The chat will start when you send the first message.
1Kisha Iyobu akakifumbua kinywa chake, akaiapiza siku yake;
2yeye Iyobu akaanza kusema kwamba:[#Yer. 20:14-18.]
3Siku niliyozaliwa ingalifaa, kama ingaliangamia, pamoja na usiku ule, waliposema: Mimba hii ni mtoto wa kiume.
4Siku hiyo ingalifaa, kama ingalikuwa yenye giza, kama Mungu wa huko juu asingaliitafuta, kama mchana nao usingaliiangaza.
5Giza lenye kivuli kiuacho na liitake kuwa lake, mawingu yenye weusi na yaikalie na kuifunika, yageuzayo mchana kuwa giza na yaipatie vituko.
6Kama giza tupu lingaliupokonya, usiku ule nao ungalifaa, kama usingalihesabiwa katika siku za mwaka huo, wala kama usingaliingia katika hesabu ya miezi!
7Ningeuona kuwa mwema, kama usingalizaa kitu, wala kama usingalisikia sauti ya shangwe.
8Wajuao kuziloga siku sharti wauapize, ndio wao waliojipa mioyo kumchochea naye nondo wa baharini.
9Nyota zake za mapambazuko na ziguiwe na giza, usione mwanga ukiungojea, wala vishale vya mapambazuko usivione,
10kwa kuwa haukufunga mlango wa tumbo la mama yangu na kuyaficha masumbuko, macho yangu yasiyaone!
11Mbona sikuweza kufa nilipotoka tumboni mwa mama? Mbona sikuzimia nilipotoka tumboni mwake?
12Mbona nilipokelewa na kuwekwa magotini? Mbona nikapata maziwa ya kuyanyonya?
13Kama sivyo, ningelala sasa na kutulia, ningelala usingizi na kujipatia mapumziko;
14ningekuwa pamoja na wafalme na wenye hukumu wa nchi waliojijengea machuguu makubwa ya kuzikiwa humo;
15au ningekuwa pamoja na wakuu waliokuwa wenye dhahabu, waliozijaza nyumba zao na kulimbika fedha;
16au ningalikwisha kuchimbiwa tu kama mimba iliyoharibika, nisipate kuwapo kama wachanga wasiouona mwanga.
17Huko ndiko, wanakokomea kuchafuka wasiomcha Mungu; ndiko, wanakopumzikia waliojichokesha kwa kuzitumia nguvu zao.
18Huko wafungwa wote pamoja hutengemana, hawasikii tena sauti ya msimamizi.
19Huko wadogo na wakubwa ni wamoja, nao watumwa wamekwisha kombolewa, wasiwe mali za mabwana zao.
20Sababu gani anampa msumbufu kuona mwanga? Sababu gani anampa kuwapo mwenye uchungu rohoni?
21Ndio wanaokingojea kifo, lakini hawakipati; kuliko vilimbiko vilivyofichwa hutaka kukizua.[#Ufu. 9:6.]
22Hao wangefurahi na kushangilia, wangechangamka kweli, kama wangeona kaburi.
23Hao ni watu waliofichwa maana ya njia zao, wao ndio, Mungu aliowazibia mizungu yote pia.[#Iy. 19:8.]
24Sharti kwanza nipige kite, ninapotaka kula, navyo vilio vyangu humwagika kama maji.
25Kwani ninapostukia kistusho, hichohicho hunipata, nacho nilichokiogopa hunijia.
26Sipati kutengemana wala kutulia wala kupumzika, kwani mahangaiko hunijia.
Elifazi wa Temani akamjibu akisema: