The chat will start when you send the first message.
1Baada ya Abimeleki akaondokea Tola, mwana wa Pua, mwana wa Dodo wa Isakari, awaokoe Waisiraeli. Naye alikuwa anakaa Samiri milimani kwa Efuraimu.
2Akawa mwamuzi wa Waisiraeli miaka 23, kisha akafa, akazikwa Samiri.
3Baada yake huyu akaondokea Yairi wa Gileadi, akawa mwamuzi wa Waisiraeli miaka 22.[#4 Mose 32:41.]
4Akawa mwenye wana 30 waliopanda wana wa punda 30, nao walikuwa wenye miji 30, nayo huitwa hata siku hii ya leo Mahema ya Yairi, nayo iko katika nchi ya Gileadi.[#Amu. 12:14.]
5Yairi alipokufa akazikwa huko Kamoni.
6Wana wa Isiraeli walipoendelea kuyafanya yaliyo mabaya machoni pake Bwana, wakiyatumikia Mabaali na Maastaroti na miungu ya Ushami na miungu ya Sidoni na miungu ya Moabu na miungu ya wana wa Amoni na miungu ya Wafilisti, basi, walipomwacha Bwana hivyo, wasimtumikie,
7makali ya Bwana yakawawakia Waisiraeli, akawauza na kuwatia mikononi mwa Wafilisti namo mikononi mwa wana wa Amoni.
8Wakawasumbua wana wa Isiraeli na kuwakorofisha; mwaka huo ikawa miaka 18, wakiwaumiza wana wa Isiraeli wote waliokaa ng'ambo ya huko ya Yordani kule Gileadi katika nchi ya Waamori.
9Wana wa Amoni walipovuka Yordani kupiga vita hata katika nchi ya Yuda na ya Benyamini nako kwao wa mlango wa Efuraimu, Waisiraeli wakasongeka sana.
10Ndipo, wana wa Isiraeli walipomlilia Bwana kwamba: Tumekukosea, tulipomwacha Mungu wetu na kuyatumikia Mabaali.
11Naye Bwana akawaambia wana wa Isiraeli: Sikuwatoa kwao Wamisri na Waamori na wana wa Amoni na Wafilisti?
12Napo, Wasidoni na Waamaleki na Wamaoni walipowatesa ninyi, nanyi mliponililia, nikawaokoa mikononi mwao.
13Lakini ninyi mmeniacha, mkatumikia miungu mingine; kwa hiyo sitawaokoa tena.
14Haya! Nendeni kuililia miungu, mliyoichagua, hiyo na iwaokoe siku za masongano yenu![#5 Mose 32:37-38; Yer. 2:28.]
15Lakini wana wa Isiraeli wakamwambia Bwana: Tumekosa! Tufanyizie yote yaliyo mema machoni pako! Lakini tuponye siku hii ya leo tu!
16Kisha wakaiondoa hiyo miungu migeni katikati yao, wakamtumikia Bwana; ndipo, roho yake ilipoona uchungu kwa ajili ya masumbuko yao Waisiraeli.[#1 Mose 35:2-4; Amu. 2:18.]
17Kisha wana wa Amoni wakaitwa kukusanyika, wakapiga makambi huko Gileadi; wana wa Isiraeli nao wakapiga makambi Misipa.
18Ndipo, watu na wakuu wa Gileadi waliposemeana kila mtu na mwenzake: Ni nani atakayeanza kupigana nao wana wa Amoni? Yeye atakuwa mkuu wao wote wakaao Gileadi.[#Amu. 11:6-11.]