ya Agano la kale na kale,[#Yoh. 10:12; 1 Petr. 2:25.]

21yeye Mungu awape nguvu ya kuyafanya mema yote, ayatakayo! Maana yeye ndiye anayetupa kuyafanya yapendezekayo mbele yake, akitushikisha njia yake Yesu Kristo. Huyu na atukuzwe kale na kale pasipo mwisho!

22Lakini nawahimiza, ndugu, yatieni mioyoni maneno haya ya kuwaonya! Kwani nimewaandikia na kukatakata.

23Jueni, ya kuwa ndugu yetu Timoteo amefunguliwa! Akija upesi, tutaonana nanyi pamoja na yeye.

24Nisalimieni wote wawaongozao na watakatifu wote! Nao wenzetu wa Italia wanawasalimu.

25Upole uwakalie ninyi nyote! Amin.

Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.
Published by: Bible Society of Tanzania