The chat will start when you send the first message.
1Bwana akamwambia Mose kwamba:
2Mchukue Haroni pamoja na wanawe na yale mavazi na mafuta ya kupaka na dume la ng'ombe atakayekuwa ng'ombe ya tambiko ya weuo na madume mawili ya kondoo na kikapu cha mikate isiyochachwa.
3Kisha ukusanye mkutano wote hapo pa kuliingilia Hema la Mkutano.
4Mose akafanya, kama Bwana alivyomwagiza, nao mkutano ukakusanyika hapo pa kuliingilia Hema la Mkutano.
5Mose akauambia mkutano: Hili ndilo, Bwana aliloliagiza kulifanya.
6Kisha Mose akamkaribisha Haroni nao wanawe, akawaosha kwa maji.
7Kisha akamvika shati, akaifunga kwa mkanda, akamvika kanzu, tena akamvika kisibau, akakifunga kwa masombo ya hicho kisibau na kukaza.
8Kisha akabandika hapo kibati, nacho hicho kibati akatia Urimu na Tumimu (Mwanga na Kweli).[#2 Mose 28:30.]
9Kisha akamvika kilemba kichwani, nao upande wa mbele wa kilemba akabandika bamba la dhahabu, ndio ile taji takatifu, kama Bwana alivyomwagiza Mose.[#2 Mose 28:36; 39:30.]
10Kisha Mose akayatwaa yale mafuta ya kupaka, akalipaka lile Kao navyo vyote vilivyomo; ndivyo, alivyovieua.[#2 Mose 30:25-26.]
11Nayo meza ya kutambikia akainyunyizia mafuta mara saba, akaipaka mafuta hiyo meza ya kutambikia na vyombo vyake vyote, hata birika na wekeo lake, avieue.
12Kisha akammiminia Haroni kichwani mafuta hayo ya kupakwa, akamweua kwa kumpaka mafuta hivyo.
13Kisha Mose akawakaribisha wana wa Haroni, akawavika shati, akazifunga kwa mikanda, akawavika vilemba virefu, kama Bwana alivyomwagiza Mose.
14Kisha akaagiza kumleta yule dume la ng'ombe ya tambiko ya weuo, naye Haroni na wanawe wakaibandika mikono yao kichwani pake yule dume la ng'ombe ya tambiko ya weuo.[#3 Mose 4.]
15Kisha wakamchinja, naye Mose akatwaa damu, akaitia kwa kidole chake katika pembe za meza ya kutambikia pande zote, akaieua hiyo meza ya kutambikia, nayo damu nyingine akaimwagia misingi ya meza ya kutambikia, akaieua nayo, ajipatie upozi.
16Akayachukua mafuta yote yaliyoshikamana na utumbo na kile kipande cha ini na mafigo yote mawili pamoja na mafuta yao, kisha Mose akayachoma moto mezani pa kutambikia.
17Lakini yule dume la ng'ombe mwenyewe pamoja na ngozi yake na nyama zake na mavi yake akamteketeza kwa moto nje ya makambi, kama Bwana alivyomwagiza Mose.
18Kisha akamtoa dume la kondoo aliye ng'ombe ya tambiko ya kuteketezwa nzima, naye Haroni na wanawe wakaibandika mikono yao kichwani pake huyu dume la kondoo.[#3 Mose 1:10-13.]
19Kisha Mose akamchinja, nayo damu akainyunyiza pande zote juu ya meza ya kutambikia.
20Kisha huyu dume la kondoo akachanguliwa vipande, naye Mose akamchoma moto, kichwa na vile vipande na mafuta;
21nao utumbo na miguu akaiosha kwa maji. Hivyo Mose akamchoma moto yule dume la kondoo wote mzima mezani pa kutambikia, awe ng'ombe ya tambiko ya kuteketezwa nzima. Ndivyo, alivyokuwa mnuko wa kupendeza, maana ni ng'ombe ya tambiko ya Bwana ya kuteketezwa kwa moto, kama Bwana alivyomwagiza Mose.
22Kisha akaagiza kuleta dume la kondoo wa pili aliye ng'ombe ya tambiko ya kujaza gao; naye Haroni na wanawe wakaibandika mikono yao kichwani pake huyo dume la kondoo.[#3 Mose 7:37.]
23Kisha Mose akamchinja, akatwaa damu kidogo, akampaka Haroni pembe ya chini ya sikio lake la kuume na kidole gumba cha mkono wake wa kuume nacho cha mguu wake wa kuume.
24Kisha Mose akawakaribisha wanawe Haroni; nao akawapaka damu pembe za chini za masikio ya kuume na vidole gumba vya mikono yao ya kuume navyo vya miguu yao ya kuume, nayo damu nyingine Mose akainyunyizia misingi ya meza ya kutambikia pande zote.
25Kisha akayatwaa mafuta, ni mkia na mafuta yote yanayoshikamana na utumbo na kipande kile cha ini na mafigo yote mawili pamoja na mafuta yao na paja la kuume,
26tena katika kikapu cha mikate isiyochachwa kilichokuwa mbele ya Bwana akatwaa mkate mmoja usiochachwa na mkate mmoja wenye mafuta na andazi jembamba moja, akayaweka juu ya mafuta na juu ya paja la kuume.
27Kisha akayaweka yote pia mikononi mwa Haroni namo mikononi mwa wanawe, akayapitisha motoni mbele ya Bwana, yawe vipaji vya tambiko vya kupitishwa motoni.
28Kisha Mose akayatwaa tena mikononi mwao, akayachoma moto mezani pa kutambikia juu ya ng'ombe ya tambiko ya kuteketezwa nzima. Hivyo ndivyo, ng'ombe za tambiko za kujaza gao zinavyotolewa, zipate kuwa mioto ya Bwana yenye mnuko wa kumpendeza.
29Kish Mose akakitwaa kidari cha yule dume la kondoo, akakipitisha motoni, kiwe kipaji cha tambiko cha kupitishwa motoni mbele ya Bwana; ndicho kipande cha ng'ombe ya tambiko ya kujaza gao kilichompasa Mose kuwa funga lake, kama Bwana alivyomwagiza Mose.
30Kisha Mose akatwaa mafuta kidogo ya kupaka na damu kidogo iliyokuwa mezani pa kutambikia, akamnyunyizia Haroni na mavazi yake nao wanawe na mavazi ya wanawe; ndivyo, alivyomweua Haroni na mavazi yake nao wanawe na mavazi yao pamoja naye.
31Kisha Mose akamwambia Haroni na wanawe: Zipikeni hizi nyama hapo pa kuliingilia Hema la Mkutano! Tena hapo ndipo, mtakapozila pamoja na mikate iliyomo katika kikapu cha vilaji vya tambiko vya kujaza gao, kama nilivyoagizwa kwamba: Haroni na wanawe na waile!
32Masao ya nyama na ya mikate mtayateketeza kwa moto.
33Tena hapo pa kuliingilia Hema la Mkutano msipatoke siku saba, mpaka siku zenu zilizowekwa za kutoa ng'ombe za tambiko za kujaza gao zitakapotimia, kwani siku za kujaza gao ni saba.
34Kama ilivyofanyika siku hii ya leo, ndivyo, Bwana alivyoagiza kufanya, mpatiwe upozi.
35Napo hapo pa kuliingilia Hema la Mkutano mtakaa siku saba mchana kutwa na usiku kucha, mwulinde ulinzi wa Bwana, msife, kwani hivyo ndivyo, nilivyoagizwa.
36Naye Haroni na wanawe wakayafanya haya maneno yote, Bwana aliyoyaagiza kinywani mwa Mose.