Iyobu 5

Iyobu 5

Asiyemcha Mungu huangamia, amchaye hupona.

1Haya! Ita, kama yuko mtu anayekuitikia! Kwao walio watakatifu utamtokea nani?

2Kwani majonzi humwua mjinga, nao wivu humwua mpuzi.

3Mimi niliona mjinga, akishusha mizizi, lakini mara sikuwa na budi kuliapiza hilo kao lake.[#Sh. 37:35-36.]

4Watoto wake hawakupata wokovu, uliwakalia mbali, Walipowaponda langoni, hakuwako mponya.

5Mavuno yake yakaliwa na mwingine aliyekuwa na njaa, akayachukua na kuyatoa penye vitalu, ingawa ni vyenye miiba, nao wenye kiu huzitwetea mali zao.

6Kwani upotovu hautoki uvumbini, wala usumbufu hauchipuki hapa nchini,

7ila mtu huzaliwa, apate kusumbuka, awe kama cheche za moto zinazoruka juu.

8Lakini aliye Mungu mimi ningemtafuta, naye Mungu ningemwambia shauri langu.

9Hufanya mambo makuu yasiyochunguzika, vioja vyake havihesabiki:[#Iy. 9:10.]

10hutoa mvua kuinyesha nchi, ayapatie mashamba maji ya juu.

11Walio wanyenyekevu huwakweza, huwapandisha kuufikia wokovu wao wasikitikao.[#Sh. 75:8; Luk. 1:52.]

12Huyatangua mawazo yao walio werevu, mikono yao isiweze kufanya kifaacho.

13Nao wenye ubingwa huwakamata kwa werevu wao, mashauri yao wapotovu yaangamie upesi.[#1 Kor. 3:19.]

14Nao mchana wao huguiwa na giza, wapapasepapase mnamo saa sita, kama ni usiku.[#Yes. 59:9-10.]

15Ndivyo, anavyowaokoa wamaskini, ukali wa upanga usiwaue, wala mikono ya wenye nguvu isiwashinde.

16Hivyo ndivyo, kingojeo kinavyomtokea naye mnyonge, lakini uovu hufumbwa kinywa chake.

17*Tazama! Mwenye shangwe ni mtu, Mungu anayemchapa! Kwa hiyo usikatae kuonywa na Mwenyezi![#Sh. 94:12; Fano. 3:11.]

18Kweli yeye huumiza, lakini tena huuguza; atakapotia kidonda, mikono yake hukiponya.[#5 Mose 32:39; Hos. 6:1.]

19Atakuokoa katika masongano sita, yawe hata saba, kisioneke kibaya kitakachokugusa.[#Fano. 24:16.]

20Penye njaa atakukomboa namo kufani, hata vitani atakukomboa mikononi mwao wenye panga.

21Penye mapigo ya ndimi za watu utafichika, usiogope hapo napo, mwangamizo utakapokuja;

22utaucheka mwangamizo, hata njaa, nao nyama wakali wa nchi hutawaogopa.

23Kwani nayo mawe ya mashambani utapatana nayo, nao nyama wa porini watatengemana huko, uliko.[#Yes. 11:6-9; Hos. 2:18.]

24Ndipo, utakapolijua hema lako kuwa lenye utengemano, napo utakapolitazama kao lako, hutaona kitakachokoseka.

25Tena utayaona mazao yako kuwa mengi, navyo vizazi vya kwako vitakuwa vingi kama majani ya nchi.

26Nguvu zako zitakuwa hazikupunguka, utakapoingia kaburini, kama viganda vinavyoingizwa, mavuno yanapotimia.*

27Tazama! Haya tumeyachunguza kuwa hivyo kweli; yasikie, nawe upate kuyajua moyoni mwako!

Iyobu anajikania.

Iyobu akajibu akisema:

Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.
Published by: Bible Society of Tanzania