The chat will start when you send the first message.
1*Alipoyaona hayo makundi ya watu akapanda mlimani, akakaa, nao wanafunzi wake wakamkaribia.
2Ndipo, alipokifumbua kinywa chake, akawafundisha akisema:
3Wenye shangwe ndio walio maskini rohoni mwao, maana hao ufalme wa mbingu ni wao.[#Yes. 57:15; Yak. 2:5.]
4Wenye shangwe ndio wanaosikitika, maana hao watatulizwa.[#Sh. 126:5; Yes. 61:2; Ufu. 7:17.; #Mat. 5:39-41; 11:29.]
5Wenye shangwe ndio wapole, maana hao watairithi nchi.[#Sh. 37:11; Luk. 18:9-14.]
6Wenye shangwe ndio wenye njaa na kiu ya kupata wongofu, maana hao watashibishwa.[#Yes. 58:7-8.]
7Wenye shangwe ndio wenye huruma, maana hao watahurumiwa.[#Yak. 2:13.]
8Wenye shangwe ndio waliotakata mioyoni mwao, maana hao watamwona Mungu.[#Sh. 24:4; 51:12; 73:1; 1 Yoh. 3:2-3.]
9Wenye shangwe ndio wapatanishi, maana hao wataitwa wana wa Mungu.[#Ebr. 12:14; Yak. 3:18.]
10Wenye shangwe ndio wanaofukuzwa kwa ajili ya wongofu wao, maana hao ufalme wa mbingu ni wao.[#Yoh. 15:18; 1 Petr. 3:18.]
11Nanyi mtakuwa wenye shangwe, watu watakapowatukana na kuwafukuza na kuwasingizia maneno mabaya yo yote yaliyo ya uwongo kwa ajili yangu mimi.[#1 Petr. 3:14.]
12Furahini na kushangilia! Kwani mshahara wenu ni mwingi mbinguni. Kwani ndivyo, walivyowafukuza wafumbuaji waliowatangulia.*[#Tume. 5:40-41; Ebr. 11:33-38; Yak. 5:10.]
13*Ninyi m chumvi ya nchi. Lakini chumvi ikiwa imepotewa na ukolezi, itatiwa kitu gani, ipate kukolea tena? Hakuna kitu tena, ilichokifalia, itatupwa tu nje, ikanyagwe na watu.[#Mar. 9:49-50; Luk. 14:34-35; Kol. 4:6.]
14Ninyi m mwanga wa ulimwengu. Mji ukiwa juu ya mlima haufichiki.[#Yoh. 8:12.]
15Nao watu wakiwasha taa hawaiweki chini ya kapu, ila huiweka juu ya mwango; ndivyo inavyowaangazia wote waliomo nyumbani.[#Mar. 4:21; Luk. 8:16.]
16Vivyo mwanga wenu uangaze mbele ya watu, wapate kuyaona matendo yenu mema, wamtukuze Baba yenu alioko mbinguni.*[#Ef. 5:8-9; 1 Petr. 2:12.]
17Msiniwazie, ya kuwa nimejia kuyatangua Maonyo au maneno ya Wafumbuaji. Sikujia kutangua, nimejia kutimiza.[#Mat. 3:15; Rom. 3:31; 10:4; 13:10.]
18Kweli nawaambiani: Mpaka hapo, mbingu na nchi zitakapokoma, hata kiandiko kimoja au kichoro kimoja kilichomo katika Maonyo hakitakoma, isipokuwa yametimizwa yote.[#Luk. 16:17; 21:33.]
19Mtu akiondoa moja tu katika maagizo hayo, ijapo liwe dogo, na kufundisha watu hivyo, huyo ataitwa mdogo kuliko wote katika ufalme wa mbingu; lakini mtu akiyafanya maagizo hayo na kufundisha watu hivyo, huyo ataitwa mkubwa katika ufalme wa mbingu.[#Mat. 22:27-40; Yak. 2:10.]
20Kwani nawaambiani: *Wongofu wenu usipoupita wongofu wao waandishi na Mafariseo, hamtaingia kabisa katika ufalme wa mbingu.[#Mat. 6:1-7; Mar. 7:3-4.]
21Mmesikia, ya kuwa watu wa kale waliambiwa: Usiue! Mtu akiua, itampasa, ahukumiwe.[#2 Mose 20:13; 21:12; 3 Mose 24:17; 5 Mose 17:8.]
22Lakini mimi nawaambiani: Kila anayemwonea ndugu yake chuki, itampasa, ahukumiwe. Naye atakayemwambia ndugu yake: Mshenzi wee! itampasa, ahukumiwe na baraza ya wakuu wote. Lakini atakayemtukana ndugu yake, itampasa, atupwe shimoni mwa moto.[#1 Yoh. 3:15.]
23Ukipeleka kipaji chako mezani pa Bwana, ukakumbuka hapo, ya kuwa ndugu yako ana mfundo moyoni kwa ajili yako,[#Mar. 11:25.]
24basi, kwanza kiache kipaji chako mbele ya meza ya Bwana! Uende kwanza, upatane na ndugu yako! Kisha urudi, ukitoe kipaji chako!
25Umwitikie mshtaki wako upesi ukiwa naye, mngaliko njiani! Maana mshtaki wako asikupeleke kwa mwenye hukumu, naye mwenye hukumu asikutie mkononi mwa askari, ukatiwa kifungoni.[#Mat. 6:14-15; 18:35; Luk. 12:58-59.]
26Kweli nakuambia: Hutatoka humo kabisa, mpaka utakapomaliza kulipa, isisalie hata senti moja*[#Mat. 18:34.]
27Mmesikia ya kuwa ilisemwa: Usizini![#Mat. 19:3-9; 2 Mose 20:14.]
28Lakini mimi nawaambiani: Kila mtu anayetazama mwanamke kwa kumtamani, basi, huyo amekwisha zini naye moyoni mwake.[#2 Sam. 1; Iy. 31:1; 2 Petr. 2:14.]
29Nawe kama jicho lako la kuume linakukwaza, ling'oe, ulitupe mbali! kwani itakufaa, kiungo kimoja tu kiangamie, kuliko mwili wako mzima ukitupwa shimoni mwa moto.[#Mat. 18:8; Mar. 9:43,47; Kol. 3:5.]
30Nawe kama mkono wako wa kuume unakukwaza, uukate, uutupe mbali! Kwani itakufaa, kiungo kimoja tu kiangamie, kuliko mwili wako mzima ukijiendea shimoni mwa moto.
31Tena ilisemwa: Mtu akimwacha mkewe ampe cheti cha kuachana.[#Mat. 19:3-9; 5 Mose 24:1.]
32Lakini mimi nawaambiani: kila mtu anayemwacha mkewe, isipokuwa kwa ajili ya ugoni, huyo anamzinisha. Naye atakayeoa mke aliyeachwa anazini.[#Luk. 16:18; 1 Kor. 7:10-11.]
33Tena mmesikia, ya kuwa watu wa kale waliambiwa: Usiape kiapo cha uwongo, lakini umtimizie Mungu, uliyomwapia![#2 Mose 20:7; 3 Mose 19:12; 4 Mose 30:3.]
34Lakini mimi nawaambiani: Usiape na kutaja yoyote, wala mbingu, kwani ndicho kiti cha kifalme cha Mungu;[#Mat. 23:16-22; Yes. 66:1; Tume. 7:49.]
35Wala nchi, kwani ndipo pa kuiwekea miguu yake; wala Yerusalemu, kwani ndio mji wa mfalme aliye mkuu;[#Sh. 48:3.]
36wala kichwa chako, kwani hata unywele mmoja tu huwezi kuugeuza uwe mweupe au mweusi.
37Mkisema: Ndio, iwe ndio kweli! Au mkisema: Sio, iwe sio kweli! Lakini yanayoyapita hayo hutoka kwa Mbaya.[#2 Kor. 1:17; Yak. 5:12.]
38Mmesikia, ya kuwa ilisemwa: Jicho kwa jicho, jino kwa jino![#3 Mose 24:19-20.]
39Lakini mimi nawaambiani: Msibishane na mbaya! Lakini mtu akikupiga kofi shavu la kuume, mgeuzie la pili, alipige nalo![#3 Mose 19:18; Rom. 12:21; 1 Petr. 2:20.]
40Mtu akitaka kushtakiana na wewe, apate kuichukua shuka yako, basi, umwachie na kanzu![#1 Kor. 6:7; Ebr. 10:34.]
41Naye atakayekushurutiza kwenda naye nusu saa, basi, nenda naye saa nzima!
42Anayekuomba umpe, naye anayetaka kukopa kwako usimgeukie mgongo!
43Mmesikie, ya kuwa ilisemwa: Umpende mwenzio, naye adui yako umchukie![#3 Mose 19:18.]
44Lakini mimi nawaambiani: Wapendeni adui zenu! Wabarikini wanaowaapiza! Wafanyieni mazuri wanaowachukia! Waombeeni wanaowachokoza na kuwafukuza![#2 Mose 23:4-5; Rom. 12:14,20; Luk. 6:27-28; 23:34; Tume. 7:60.]
45Fanyeni hivi, mpate kuwa wana wa Baba yenu alioko mbinguni! Kwani yeye huwacheshea jua lake wabaya na wema, tena huwanyeshea mvua waongofu nao wapotovu.[#Ef. 5:1.]
46Kwani mkiwapenda wanaowapendani mtapata mshahara gani? Je? Hata watoza kodi hawafanyi hivyo hivyo?
47Tena mkiwaamkia ndugu zenu tu mnawapitaje wengine? Je? Hata wamizimu hawafanyi vivyo hivyo?
48Basi, ninyi mwe watimilifu, kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mtimilifu![#3 Mose 19:2; 5 Mose 18:13; Ef. 5:1-2.]