Mashangilio 129

Mashangilio 129

Masongano na wokovu wa Waisiraeli.

1Wamenisonga mara nyingi tangu ujana wangu; ndivyo, watakavyosema wao Waisiraeli.

2Wamenisonga mara nyingi tangu ujana wangu, lakini hawakupata kunishinda.

3Walimaji walilima mgongoni kwangu, wakatengeneza kuko huko matuta mazima.[#Yes. 50:6; 51:23.]

4Lakini Bwana ni mwongofu, amezikata kamba zao wasiomcha.[#Sh. 2:3.]

5Sharti watwezwe na kurudishwa nyuma wote wachukizwao na Sioni!

6Sharti wawe kama majani yaliyoko kipaani juu ya nyumba! Miche yao hunyauka ikiwa haijachanua bado.

7Hapo mvunaji hawezi kukijaza kiganja chake tu, wala mfunga miganda hapajazi penye kifua chake.

8Wapitao wasiseme: Bwana na awabariki! Lakini ninyi tunawabariki katika Jina la Bwana.[#Ruti 2:4.]

Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.
Published by: Bible Society of Tanzania