Iyobu 14

Iyobu 14

Watu hutoweka upesi.

1*Mtu aliyezaliwa na mwanamke huwapo siku chache, nayo anayoyashiba ni mahangaiko tu.

2Huchanua kama ua, kisha hupukutika, hupita upesi kama kivuli, hakai.[#Sh. 90:5.]

3Ingawa awe hivyo, unayafumbua macho, kusudi yamlinde; lakini mimi unanipeleka shaurini, tusemeane huko.

4Miongoni mwao waliotoka kwa mwenye uchafu yuko atakataye? Hata mmoja tu hayuko.[#Sh. 14:3.]

5Mtu amekwisha kukatiwa siku zake, miezi yake imekwisha kuhesabiwa na wewe mwenyewe, umeiweka mipaka yake, asiipite.*[#Sh. 31:16; 39:5.]

6Ikiwa hivyo, acha kumtazama, apate kupumzika, aifurahie hiyo siku yake kama mkibarua![#Iy. 7:1-2.]

7Kwani kiko kingojeo kinachoupasa huo mti nao: kama unakatwa, huchipuka tena, nayo hayo machipukizi yake hayakomi.

8Mizizi yake ikioza nchini ndani, nalo shina lake likifa mchangani,

9kwa unyevu wa maji tu utachipuka tena, upate matawi sawasawa kama mche mpya.

10Lakini mtu akifa hutoweka, mwana wa Adamu akiisha kuzimia huenda wapi?

11Maji ya bahari hupwa, nayo ya mtoni hupotea kabisa, pawe pakavu.

12Vivyo hivyo naye mtu akija kulala hainuki tena; mpaka mbingu zitakapotoweka, hawaamki, wala hawataamshwa usingizini mwao.[#Iy. 7:10; 19:25.]

13Laiti ungenificha kuzimuni, ukanilindia huko, mpaka yatulie makiali yako! Muda ulionikatia utakapokwisha pita, ungenikumbuka hapo![#Sh. 27:5; 31:21; Yes. 26:20.]

14Mtu atarudi uzimani tena akiisha kufa? Kama ndivyo, ningengoja siku zangu zote za kushindana na mateso, mpaka nitakapopokelewa na mwenzangu mwingine.[#Iy. 7:1.]

15Hapo ningekuitikia, utakaponiita kwa kukitunukia kiumbe cha mikono yako.

16Sasa ukizihesabu nyayo zangu po pote, zilipokanyaga, makosa yangu nayo huyaangalii?

17Hapo maovu yangu yangefungiwa mfukoni na kutiwa muhuri, nazo manza zangu, nilizozikora, ungezifuta.[#Hos. 13:12.]

18Lakini sivyo; mlima ukianguka hutoweka, nao mwamba huondoka mahali pake, ulipokuwapo.

19Maji husaga mawe, yawe madogo, nayo mafuriko ya maji huuchukua mchanga wa nchi, hivyo nacho kingojeo cha mtu unakiangamiza.[#Rom. 5:5.]

20Unamshinda siku zote pia, ajiendee, unaugeuza uso wake ukimtuma kujiendea.

21Wanawe kama wanapata macheo, havijui; au kama wananyenyekezwa, hayatambui mambo yao.

22Huyasikia tu maumivu ya mwili wake yeye, nayo roho yake husikitika kwa ajili yake yeye.

Elifazi anasema mara ya pili: Wasiomcha Mungu hupatwa na mabaya.

Elifazi wa Temani akajibu akisema:

Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.
Published by: Bible Society of Tanzania