The chat will start when you send the first message.
1Haleluya! *Namshukuru Bwana kwa moyo wote kwenye mkutano wao wanyokao mioyo nako kwao wateule.
2Matendo yake Bwana ni makubwa, yanachunguzika kwao wote wapendezwao nayo.[#Sh. 104:24.]
3Kazi zenye urembo na utukufu ndizo zake, wongofu wake husimama kale na kale.[#Sh. 148:6.]
4Alifanya ukumbusho wa vioja vyake, yeye Bwana aliye mwenye utu na mwenye huruma.[#2 Mose 12; Luk. 22:19-20.]
5Huwapa vilaji wao wamwogopao, Agano lake hulikumbuka kale na kale.[#Sh. 145:15.]
6Matendo yake yenye nguvu huyatangazia walio ukoo wake, awape nao urithi uliokuwa wao wamizimu.
7Matendo ya mikono yake ni yenye welekevu na yenye wongofu, maagizo yake yote yanategemeka,
8maana yalishikizwa kuwa ya kale na kale, hufanyizwa kwa welekevu na kwa unyofu.
9Walio ukoo wake aliwapatia ukombozi, akaagiza, Agano lake liwepo kale na kale. Jina lake ni takatifu, linaogopesha.
10Kumcha Bwana ndio mwanzo wa werevu wa kweli; huu ndio utambuzi mwema kwao wote wafanyao hivyo. Matukuzo yake husimama kale na kale.*[#Fano. 1:7.]