The chat will start when you send the first message.
1Kwa hiyo imetupasa kujikaza, tushikamane nayo, tuliyoyasikia, tusitengeke penye wokovu!
2Kwani neno lile lililosemwa na malaika lilikuwa na nguvu; kila aliyepitana nalo naye aliyekataa kulisikia akapata lipizi limpasalo.[#Tume. 7:53; Gal. 3:19.]
3Je? Sisi tutalikimbia tunapoubeza wokovu ulio mkuu kama huu? Kwani ulianza kutangazwa naye Bwana, kisha ukashupazwa kwetu nao waliousikia.[#Ebr. 10:29; 12:25.]
4Naye Mungu akaushuhudia na kufanya vielekezo na vioja na vyenye nguvu vingi na kuwagawia watu Roho takatifu kila mtu, kama alivyomtakia.[#Mar. 16:20; 1 Kor. 12:4,11; 2 Kor. 12:12.]
5Kwani malaika sio, aliowapa kuutawala ulimwengu utakaokuja, tunaousema.
6Lakini pako paliposemwa ushuhuda wa kwamba:
Mtu ndio nini, umkumbuke?
Mwana wa mtu naye, umkague?
7Ulimpunguza kidogo, asilingane na malaika,
ukamvika kilemba chenye utukufu na macheo,
8yote pia ukayaweka kuwa chini miguuni pake.
Basi, hapo, alipoviweka vyote chini yake, hakukisaza hata kimoja, asichokiweka chini yake. Lakini sasa hatujaona bado, ya kuwa vyote vimewekwa chini yake.
9Lakini kule kwamba: Alipunguzwa kidogo, asilingane na malaika, tunaona, ya kuwa kumetimia kwake Yesu. Kwa hivyo, alivyokufa matesoni, alivikwa kilemba chenye utukufu na macheo, maana aligawiwa na Mungu, awaonjee wote uchungu wa kufa.[#Ebr. 5:4; Fil. 2:8-9.]
10Kwani ni kwa ajili yake Mungu, vyote vikiwapo, naye ndiye aliyeviumba vyote; kwa hiyo ilimpasa, ile kazi ya kutimilika matesoni ampe yule aliyepeleka wana wengi kwenye utukufu alipowaokoa, apate kuwa kiongozi wao.[#Rom. 11:36.]
11Kwani mwenye kutakasa nao wenye kutakaswa, wote walitoka kwake yeye mmoja. Kwa sababu hii haoni soni ya kuwaita ndugu akisema:[#Mat. 12:49; 25:40; Mar. 3:34-35; Yoh. 20:17.]
12Nitawasimulia ndugu zangu mambo ya Jina lako,
nitakuimbia wewe katikati yao walio wateule.
13Tena anasema:
Mimi nitakuwa ninamwegemea yeye.
Tena anasema:
Tazama mimi niko pamoja na hawa watoto, Mungu alionipa.
14Kwa sababu wale watoto wanayo miili yenye damu na nyama, vivyo hivyo na yeye alijipa mwili ulio hivyo kama yao; kwani alitaka, kufa kwake kumtangue yule aliyekuwa mwenye nguvu za kufa, maana ndiye yule Msengenyaji.[#Ebr. 2:17; Yoh. 12:31; 2 Tim. 1:10; 1 Yoh. 3:8.]
15Hivyo alitaka kuwakomboa wote walioshikwa utumwani siku zote za maisha yao, wakiogopa kufa.
16Kwani aliovitunzia hivyo, sio malaika, ila ndio wao wa uzao wake Aburahamu, aliowatunzia.
17Kwa hiyo ilimpasa kufanana na ndugu zake katika mambo yote, apate kuwa mtambikaji mkuu aliye mwenye huruma na welekevu machoni pake Mungu, aweze kuwa kole ya kuyalipa makosa ya watu.[#Fil. 2:7.]
18Kwani kwa hivyo, alivyoteseka na kujaribiwa mwenyewe, anaweza kuwasaidia wanaojaribiwa.[#Ebr. 4:15.]