Mateo 24

Mateo 24

Mambo yatakayokuja.

(1-51: Mar. 13:1-37; Luk. 21:5-36.)

1Yesu alipotika Patakatifu akaenda zake. Wakamjia wanafunzi wake, wakamwonyesha majengo ya hapo Patakatifu;

2ndipo, alipojibu akiwaambia: Je? Mwayatazama haya yote? Kweli nawaambiani: Hapa halitaachwa hata jiwe moja juu ya jiwe lenziwe lisiloporomoshwa chini.[#Luk. 19:44.]

3Kisha alipokaa mlimani pa michekele, wanafunzi wakamjia; walipokuwa peke yao wakasema: Tuambie, hayo yatakuwapo lini? Tena kielekezo cha kurudi kwako na cha mwisho wa dunia ni nini?

4Yesu akajibu akiwaambia: Angalieni, mtu asiwapoteze!

5Kwani wengi watakuja kwa jina langu na kusema: Mimi ni Kristo; nao watapoteza wengi.[#Mat. 24:24; Tume. 5:36-37; 1 Yoh. 2:18.]

6Tena mtasikia vita na mavumi ya vita; vitazameni tu, msivihangaikie! Kwani hivyo sharti viwepo, lakini huo sio mwisho.

7Kwani watainukiana taifa na taifa, tena wafalme na wenzao wafalme; mahali penginepengine patakuwa na kipundupindu, pengine na njaa, pengine na matetemeko.[#2 Mambo 15:6; Yes. 19:2.]

8Lakini hayo yote ni mwanzo tu wa uchungu.

9Hapo watatoa ninyi, mpate kuumizwa, hata kuuawa, tena mtachukiwa na makabila yote kwa ajili ya Jina langu.[#Mat. 10:17,22; Yoh. 15:18; 16:2.]

10Hapo ndipo, wengi watakapokwazwa, watoane wenyewe kila mtu na mwenziwe kwa kuchukiana wao kwa wao.[#Dan. 11:41.]

11Hata wafumbuaji wa uwongo wengi watainuka na kupoteza wengi.[#Mat. 7:15; 2 Petr. 2:1; 1 Yoh. 4:1.]

12kwa sababu upotovu utazidi kuwa mwingi, upendo wa wengi utapoa.[#2 Tes. 2:10; 2 Tim. 3:1-5.]

13Lakini atakayevumilia mpaka mwisho ndiye atakayeokoka.[#Mat. 10:22; Ufu. 2:10; 13:10.]

14Nao huu utume mwema wa ufalme wa Mungu utatangawa ulimwenguni mote, uje, unishuhudie kwa wamizimu wote. Kisha ndipo, mwisho utakapokuja.[#Mat. 10:18; 28:19.]

15*Hapo ndipo, mtakapochafukwa mioyo mkiona, mwangamizaji atapishaye akisimama mahali Patakatifu, kama mfumbuaji Danieli alivyosema; mwenye kupasoma hapa sharti aangalie, ajue maana![#Dan. 9:26-27; 12:11.]

16Siku zile watakaokuwako Yudea na wakimbilie milimani!

17Mtu atakayekuwapo nyumbani juu asishuke kuvichukua vilivyomo nyumbani mwake![#Luk. 17:31.]

18Naye atakayekuwako shambani asirudi nyuma kuichukua nguo yake!

19Lakini watakaoona vibaya zaidi ndio wenye mimba na wenye kunyonyesha siku zile.

20Lakini ombeni, kukimbia kwenu kusitimie siku za kipupwe wala siku ya mapumziko![#Tume. 1:12.]

21Kwani hapo patakuwa na maumivu makuu kuyapita yote yaliyopatikana tangu mwanzo wa ulimwengu mpaka sasa, hata halafu hayatapatikana tena kama hayo.[#Dan. 12:1; Yoe. 2:2.]

22Nazo siku zile kama hazingalipuinguzwa, hangaliokoka mtu hata mmoja. Lakini kwa ajili ya wale waliochaguliwa siku zile zitapunguzwa.

23Hapo mtu akiwaambia: Tazama, huyu hapa ni Kristo! au akisema: Yule kule! msiitikie!

24Kwani watainuka makristo wa uwongo na wafumbuaji wa uwongo; nao watatoa vielekezo vikubwa na vioja, wawapoteza hata waliochaguliwa, kama inawezekana.[#Mat. 24:5,11; 5 Mose 13:1-3; 2 Tes. 2:8-9.]

25Tazameni, nimetangua kuwaambia ninyi.

26Basi, watakapowaambia ninyi: Tazameni, yuko jangwani! msitoke kwenda kule! Au: Yule! Yumo nyumbani! msiitikie!

27Kwani kama umeme unavyotoka maawioni, ukamulika mpaka machweoni, ndivyo, kutakavyokuwa kurudi kwake Mwana wa mtu.[#Luk. 17:23-24.]

28Penye nyamafu ndipo, tai watakapokusanyikia.*[#Iy. 39:30; Hab. 1:8; Luk. 17:37.]

29Maumivu ya siku zile yatakapopita, papo hapo jua litakuwa jeusi lenye giza, nao mwezi hautaumulikisha mwanga wake, nazo nyota zitaanguka toka mbinguni, nazo nguvu za mbingu zitatukutishwa.[#Yes. 13:10; 34:4; 2 Petr. 3:10.]

30Hapo ndipo, patakapoonekana mbinguni kielekezo cha Mwana wa mtu. Ndipo, watakapoomboleza wao wa makabila yote ya nchi, watakapomwona Mwana wa mtu, anavyokuja juu ya mawingu toka mbinguni mwenye nguvu na utukufu mwingi.[#Mat. 26:64; Dan. 7:13-14; Zak. 12:10; Ufu. 1:7; 19:11-12.]

31Naye atawatuma malaika zake wenye mabaragumu yanayolia sana, wawakusanye waliochaguliwa naye toka pande zote nne, upepo unapotokea, waanzie mwanzoni kwa mbingu, waufikishe mwisho wake.[#5 Mose 30:4; Yes. 27:13; Zak. 2:6; 1 Kor. 15:52; 1 Tes. 4:16; Ufu. 8:1-2.]

32Jifundisheni mfano kwa mkuyu: matawi yake yanapochipua na kuchanua majani, mnatambua, ya kuwa siku za vuli ziko karibu.

33Vivyo hivyo nanyi mtakapoyaona hayo yote tambueni, ya kuwa mwisho umewafikia milangoni!

34Kweli nawaambiani: Kizazi hiki hakitakoma, mpaka yatakapokuwapo hayo yote.

35Mbingu na nchi zitakoma, lakini maneno yangu hayatakoma.[#Mat. 5:18; 1 Petr. 1:25.]

36Lakini ile siku na saa yake itakapofikia, mtu hapajui, wala malaika wa mbingu, wala Mwana, ila Baba peke yake tu.[#Tume. 1:7; 1 Tes. 5:1-2.]

37Kama vilivyokuwa siku za Noa, ndivyo kutakavyokuwa kurudi kwake Mwana wa mtu.[#1 Mose 6:7-9,21; Luk. 17:26-27.]

38Kwani siku zile zilizoyatangulia yale mafuriko makubwa ya maji walikuwa wakila, hata wakinywa, wakioa, hata wakiozwa mpaka siku, Nao alipoingia katika chombo kikubwa.[#1 Mose 7:7; 2 Petr. 3:5-6.]

39Hawakuyatambua, mpaka mafuriko makubwa ya maji yakaja, yakawachukua wote pia. Ndivyo, kutakavyokuwa hata kurudi kwake mwana wa mtu.

40Hapo wawili watakuwa shambani, mmoja atapokewa, mmoja ataachwa.[#Luk. 17:35-36.]

41Hapo wawili watakuwa shambani, mmoja atapokewa, mmoja ataachwa.

42Kwa hiyo kesheni! Kwani hamwijui siku, atakapojia Bwana wenu.[#Mat. 25:13; 1 Tes. 5:2.]

43Lakini litambueni neno hili: Kama mwenye nyumba angaliijua zamu, mwizi atakayojia, angalikesha, asiache, nyumba yake ibomolewe.[#Luk. 12:39-46.]

44Kwa sababu hiyo nanyi mwe tayari! Kwani Mwana wa mtu atajia saa, msiyomwazia.[#Ufu. 16:15.]

45Basi, yuko nani aliye mtumwa mwelekevu na mwerevu, bwana wake akimpa kuwatunza wa nyumbani mwake, awape vyakula, saa yao itakapofika?

46Mwenye shangwe ni mtumwa yule, bwana wake atakayemkuta, akifanya hivyo, atakapokuja.

47Kweli nawaambiani: Atampa kuzitunza mali zake zote.[#Mat. 25:21,23.]

48Lakini mtumwa aliye mwovu atasema moyoni mwake: Bwana wangu anakawia,[#Mbiu. 8:11; 2 Petr. 3:4.]

49akaanza kuwapiga watumwa wenziwe na kula na kunywa pamoja na walevi.

50Basi, bwana wake mtumwa yule atamjia siku, asiyomngojea, na saa, asiyoitambua,

51kisha atamchangua kuwa vipande viwili, nalo fungu lake atampa pamoja na wajanja. Ndiko, kitakakokuwa kilio na kukereza meno.[#Mat. 8:12.]

Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.
Published by: Bible Society of Tanzania