Iyobu 25

Iyobu 25

1Utawalaji na utisho uko kwake

2anayepatengemanisha pake palipo huko juu.

3Je? Vikosi vyake vinahesabika? Yuko nani asiyetokewa na mwanga wake?

4Kwa hiyo mtu atawezaje kuwa mwongofu machoni pake Mungu? Aliyezaliwa na mwanamke atawezaje kutakata?[#Iy. 9:2.]

5Ukiutazama mwezi utauona: hauangazi kabisa, wala nyota hazitakati machoni pake.[#Iy. 15:15.]

6Sembuse mtu aliye dudu! Sembuse mwana wa Adamu aliye funyo![#Iy. 4:19-20.]

Jibu la nane la Iyobu: Utukufu wa Mungu hauchunguziki.

Iyobu akajibu akisema:

Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.
Published by: Bible Society of Tanzania