Yohana 16

Yohana 16

1Haya nimewaambia, maana msije kukwazwa.[#Yoh. 14:29.]

2Watawakataza kuziingia nyumba za kuombea; kweli saa inakuja, kila mwenye kuwaua ninyi atakapodhani, ya kuwa anamtumikia Mungu.[#Mat. 24:9.]

3Hivyo watavifanya, kwa sababu hawakumtambua Baba wala mimi.[#Yoh. 15:21.]

4Lakini nimewaambia haya, kwamba saa yao itakapokuja, myakumbuke, ya kuwa mimi nimewaambia ninyi. Lakini tangu mwanzo sikuwaambia haya kwa hivyo, nilivyokuwa pamoja nanyi.*

Kazi ya mtuliza mioyo.

5*Lakini sasa nakwenda kwake yeye aliyenituma, tena kwenu hakuna anayeniuliza: Unakwenda wapi?[#Yoh. 7:33.]

6Ila kwa sababu nimewaambia haya, mioyo yenu imejaa masikitiko.

7Lakini mimi nawaambiani lililo la kweli: Inawafalia, mimi niende zangu. Kwani nisipokwenda zangu, mtuliza mioyo hatawajia. Lakini nitakapokwenda, nitamtuma kwenu.[#Yoh. 14:16,26.]

8Naye atakapokuja atawaumbua wao wa ulimwengu kuwa wenye makosa wasio nalo la kujikania, wanaopaswa na kuhukumiwa.[#1 Kor. 14:24.]

9Ndio wenye makosa, kwa kuwa hawanitegemei mimi;[#Yoh. 3:18; 15:22,24.]

10hawana la kujikania, kwa kuwa nakwenda kwa Baba, nanyi hamnioni tena;[#Tume. 5:31; Rom. 4:25; 1 Petr. 3:18.]

11wapaswa na kuhukumiwa, kwa kuwa mtawala ulimwengu huu amekwisha kuhukumiwa.[#Yoh. 12:31; 14:30.]

12Yako maneno mengi bado, ninayotaka kuwaambia; lakini sasa mngeyaona kuwa mzigo usiochukulika.[#1 Kor. 3:1.]

13Lakini yule atakapokuja, yule Roho wa kweli, yeye atawaongoza, awapeleke penye yote yaliyo ya kweli. Kwani hatayasema maneno yake mwenyewe, ila atayasema, atakayoyasikia, awatangazie nayo yatakayokuja.[#Yoh. 14:26; 1 Yoh. 2:27.]

14Yeye ndiye atakayenitukuza, kwani katika yale yaliyo yangu ndimo, atakamoyatwaa, atakayowatangazia ninyi.

15Yote, Baba aliyo nayo, ni yangu; kwa hiyo nilisema: Katika yale yaliyo yangu ndimo, atakamoyatwaa, atakayowatangazia ninyi.*[#Yoh. 17:10.]

Bado kidogo.

16*Bado kidogo hamtaniona; tena patakapopita kitambo kidogo, mtaniona tena, kwa sababu ninakwenda kwa Baba.[#Yoh. 14:19.]

17Basi, kulikuwako wanafunzi wake waliosemezana wao kwa wao: Neno hili, analotuambia, ni neno gani la kwamba: Bado kidogo hamtaniona, tena patakapopita kidogo, mtaniona? Na tena: Ninakwenda kwa Baba?

18Wakasema: Lile bado kidogo, alisemalo, ni kusemaje? Hatujui, analosema.

19Kwa kuwatambua, ya kuwa walitaka kumwuliza, Yesu akawaambia: Mnaulizana kwa hilo, nililolisema: Bado kidogo hamtaniona; tena patakapopita kidogo, mtaniona?

20Kweli kweli nawaambiani: Ninyi mtalia na kuomboleza, lakini wao wa ulimwengu watafurahi. Ninyi mtasikitika, lakini sikitiko lenu litageuka kuwa furaha.

21Mwanamke anapozaa husikitika, kwani saa yake imekuja; lakini akiisha kumzaa mwana hayakumbuki tena maumivu, ila hufurahi kwa ajili ya mtu aliyezaliwa kukaa ulimwenguni.[#Yes. 26:17.]

22Basi, nanyi sasa mnasikitika, lakini tutaonana tena, ndipo, mioyo yenu itakapofurahi; hiyo furaha yenu hakuna atakayeiondoa kwenu.

23Siku ile hamtaniuliza neno.*

*Kweli kweli nawaambiani: Lo lote, mtakalomwomba Baba, atawapa katika Jina langu.

24Mpaka leo hakuna, mliloliomba katika Jina langu. Ombeni! Ndipo, mtakapopewa, furaha yenu iwe imetimizwa yote![#Yoh. 15:11.]

25Haya nimewaambia kwa mifano. Lakini saa inakuja, itakapokuwa, nisiseme nanyi tena kwa mifano, ila nitawatolea waziwazi mambo ya Baba.

26Siku ile mtaomba katika Jina langu, nani siwaambii: Mimi nitawaombea ninyi kwake Baba.

27Kwani Baba mwenyewe anawapenda, kwa sababu ninyi mmenipenda mimi na kunitegemea kwamba: Mimi nimetoka kwa Baba.[#Yoh. 14:21.]

28Nimetoka kwa Baba, nikaingia ulimwenguni; tena nauacha ulimwengu, niende kwa Baba.

29Ndipo, wanafunzi wake waliposema: Tazama, sasa unasema waziwazi, usiseme mfano wo wote.[#Yoh. 16:25.]

30Sasa tunajua, ya kuwa unayajua yote, ya kuwa huulizwi na mtu. Kwa hiyo tunakutegemea, ya kuwa umetoka kwa Mungu.

31Yesu akawajibu: Sasa mnanitegemea?

32Tazameni, saa inakuja, tena imekwisha fika, mtawanyike kila mtu na kwao kwenyewe, mniache mimi, niwe peke yangu. Lakini mimi sipo peke yangu, kwani Baba yupo pamoja nami.[#Yoh. 8:29; Mat. 26:31; Mar. 14:27; Zak. 13:7.]

33Haya nimewaambia, mpate kutengemana mwangu. Ulimwenguni mnayo maumivu; lakini tulieni mioyo! Mimi nimeushinda ulimwengu.*[#Yoh. 14:27; Rom. 5:1; 1 Yoh. 5:4.]

Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.
Published by: Bible Society of Tanzania