Yeremia 45

Yeremia 45

Yeremia anautuliza moyo wa Baruku.

1Hili ndilo neno, mfumbuaji Yeremia alilomwambia Baruku, mwana wa Neria, alipoyaandika maneno haya katika kitabu, Yeremia akiyasema kwa kinywa chake, katika mwaka wa nne wa Yoyakimu, mwana wa Yosia, mfalme wa Yuda, akimwambia:[#Yer. 36:4.]

2Hivi ndivyo, Bwana Mungu wa Isiraeli anavyokuambia Baruku:

3Unasema: Yamenipata, kwani Bwana anayaongeza maumivu yangu na kunitia majonzi! Nimechoka kwa kupiga kite, sioni pa kutulia.

4Utamwambia hivyo: Hivi ndivyo, Bwana anavyosema: Unaniona mimi, ninavyoyabomoa, niliyoyajenga, ninavyoyang'oa, niliyoyapanda! Vinakuwa hivyo katika nchi yote nzima.

5Inakuwaje, wewe ukijitakia mambo makuu? Usijitakie hayo! Unaniona, ninavyowaletea mabaya wote wenye miili ya nyama, ndivyo, asemavyo Bwana; lakini wewe nitakupa roho yako kuwa pato lako mahali po pote, utakapokwenda.[#Yer. 39:18; 43:6.]

Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.
Published by: Bible Society of Tanzania