The chat will start when you send the first message.
1Angalieni, msigawie watu vipaji vyenu machoni pa watu, kwamba wawaone! Msipojiangalia hivyo, hamna mshahara kwa Baba yenu alioko mbinguni.
2Basi, ukimgawia mtu usipigishe baragumu mbele yako kama wanavyofanya wajanja katika nyumba za kuombea na katika njia za mijini, wapate kutukuzwa na watu. Kweli nawaambiani: wamekwisha upata mshahara wao.[#1 Kor. 13:3.]
3Lakini wewe ukimgawia mtu, mkono wako wa kushoto usitambue, wa kuume unayoyafanya,[#Mat. 25:37-40; Rom. 12:8.]
4huko kugawa kwako kuwe kumejificha! Ndipo, Baba yako anayeyaona hata yanayojificha atakapokulipa waziwazi.
5Tena mnapomwomba Mungu msiwe kama wajanja! Kwani wanapenda kuomba wakisimama katika nyumba za kuombea na pembeni pa njia za mijini, watu wapate kuwaona. Kweli nawaambiani: wamekwisha upata mshahara wao.[#Mat. 23:5.]
6Lakini wewe unapoomba uingie mwako chumba cha ndani na kuufunga mlango wako! Kisha umwombe Baba yako alioko fichoni! Ndipo, Baba yako anayeyaona hata yanayojificha atakapokulipa waziwazi.[#2 Fal. 4:33; Yes. 26:20.]
7Tena mnapoomba msijisemee maneno tu kama wamizimu! Kwani hudhani, ya kuwa maneno yao mengi yatawapatia kusikilizwa.[#Yes. 1:15.]
8Msifanane nao! Kwani Baba yenu anayajua yanayowapasa, mnapokuwa hamjamwomba.[#Mat. 6:32.]
9Ninyi mnapoomba mwombe hivi: Baba yetu ulioko mbinguni, Jina lako litakaswe![#Luk. 11:2-4.]
10Ufalme wako uje! Uyatakayo yatimizwe nchini, kama yanavyotimizwa mbinguni![#Mat. 7:21; Luk. 22:42.]
11Tupe leo chakula chetu cha kututunza!
12Tuondolee makosa yetu, kama nasi tulivyowaondolea waliotukosea![#Mat. 6:14-15; 18:21-35.]
13Usituingize majaribuni! Ila tuokoe maovuni! Kwani wako ni ufalme na nguvu na utukufu kale na kale. Amin.[#1 Mambo 29:11-13; Luk. 22:32; Yoh. 17:15; 1 Kor. 10:13.]
14Kwani ninyi mnapowaondolea watu makosa yao, Baba yenu wa mbinguni atawandolea ninyi vilevile.[#Mat. 18:21-35.]
15Lakini ninyi msipowaondolea watu makosa yao, hata Baba yenu hatawaondolea ninyi makosa yenu.[#Mar. 11:25-26.]
16Tena mnapofunga msikunjamane nyuso kama wajanja! Kwani huzirembua nyuso, kusudi watu wawaone, wanavyofunga. Kweli nawaambiani: Wamekwisha upata mshahara wao.[#Yes. 58:5-9.]
17Lakini wewe unapofunga jipake kichwa chako mafuta, unawe nao uso wako,
18kusudi watu wasikuone, ya kama unafunga, ila akuone Baba yako alioko fichoni. Ndipo, Baba yako anayeyaona yanayojificha atakapokulipa.
19Msijilimbikie malimbiko nchini, mende na kutu zinapoyaharibu! Nao wezi huyafukua na kwiba.
20Lakini jilimbikieni malimbiko mbinguni, yasikoharibiwa na mende wala na kutu, wala wezi wasikoyafukua na kwiba![#Mat. 19:21; Luk. 12:20,33-34; Kol. 3:1-2; Ebr. 10:34.]
21Kwani limbiko lako liliko, ndiko, nao moyo wako utakakokuwa.
22Taa ya mwili ni jicho. Basi jicho lako liking'aa, mwili wako wote utakuwa na mwanga.[#Luk. 11:34-36.]
23Lakini jicho lako likiwa bovu, mwili wako wote utakuwa na giza. Basi, mwanga uliomo ndani yako unapokuwa giza, giza yenyewe itakuwaje?
24*Hakuna mtu anayeweza kutumikia mabwana wawili. Kwani itakuwa hivi: atamchukia wa kwanza na kumpenda wa pili, au atashikamana naye wa kwanza na kumbeza wa pili. Hamwezi kuwatumikia wote wawili, Mungu na Mali za Nchini (Mamona).[#Luk. 16:9,14.]
(25-33: Luk. 12:22-31.)25Kwa hiyo nawaambiani: Msiyasumbukie maisha yenu mkisema: Tutakula nini? Tutakunywa nini? Wala msiisumbukie miili yenu mkisema: Tutavaa nini? Je? Maisha hayapiti vyakula? Nao mwili haupiti mavazi?[#Fil. 4:6; 1 Tim. 6:6; Ebr. 13:5; 1 Petr. 5:7.]
26Watazameni ndege wa angani! Hawapandi, wala hawavuni, wala hawakusanyi waweke vichanjani. Naye Baba yenu wa mbinguni anawalisha nao. Je? Nyinyi hamwapiti hao?[#Mat. 10:29-31.]
27Tena kwenu yuko nani anayeweza kwa kusumbuka kwake kujiongezea miaka yake kipande kama cha mkono mmoja tu?
28Tena yale mavazi, mbona mnayasumbukia? Jifundisheni mnapoyatazama maua ya uwago yaliyoko porini kama yanavyokua! Hayafanyi kazi, wala hayafumi nguo.
29Lakini nawaambiani: Hata Salomo katika utukufu wake wote hakuvikwa kama moja lao.[#1 Fal. 10.]
30Basi Mungu akiyavika hivyo majani ya porini yanayokaa leo tu, kesho yatupwe katika mabiwi, yateketee, Je? Hatazidi kuwavika ninyi? Mbona mna mtegemea kidogo tu?
31Basi msisumbuke mkisema: Tutakula nini? au: Tutakunywa nini? au: Tutavaa nini?
32Kwani wamizimu ndio wanaoyatafuta hayo yote; lakini Baba yenu wa mbinguni amewajua, ya kuwa mnapaswa nayo hayo yote.
33Utafuteni kwanza ufalme wa Mungu na wongofu wake! Ndivyo, mtakavyopewa hayo yote.[#Rom. 14:17; 1 Fal. 3:13-14; Sh. 37:4,25.]
34Basi, msisumbukie ya kesho! Kwani siku ya kesho itayasumbukia yaliyo yake. Inatosha, kila siku iwe na uovu wake.[#Mat. 6:11; 2 Mose 16:19.]