The chat will start when you send the first message.
1Mungu, nikushangiliaye, usinyamaze!
2Kwani waisokucha na wadanganyifu wamenifumbulia vinywa, wakasema na mimi kwa ndimi zilizo zenye uwongo.
3Maneno yenye machukivu yakanizunguka; lakini wakinigombeza hivyo, hakuna sababu yo yote.
4Kwa hivyo, ninavyowapenda, wananipingia, nami naliwaombea wao hao.
5Kweli kwa mema, niliyowafanyizia, wananirudishia mabaya, kwa upendo wangu wananirudishia uchukivu.[#Sh. 35:12.]
6Weka mtu asiyekucha, amwangalie aliye hivyo! Satani mwenyewe amsimamie kuumeni kwake!
7Kwenye hukumu sharti atokezwe kuwa mwenye kushindwa, nako kuomba kwake sharti kuwaziwe kuwa kukosa!
8Siku zake na zifupizwe kuwa chache! Mtu mwingine na autwae ukaguzi wake![#Tume. 1:20.]
9Watoto wake na waachwe peke yao! Naye mkewe na awe mjane!
10Wanawe na waje kutangatanga na kuombaomba kwa kufukuzwa kwenye mahame yao, wakijitafutia vyakula!
11Mkopeshaji na ajitwalie yote yaliyo yake, tena wageni na wapokonye aliyoyapata na kuyasumbukia!
12Pasiwepo anayemwendea kwa upole, wala pasiwepo anayewahurumia watoto wake walioachwa peke yao!
13Watoto, atakaowaacha, sharti waje kung'olewa, katika kizazi cha pili sharti jina lao litoweke!
14Manza, baba zake walizozikora na zikumbukwe kwake Bwana! Makosa ya mama yake yasifutwe,[#2 Mose 20:5.]
15yawepo machoni pake Bwana siku zote! Aung'oe ukumbusho wao katika nchi![#Fano. 10:7.]
16Kwa sababu hakukumbuka kufanya yenye upole, akawakimbiza kwake wanyonge na wakiwa nao waliopondeka mioyo, awaue kabisa.
17Apizo, alilolipenda, na limjie mwenyewe! Kwa kuwa hakupendezwa na mbaraka, na imkalie mbali naye!
18Akajivika apizo, kama ni kanzu yake, likamwingia moyoni, kama ni maji, au kama ni kiini kilichomo katika mifupa yake.[#4 Mose 5:22.]
19Na limwie kama vazi la kujifunika, au kama mshipi, anaojifunga siku zote!
20Hayo Bwana awalipishe wao wanipingiao, nao wanaoisingizia roho yangu kuwa yenye mabaya!
21Nawe Mungu, Bwana wangu, nifanyizie yalipasayo Jina lako! Kwa kuwa upole wako ni mwema, nipoe!
22Kwani mimi ni mnyonge hata mkiwa, nao moyo wangu humu kifuani mwangu umeumia.
23Ninajiendea kama kivuli kinachojivuta, ninafukuzwa kama funutu.
24Magoti yangu yamelegea kwa kufunga mifungo, nyama za mwili wangu zimekonda, hazina mafuta.
25Kwa hiyo mimi nimekuwa kwao mtu wa kumsimanga, wanaponiona huvitingisha vichwa vyao.[#Sh. 22:8.]
26Nisaidie Bwana, Mungu wangu! Niokoe kwa upole wako!
27Ndipo, watakapoujua mkono wako, ya kuwa ndio, tena watajua, ya kuwa umeyafanya, wewe Bwana.
28Wao na waapize! Nawe na ubariki! Wakiinuka na wapatwe na soni, mtumishi wako afurahi![#Mat. 5:11.]
29Sharti wavikwe mabezo wao wanipingiao, soni zao ziwafunika kama nguo![#Sh. 35:26.]
30Na nimshukuru Bwana sanasana kwa kinywa changu! Kwenye watu wengi na nimshangilie!
31Kwani aliye mkiwa humsimamia kuumeni kwake, amwokoe mikononi mwao waliompatiliza.