The chat will start when you send the first message.
1*Nakushukuru, Bwana, ya kuwa ulinichafukia,
kwani machafuko yako yamegeuka, ukanituliza moyo.
2Mtazamieni Mungu aniokoaye!
Pasipo woga wo wote ninamngojea,
kwani Bwana ni nguvu yangu na shangilio langu,
yeye Bwana ndiye aniokoaye.
3Kwa furaha mtachota maji visimani kwenye wokovu.[#Sh. 46:5; Zak. 13:1.]
Mshukuruni Bwana, nalo Jina lake litambikieni!
Yajulisheni makabila ya watu matendo yake!
Wakumbusheni kwamba: Jina lake ni boma!
5Mshangilieni Bwana! Kwani hufanya makuu.
Hayo sharti yajulikane katika nchi zote!
6Pigeni shangwe na vigelegele, ninyi mkaao Sioni!
Kwani aliye mkuu kwenu katikati ndiye Mtakatifu wa Isiraeli.*