Mashangilio 126

Mashangilio 126

Utulivu wa mioyo yao waliao machozi.

1*Bwana atakapowakomboa Wasioni waliotekwa akiwarudisha kwao, ndipo, tutakapokuwa kama watu wenye kuota ndoto:[#Sh. 14:7.]

2vinywa vyetu vitajaa macheko, nazo ndimi zetu zitapiga vigelegele. Ndipo, nao wamizimu watakaposema: Bwana amewafanyizia makuu!

3Kweli Bwana ametufanyizia mambo makuu, kwa hiyo twaona furaha.

4Bwana, wakomboe wenzetu waliotekwa ukiwarudisha kwetu, tuwe kama mito ya mchanga iliyojazwa maji na mvua ya vuli!

5Waliomiaga mbegu na kulia machozi ndio watakaovuna na kupiga vigelegele.[#Mat. 5:4.]

6Kweli waliokwenda njia zao na kulia machozi walipopeleka mbegu za kumiaga ndio watakaokuja na kupiga vigelegele wakichukua vicha, walivyovivuna.*[#Yes. 35:10.]

Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.
Published by: Bible Society of Tanzania