4 Mose 7

4 Mose 7

Matunzo, wakuu waliyolitolea Hema Takatifu.

1Ikawa siku hiyo, Mose alipokwisha kulisimamisha Kao na kulipaka mafuta na kulieua kuwa takatifu pamoja na vyombo vyake vyote na kuipaka mafuta nayo meza ya kutambikia pamoja na vyombo vyake vyote na kuvieua kuwa vitakatifu,[#2 Mose 40:9-10.]

2ndipo, wakuu wa Waisiraeli waliokuwa vichwa vya milango ya baba zao walipovitoa vipaji vyao vya tambiko, kwa kuwa wakuu wa mashina waliowasimamia wale waliokaguliwa.

3Wakayaleta hayo matoleo yao, wakatoa mbele ya Bwana magari sita yenye mafuniko na ng'ombe kumi na wawili, kila wakuu wawili wakitoa gari moja, na kila mkuu mmoja akitoa ng'ombe mmoja; hapo mbele ya Kao ndipo, walipoyatoa.

4Bwana akamwambia Mose kwamba:

5Yachukue kwao, nayo yatumiwe kuusaidia utumishi wa Hema la Mkutano. Uwape Walawi, kila mtu kama kazi ya utumishi wake ilivyo.

6Mose akayachukua hayo magari pamoja na ng'ombe, akawapa Walawi.

7Magari mawili na ng'ombe wanne akawapa wana wa Gersoni kwa hivyo, utumishi wao ulivyokuwa.

8Magari manne na ng'ombe wanane akawapa wana wa Merari kwa hivyo, utumishi wao ulivyokuwa, Itamari, mwana wa mtambikaji Haroni, aliousimamia.[#2 Mose 38:21; 4 Mose 4:28,33.]

9Lakini wana wa Kehati hakuwapa, kwani utumishi wao ulikuwa wa Pataktifu, hawakuwa na budi kuvichukua vyombo vyake mabegani.[#4 Mose 4:15.]

10Kisha wakuu wakatoa vipaji vya weuo wa meza ya kutambikia siku hiyo, ilipopakwa mafuta; ndipo, wakuu walipoyatoa matoleo yao mbele ya meza ya kutambikia.

11Bwana akamwambia Mose: Kila mkuu mmoja awe na siku yake, nayo hiyo siku yake ndipo kila mkuu mmoja ayatoe matoleo yake ya weuo wa meza ya kutambikia.[#4 Mose 1:4-16; 2:3-29.]

12Aliyeyatoa matoleo yake siku ya kwanza alikuwa Nasoni, mwana wa Aminadabu, wa shina la Yuda.

13Matoleo yake yalikuwa: bakuli moja ya fedha, kiasi chake kilikuwa fedha 130, na chano kimoja cha fedha, kiasi chake kilikuwa fedha 70, nazo ni zile fedha zilizotumika Patakatifu; zote mbili zilikuwa zimejaa unga mwembamba wa ngano uliochanganywa na mafuta kuwa kilaji cha tambiko;

14tena kijiko kimoja cha dhahabu, kiasi chake kilikuwa fedha 180, nacho ilikuwa kimejaa mavukizo;

15tena dume moja la ng'ombe aliye kijana bado na dume moja la kondoo na mwana kondoo mmoja wa mwaka mmoja kuwa ng'ombe za tambiko za kuteketezwa nzima,

16tena dume moja la mbuzi kuwa ng'ombe ya tambiko ya weuo,

17tena ng'ombe wawili na madume matano ya kondoo na wana mbuzi watano na wana kondoo watano wa mwaka mmoja kuwa ng'ombe za tambiko za shukrani. Haya yalikuwa matoleo yake Nasoni, mwana wa Aminadabu.

18Siku ya pili Netaneli, mwana wa Suari, mkuu wa Isakari, akaleta vipaji vyake.

19Matoleo yake, aliyoyatoa, yalikuwa: bakuli moja ya fedha, kiasi chake kilikuwa fedha 130, na chano kimoja cha fedha, kiasi chake kilikuwa fedha 70, nazo ni zile fedha zilizotumika Patakatifu; zote mbili zilikuwa zimejaa unga mwambamba wa ngano uliochanganywa na mafuta kuwa kilaji cha tambiko;

20tena kijiko kimoja cha dhahabu, kiasi chake kilikuwa fedha 180, nacho kilikuwa kimejaa mavukizo;

21tena dume moja la ng'ombe aliye kijana bado na dume moja la kondoo na mwana kondoo mmoja wa mwaka mmoja kuwa ng'ombe za tambiko za kuteketezwa nzima,

22tena dume moja la mbuzi kuwa ng'ombe ya tambiko ya weuo,

23tena ng'ombe wawili na madume matano ya kondoo na wana mbuzi watano na wana kondoo watano wa mwaka mmoja kuwa ng'ombe za tambiko za shukrani. Haya yalikuwa matoleo yake Netaneli, mwana wa Suari.

24Siku ya tatu Eliabu, mwana wa Heloni, mkuu wa wana wa Zebuluni, akaleta vipaji vyake.

25Matoleo yake yalikuwa: bakuli moja ya fedha kiasi chake kilikuwa fedha 130, na chano kimoja cha fedha, kiasi chake kilikuwa fedha 70, nazo ni zile fedha zilizotumika Patakatifu; zote mbili zilukuwa zimejaa unga mwembamba wa ngano uliochanganywa na mafuta kuwa kilaji cha tambiko;

26tena kijiko kimoja cha dhahabu, kiasi chake kilikuwa fedha 180, nacho kilikuwa kimejaa mavukizo;

27tena dume moja la ng'ombe aliye kijana bado na dume moja la kondoo na mwana kondoo mmoja wa mwaka mmoja kuwa ng'ombe za tambiko za kuteketezwa nzima,

28tena dume moja la mbuzi kuwa ng'ombe ya tambiko ya weuo,

29tena ng'ombe wawili na madume matano ya kondoo na wana mbuzi watano na wana kondoo watano wa mwaka mmoja kuwa ng'ombe za tambiko za shukrani. Haya yalikuwa matoleo yake Eliabu, mwana wa Heloni.

30Siku ya nne Elisuri, mwana wa Sedeuri, mkuu wa wana wa Rubeni, akaleta vipaji vyake.

31Matoleo yake yalikuwa: bakuli moja ya fedha, kiasi chake kilikuwa 130, na chano kimoja cha fedha, kiasi chake kilikuwa fedha 70, nazo ni zile fedha zilizotumika Patakatifu; zote mbili zilikuwa zimejaa unga mwembamba wa ngano uliochanganywa na mafuta kuwa kilaji cha tambiko;

32tena kijiko kimoja cha dhahabu, kiasi chake kilikuwa fedha 180, nacho kilikuwa kimejaa mavukizo;

33tena dume moja la ng'ombe aliye kijana bado na dume moja la kondoo na mwana kondoo mmoja wa mwaka mmoja kuwa ng'ombe za tambiko za kuteketezwa nzima,

34tena dume moja la mbuzi kuwa ng'ombe ya tambiko ya weuo.

35tena ng'ombe wawili na madume matano ya kondoo na wana mbuzi watano na wana kondoo watano wa mwaka mmoja kuwa ng'ombe za tambiko za shukrani. Haya yalikuwa matoleo yake Elisuri, mwana wa Sedeuri.

36Siku ya tano Selumieli, mwana wa Surisadai, mkuu wa wana wa Simeoni akaleta vipaji vyake.

37Matoleo yake yalikuwa: bakuli moja ya fedha, kiasi chake kilikuwa fedha 130, na chano kimoja cha fedha, kiasi chake kilikuwa fedha 70, nazo ni zile fedha zilizotumika Patakatifu; zote mbili zilikuwa zimejaa unga mwembamba wa ngano uliochanganywa na mafuta kuwa kilaji cha tambiko;

38tena kijiko kimoja cha dhahabu, kiasi chake kilikuwa fedha 180, nacho kilikuwa kimejaa mavukizo;

39tena dume moja la ng'ombe aliye kijana bado na dume moja la kondoo na mwana kondoo mmoja wa mwaka mmoja kuwa ng'ombe za tambiko za kuteketezwa nzima,

40tena dume moja la mbuzi kuwa ng'ombe ya tambiko ya weuo,

41tena ng'ombe wawili na madume matano ya kondoo na wana mbuzi watano na wana kondoo watano wa mwaka mmoja kuwa ng'ombe za tambiko za shukrani. Haya yalikuwa matoleo yake Selumieli, mwana wa Surisadai.

42Siku ya sita Eliasafu, mwana wa Deueli, mkuu wa wana wa Gadi, akaleta vipaji vyake.

43Matoleo yake yalikuwa: bakuli moja ya fedha, kiasi chake kilikuwa fedha 130, na chano kimoja cha fedha, kiasi chake kilikuwa fedha 70, nazo ni zile fedha zilizotumika Patakatifu; zote mbili zilikuwa zimejaa unga mwembamba wa ngano uliochanganywa na mafuta kuwa kilaji cha tambiko;

44tena kijiko kimoja cha dhahabu, kiasi chake kilikuwa fedha 180, nacho kilikuwa kimejaa mavukizo;

45tena dume moja la ng'ombe aliye kijana bado na dume moja la kondoo na mwana kondoo mmoja wa mwaka mmoja kuwa ng'ombe za tambiko za kuteketezwa nzima,

46tena dume moja la mbuzi kuwa ng'ombe ya tambiko ya weuo,

47tena ng'ombe wawili na madume matano ya kondoo na wana mbuzi watano na wana kondoo watano wa mwaka mmoja kuwa ng'ombe za tambiko za shukrani. Haya yalikuwa matoleo yake Eliasafu, mwana wa Deueli.

48Siku ya saba Elisama, mwana wa Amihudi, mkuu wa wana wa Efuraimu, akaleta vipaji vyake.

49Matoleo yake yalikuwa: bakuli moja ya fedha, kiasi chake kilikuwa fedha 130, na chano kimoja cha fedha, kiasi chake kilikuwa fedha 70, nazo ni zile fedha zilizotumika Patakatifu; zote mbili zilikuwa zimejaa unga mwembamba wa ngano uliochanganywa na mafuta kuwa kilaji cha tambiko;

50tena kijiko kimoja cha dhahabu, kiasi chake kilikuwa fedha 180, nacho kilikuwa kimejaa mavukizo;

51tena dume moja la ng'ombe aliye kijana bado na dume moja la kondoo na mwana kondoo mmoja wa mwaka mmoja kuwa ng'ombe za tambiko za kuteketezwa nzima,

52tena dume moja la mbuzi kuwa ng'ombe ya tambiko ya weuo,

53tena ng'ombe wawili na madume matano ya kondoo na wana mbuzi watano na wana kondoo watano wa mwaka mmoja kuwa ng'ombe za tambiko za shukrani. Haya yalikuwa matoleo yake Elisama, mwana wa Amihudi.

54Siku ya nane Gamulieli, mwana wa Pedasuri, mkuu wa wana wa Manase, akaleta vipaji vyake.

55Matoleo yake yalikuwa: bakuli moja ya fedha, kiasi chake kilikuwa fedha 130, na chano kimoja cha fedha kiasi chake kilikuwa fedha 70, nazo ni zile fedha zilizotumika Patakatifu; zote mbili zilikuwa zimejaa unga mwembamba wa ngano uliochanganywa na mafuta kuwa kilaji cha tambiko;

56tena kijiko kimoja cha dhahabu, kiasi chake kilikuwa fedha 180, nacho kilikuwa kimejaa mavukizo;

57tena dume moja la ng'ombe aliye kijana bado na dume moja la kondoo na mwana kondoo mmoja wa mwaka mmoja kuwa ng'ombe za tambiko za kuteketezwa nzima;

58tena dume moja la mbuzi kuwa ng'ombe ya tambiko ya weuo;

59tena ng'ombe wawili na madume matano ya kondoo na wana mbuzi watano na wana kondoo watano wa mwaka mmoja kuwa ng'ombe za tambiko za shukrani. Haya yalikuwa matoleo yake Gamulieli, mwana wa Pedasuri.

60Siku ya tisa Abidani, mwana wa Gideoni, mkuu wa wana wa Benyamini, akaleta vipaji vyake.

61Matoleo yake yalikuwa: bakuli moja ya fedha, kiasi chake kilikuwa fedha 130, na chano kimoja cha fedha, kiasi chake kilikuwa fedha 70, nazo ni zile fedha zilizotumika Patakatifu; zote mbili zilikuwa zimejaa unga mwembamba wa ngano uliochanganywa na mafuta kuwa kilaji cha tambiko;

62tena kijiko kimoja cha dhahabu, kiasi chake kilikukwa fedha 180, nacho kilikuwa kimejaa mavukizo;

63tena dume moja la ng'ombe aliye kijana bado na dume moja la kondoo na mwana kondoo mmoja wa mwaka mmoja kuwa ng'ombe za tambiko za kuteketezwa nzima,

64tena dume moja la mbuzi kuwa ng'ombe ya tambiko ya weuo,

65tena ng'ombe wawili na madume matano ya kondoo na wana mbuzi watano na wana kondoo watano wa mwaka mmoja kuwa ng'ombe za tambiko za shukrani. Haya yalikuwa matoleo yake Abidani, mwana wa Gideoni.

66Siku ya kumi Ahiezeri, mwana wa Amisadai, mkuu wa wana wana wa Dani, akaleta vipaji vyake.

67Matoleo yake yalikuwa: bakuli moja ya fedha, kiasi chake kilikuwa fedha 130, na chano kimoja cha fedha, kiasi chake kilikuwa fedha 70, nazo ni zile fedha zilizotumika Patakatifu; zote mbili zilikuwa zimejaa unga mwembamba wa ngano uliochanganywa na mafuta kuwa kilaji cha tambiko;

68tena kijiko kimoja cha dhahabu, kiasi chake kilikuwa fedha 180, nacho kilikuwa kimejaa mavukizo;

69tena dume moja la ng'ombe aliye kijana bado na dume moja la kondoo na mwana kondoo mmoja wa mwaka mmoja kuwa ng'ombe za tambiko za kuteketezwa nzima,

70tena dume moja la mbuzi kuwa ng'ombe ya tambiko ya weuo;

71tena ng'ombe wawili na madume matano ya kondoo na wana mbuzi watano na wana kondoo watano wa mwaka mmoja kuwa ng'ombe za tambiko za shukrani. Haya yalikuwa matoleo yake Ahiezeri mwana wa Amisadai.

72Siku ya kumi na moja Pagieli, mwana wa Okrani, mkuu wa wana wa Aseri, akaleta vipaji vyake.

73Matoleo yake yalikuwa: bakuli moja ya fedha, kiasi chake kilikuwa fedha 130, na chano kimoja cha fedha, kiasi chake kilikuwa fedha 70, nazo ni zile fedha zilizotumika Patakatifu; zote mbili zilikuwa zimejaa unga mwembamba wa ngano uliochanganywa na mafuta kuwa kilaji cha tambiko;

74tena kijiko kimoja cha dhahabu, kiasi chake kilikuwa fedha 180, nacho kilikuwa kimejaa mavukizo;

75tena dume moja la ng'ombe aliye kijana bado na dume moja la kondoo na mwana kondoo mmoja wa mwaka mmoja kuwa ng'ombe za tambiko za kuteketezwa nzima,

76tena dume moja la mbuzi kuwa ng'ombe ya tambiko ya weuo,

77tena ng'ombe wawili na madume matano ya kondoo wa mwaka mmoja na wana mbuzi watano na wana kondoo watano wa mwaka mmoja kuwa ng'ombe za tambiko za shukrani. Haya yalikuwa matoleo yake Pagieli, mwana wa Okrani.

78Siku ya kumi na mbili Ahira, mwana wa Enani, mkuu wa wana wa Nafutali, akaleta vipaji vyake.

79Matoleo yake yalikuwa: bakuli moja ya fedha, kiasi chake kilikuwa fedha 130, na chano kimoja cha fedha, kiasi chake kilikuwa fedha 70, nazo ni zile fedha zilizotumika Patakatifu; zote mbili zilikuwa zimejaa unga mwembamba wa ngano uliochanganywa na mafuta kuwa kilaji cha tambiko;

80tena kijiko kimoja cha dhahabu, kiasi chake kilikuwa fedha 180, nacho kilikuwa kimejaa mavukizo;

81tena dume moja la ng'ombe aliye kijana bado na dume moja la kondoo na mwana kondoo mmoja wa mwaka mmoja kuwa ng'ombe za tambiko za kuteketezwa nzima,

82tena dume moja la mbuzi kuwa ng'ombe ya tambiko ya weuo,

83tena ng'ombe wawili na madume matano ya kondoo na wana mbuzi watano na wana kondoo watano wa mwaka mmoja kuwa ng'ombe za tambiko za shukrani. Haya yalikuwa matoleo yake Ahira, mwana wa Enani.

84Hivi vilikuwa vipaji, wakuu wa Waisiraeli walivyovitoa vya weuo wa meza ya kutambikia siku hiyo, ilipopakwa mafuta: mabakuli yaa fedha 12 na vyano vya fedha 12 na vijiko vya dhahabu 12.

85Kila bakuli moja kiasi chake kilikuwa fedha 130, kila chano kimoja kiasi chake kilikuwa fedha 70; jumla ya fedha za hivi vyombo ilikuwa fedha 2400, nazo ni zile fedha zilizotumika Patakatifu.

86Vijiko vya dhahabu vilivyojaa mavukizo vilikuwa 12, kila kijiko kimoja kiasi chake kilikuwa vipande kumi vya dhahabu, ndio fedha 180; dhahabu zote za hivyo vijiko vilikuwa vipande 120, ndio fedha 2160.

87Jumla ya ng'ombe za tambiko za kuteketezwa nzima ilikuwa: madume 12 ya ng'ombe, mmadume 12 ya kondoo, wana kondoo wa mwaka mmoja 12 pamoja na vilaji vyao vya tambiko; tena madume 12 ya mbuzi kuwa ng'ombe za tambiko za weuo.

88Nayo jumla ya ng'ombe za tambiko za shukrani ilikuwa: Ng'ombe 24, madume 60 ya kondoo, wana mbuzi 60, wana kondoo 60 wa mwaka mmoja; hivi vilikuwa vipaji vya weuo wa meza ya kutambikia, ilipokwisha kupakwa mafuta.

89Kisha kila mara Mose alipoingia Hemani mwa Mkutano kusema na Bwana alisikia, sauti yake ikisema naye toka hapo penye Kiti cha Upozi kilicholifunika Sanduku la Ushahidi, nayo ilitoka katikati ya Makerubi, ikasema naye.[#2 Mose 25:21-22; 1 Sam. 3:3-14.]

Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.
Published by: Bible Society of Tanzania