The chat will start when you send the first message.
1Kwa hiyo na tuyaache mafundisho ya kwanza ya Kristo, tuendelee kuwafundisha yaliyo ya kutimiza! Tusiweke tena msingi na kuwafundisha kwamba: Juteni mkiyaacha matendo yawauayo! Kisha mtegemeeni Mungu!
2Tuyaache nayo mafundisho ya ubatizo na ya kubandikiwa mikono na ya ufufuko wa wafu na ya hukumu ya kale na kale!
3Hayo tutayafuata, Mungu atakapotupa ruhusa.[#Ebr. 6:8; 10:26-29; Mat. 12:31; 2 Petr. 2:20-21; 1 Yoh. 5:16.]
4Kwani waliokwisha kuangazwa mioyo na kukionja kipaji kitokacho mbinguni na kugawiwa Roho takatifu
5na kulionja Neno la Mungu lililo zuri na kuzionja nguvu za siku zitakazokuja,
6basi, walio hivyo wakitengeka, haiwezekani tena kuwapatia upya, wapate kujuta. Kwani hao humwamba msalabani Mwana wa Mungu mara kwa mara pamoja na kumfyoza, huku ndiko kujiangamiza.
7Kwani nchi, ikiinywa mvua iinyeayo mara nyingi, huzaa maboga yanayowafalia wailimao, ikichipushwa na Mungu.
8Lakini ikizaa miiba na mibigili haifai tena, ikafikia kuapizwa, nayo mwisho huteketea.
9Lakini hata tukisema hivyo, wapendwa, kwa ajili yenu ninyi tumejipa moyo wa kwamba: Yale mema yatupayo wokovu mnayo.
10Kwani Mungu siye mpotovu, hatayasahau matendo ya upendo wenu, mliyoyatumia ya kulikuza Jina lake na kuwatumikia watakatifu toka kale hata sasa.[#Ebr. 10:32-34.]
11Lakini twataka sana, kila mmoja wenu ajikaze vivyo hivyo, apate kukishika kingojeo chetu chote kizima mpaka mwisho,[#Ebr. 3:14; Fil. 1:6.]
12msipate kuwa wavivu, ila mwaige wale walio wenye kuvirithi viagio kwa hivyo, walivyovitegemea na kuvumilia.
13Kwani Mungu alipomwekea Aburahamu kiagio aliapa na kujitaja mwenyewe kwa kukosa aliye mkubwa kumpita, amtaje akiapa.[#1 Mose 22:16-17.]
14Akasema: Nitakubariki kweli, nikupe kuwa watu wengi sana.
15Naye alipovumilia akaona, kiagio kilivyotimia.
16Kwani watu wakiapa hutaja aliye mkubwa kuliko wao, nacho kiapo hukomesha kwao mabishano yote na kulitia nguvu lile neno.[#2 Mose 22:11.]
17Naye Mungu alipotaka sana kuwaonyesha wenye kiagio kwamba: Ayatakayo yeye hayatanguki kamwe, akaapa, wapate kutulia.
18Akataka, hayo mambo mawili yasiyotanguka kamwe - maana haiwezekani, Mungu aseme uwongo - yatupe matulizo yenye nguvu sisi tuliomkimbilia, tupate kukishika kingojeo chetu, tulichowekewa.
19Hicho tunakishika, kiwe nanga ya moyo isiyokosa nguvu za kutuliza; nacho ndicho kituingizacho namo mle ndani, tulimopingiwa na lile pazia.[#3 Mose 16:2,12.]
20Humo ndimo, Yesu alimoingia, atufungulie njia, akawa mtambikaji mkuu wa kale na kale, kama Melkisedeki alivyokuwa.[#Ebr. 5:6.]