The chat will start when you send the first message.
1Mose akawaambia wakuu wa mashia ya wana wa Isiraeli kwamba: Hili ndilo neno, Bwana aliloliagiza:[#3 Mose 27:2-25.]
2Mtu akimwapia Bwana kumtolea cho chote au kiapo cha kujifungia kifungo cho chote, asilitangue neno lake, ila sharti ayafanye yote, kama kinywa chake kilivyoyasema.[#5 Mose 23:21; Amu. 11:35; Mbiu. 5:4-5.]
3Mwanamke akimwapia Bwana kumtolea cho chote, au akijifungia kiungo, akingali nyumbani mwa baba yake, au akingali kijana bado,
4naye baba yake akipata habari ya kule kuapa kwake au ya kujifungia kifungo cho chote, basi, baba yake akimnyamazia kimya, yote aliyoyaapa yatakuwapo, navyo vifungo vyote, alivyojifungia, vitakuwa vimemfunga.
5Lakini baba yake akimkataza siku hiyo, anapopata habari, basi, yote aliyoyaapa navyo vifungo vyote, alivyojifungia, havitakuwapo, naye Bwana atamwondolea jambo hilo, kwa kuwa baba yake amemkataza.
6Lakini atakapoolewa akiwa mwenye mambo, aliyoyaapa, au midomo yake iliyojisemea tu ya kjifungia kifungo,
7basi, mumewe akipata habari na kumnyamazia kimya siku hiyo, anapopata habari, yatakuwapo aliyoyaapa, navyo vifungo, alivyojifungia, vitakuwapo.
8Lakini mumewe akimkataza siku hiyo, anapopata habari, basi, yeye atakuwa ameyatangua hayo mambo, aliyokuwa nayo kwa kuapa, nayo yale, midomo yake iliyojisemea tu ya kujifungia kifungo, naye Bwana atamwondolea jambo hilo.
9Lakini mjane au mwanamke aliyeachana na mumewe atakayoyaapa navyo vifungo vyote, atakavyojifungia, vitakuwapo, vimfunge.
10Mwanamke akijiapia mambo yo yote nyumbani mwa mumewe au akijifungia kifungo cho chote kwa kiapo,
11basi, mumewe akipata habari yake na kumnyamazia kimya, asimkataze, yote aliyoyaapa yatakuwapo, navyo vifungo vyote, alivyojifungia, vitakuwapo.
12Lakini mumewe akivitangua kabisa siku hiyo, anapopata habari, basi, yote yaliyotoka midomoni mwa mkewe ya kiapo nayo ya kujifungia kifungo hayatakuwapo, kwa kuwa mumewe ameyatangua, naye Bwana atamwondolea jambo hilo.
13Yote, mwanamke aliyoyaapa, navyo vifungo vyote, alivyojifungia kwa kiapo vya kujiumiza mwenyewe, mumewe anaweza kuyatia nguvu, yawepo, tena mumewe anaweza kuyatangua.
14Mumewe akimnyamazia kimya tangu leo hata kesho, basi, amekwisha kuyatia nguvu, yawepo yote, aliyoyaapa, navyo vifungo vyote, alivyojifungia, amekwisha kuvitia nguvu navyo, viwepo, kwani amemnyamazia kimya siku hiyo, alipopata habari.
15Naye akiisha kupata habari, tena akivitangua siku za nyuma hana budi kujitwika manza za mkewe.
16Haya ndiyo maongozi, Bwana aliyomwagiza Mose ya kuwaongoza mtu na mkewe, hata baba na mwanawe wa kike, akiwa angaliko kijana na kukaa nyumbani mwa baba yake.